Tetesi: TANESCO yadaiwa kusitisha malipo ya mwezi kwa IPTL na wengineo

Tetesi: TANESCO yadaiwa kusitisha malipo ya mwezi kwa IPTL na wengineo

Status
Not open for further replies.
Leo jioni nikirudi nyumbani nitaomba kwa nguvu zangu zote ili tetesi hii iwe ya uhakika, na kwa yoyote aliyehusika kuunvuja/kusitisha Mungu amtie nguvu aendelee na mapambano.
 
Halafu wajanja waje wazile tena!!

Dawa siyo kusitisha kulipa bali ni kumalizana na IPTL na kuwashughulikia wote waliosababisha hili!! Kusitisha tu bila kufuata sheria kunaweza kutucost zaidi huko mbeleni.

Kwa nini wahusika hawachukuliwi hatua?? Kama JK aliwashughulikia akina Mramba na Yona kwa kulisababisha Taifa hasara vipi hawa wa IPTL na Escrow!!?

Usanii unaendelea hapa!!
kusitisha ni hatua muhimu sana kama ya huko unakotaka kwenda. Subiri mtoto azaliwe ndo ununue nepi mrati tu mimba imeshaonekana usiwe na haraka
 
wasiwasi wangu.

BAADA YA KUSITISHA HAO JAMAA WASIJE KWENDA MAHAKAMANI NA KUSHINDA KESI KISHA TAIFA LIKAINGIA GHARAMA ZA KULIPISHWA MABILIONI YA SHILINGI. NI HAYO TU
na Tanzania kama taifa tuna kawaida ya kushindwa kesi za mikataba ya kibiashara.
 
Mungu Mkubwa, JAMANI Huyu mdudu IPTL hivi atakwisha lini? Rais JPM naomba uanze Kunyonga watu hasa wale waliosaini mkataba wa kuiongezea muda kampuni hii kinyume cha mkataba.

Hili lidudu IPTL ni la nani? kwa nini linaisumbua nchi hivi?

Tena ikibidi JPM Angusha Kombora kwenye mitambo yao tu kama hujuma, tumechoka, nimechoka, bora nchi iwe na mgao kuliko kuwa na hili lidubuwasha
Historia ya Mradi wa IPTL

Makubaliano kati ya Serikali na IPTL kuanzisha mradi wa kufua umeme wenye uwezo wa kuzalisha MW 100 yalifikiwa ili kukabiliana na tatizo la uhaba wa umeme katika miaka ya 1990. Serikali ilialika sekta binafsi kuwekeza katika uzalishaji umeme kwa vile haikuwa na fedha za kugharimia miradi ya umeme.

Kampuni ya VIP Engineering and Marketing Ltd ya Tanzania (VIP) iliweza kuishawishi Serikali kualika Kampuni ya Mechmar Corporation ya Malasyia (MECHMAR).

Baada ya MECHMAR kuonesha kuwa inaweza kuzalisha MW 100 katika Jiji la Dar es Salaam, ilisaini makubaliano (MoU) na Serikali. Mwaka 1994 Kampuni ya MECHMAR na Kampuni ya VIP kwa pamoja zilianzisha Kampuni ya IPTL, kama kampuni binafsi iliyokuwa inamilikiwa na MECHMAR kwa asilimia 70 na VIP kwa asilimia 30.

Kampuni ya IPTL ilipewa leseni ya kujenga-kumiliki na-kuendesha (Build-Own-Operate) mtambo wa kuzalisha MW 100 za umeme wa mafuta mazito katika eneo la Tegeta-Salasala.

Waziri Muhongo anasema; “Mkataba wa kununua umeme kati ya TANESCO na IPTL (Power Purchase Agreement-PPA) ulisainiwa Mei 26, 1995 kwa kipindi cha miaka 20, ingawa utekelezaji wake ulianza mwaka 2002. Katika mkataba wa PPA, TANESCO ndiye mnunuzi pekee wa umeme kutoka mtambo wa IPTL.

“Kulingana na IPTL kutakiwa kuiuzia TANESCO umeme usiopungua asilimia 85 ya umeme unaozalishwa kila siku, pamoja na mkataba huo, Serikali ilisaini mikataba miwili ambayo ni Mkataba wa Utekelezaji (Implementation Agreement) na Mkataba wa Dhamana (Guarantee Agreement), ambako ilikusudiwa kuwa endapo TANESCO itashindwa kulipa gharama za kununua umeme, Serikali ichukue dhamana ya kulipa gharama hizo kwa niaba ya TANESCO.

“Gharama za uwekezaji wa mradi huo zilikadiriwa kuwa dola milioni 150 za Marekani. IPTL walitakiwa kutoa asilimia 30 kama mtaji na asilimia 70 kama mkopo. Makubaliano kati ya wanahisa hao ni kwamba MECHMAR watoe fedha za mtaji na mchango wa VIP uwe huduma muhimu za kuwezesha kuanzishwa kwa IPTL na eneo la kiwanja kitakachojengwa mtambo wa kuzalisha umeme huko Tegeta Salasala.

“Kwa maelezo yote hayo, utaona kuwa Serikali na TANESCO siyo wabia, bali wateja wa kampuni ya IPTL. Hata hivyo, wanahisa wa IPTL (MECHMAR na VIP) hawakutoa asilimia 30 ya mtaji kama walivyotakiwa ila waligeuza fedha za mkopo kuwa mtaji. Kwa lugha nyingine wanahisa hao walidanganyana wenyewe.”

Kwa maelezo ya Profesa Muhongo, baada ya mkataba huo kutiwa saini Februari 4, 1997; IPTL iliingia mkataba wa ujenzi (EPC Contract) na Kampuni ya Wartsila ya Uholanzi. Juni 28, 1997 IPTL iliingia mkataba wa mkopo (Syndication Loan Agreement) na umoja wa mabenki ya Malaysia kwa ajili ya mkopo wa dola milioni 105 za Marekani ikiwa ni asilimia 70 ya mtaji wa IPTL.

Hata hivyo, anasema IPTL walitakiwa kuchukua dola 85,862,022.08 za Marekani kutoka dola milioni 105 za Marekani zilizotolewa kama mkopo.

“Si Serikali wala TANESCO waliokuwa sehemu ya mkataba huo. Mkopo huo ulitakiwa kurudishwa katika kipindi cha miaka minane na riba ilikuwa asilimia 2.5 kwa mwaka. Grace period ya mkopo huo ilikuwa miezi 18. Dhamana ya mkopo ilikuwa kiwanja cha Tegeta ambako mtambo wa kuzalisha umeme utawekwa pamoja na mtambo wa kuzalisha umeme. Mradi wa IPTL ulianza uzalishaji umeme Januari, 2002 na ndiyo utekelezaji wa mkataba ulipoanza,” anasema Profesa Muhongo.

Anasema kulingana na PPA, malipo ya gharama za umeme ambazo TANESCO inatakiwa kulipa ni ya aina mbili — energy na capacity charges. Capacity charge ni gharama za uendeshaji na matengenezo (O&M) pamoja na vilainishi, ambazo zinalipwa hata kama TANESCO haitumii umeme unaozalishwa na IPTL. Energy charges ni gharama za kuzalisha umeme ambazo TANESCO inalipa ikitumia umeme wa IPTL.

Ujenzi wa mtambo ulianza mwaka 1997 na kukamilika mwaka uliofuata, lakini uzalishaji ulianza Februari 15, 2002 (Commercial Operational Date). Mtambo ulichelewa kuanza uzalishaji kutokana na mgogoro kati ya TANESCO na IPTL katika Mahakama ya Usuluhishi ya Kimataifa (ICSID).
 
Jamani hizi kesi si tumekuwa tukishindwa kila tunakokimbilia? Yaani hizi fedha tena wanataka kuziweka kwenye ESCROW account ili waje waseme siyo fedha ya umma? Tunatafuta kuibiwa tena jamani, eeeh Mungu tuhurumie sisi waja wako! Hii nchi sijui ina laana gani! Je, tumejiridhisha kwamba hatujavunja sheria kusitisha hayo malipo? Dawa ya deni kulipa. Kama anataka kufanikiwa awafurushe wote waliohusika na hili dubwasha IPTL, sasa wasiwasi wangu ni ile ahadi yake ya kuwaahidi watu walale usingizi wa pono yeye atawalinda!! Akimalizana na hili dubwasha ahamie kwenye madini, kule nako tunapigwa siyo kidogo, mbugani nako it is not better, kote huko nako tunapigwa!
 
wasiwasi wangu.

BAADA YA KUSITISHA HAO JAMAA WASIJE KWENDA MAHAKAMANI NA KUSHINDA KESI KISHA TAIFA LIKAINGIA GHARAMA ZA KULIPISHWA MABILIONI YA SHILINGI. NI HAYO TU
kwa hiyo unashauri nini??
 
Hapo JPM amecheza vizuri sana, sasa ni kwamba fedha zote ambazo walitakiwa kulipwa hao IPTL zimesitishwa nadhani wanasubiri rufaa iliyokatwa na TANESCO, kama TANESCO wakishindwa kesi basi fedha hizo walipwe Standard charted tu.

huo mtambo wa IPTL utaifishwe tu, nadhani na IPTL wanaweza kuacha kutuuzia UMEME, hapo ndo patamu ili mkataba uvunjwe tu
hala hala hayo malipo yanayositishwa yasije yakaanzishiwa ESCROW nyingine!
 
Kampuni ya Uzalishaji na Usambazi wa Umeme nchini (TANESCO) imesitisha malipo ya kila mwezi kwa kampuni ya kufua umeme ya IPTL na zinazofanana na hizo.

Hiyo inafuatia,pamoja na maagizo toka juu, utata unaoigubika mikataba ya makampuni hayo na hasa katika utekelezaji wake. IPTL imekuwa kiini cha migogoro ihusuyo TANESCO kwa miaka kadhaa sasa.

Mzee Tupatupa wa Lumumba,Dar es Salaam
Maamuzi haya kwa kwetu yanaweza kuwa na faida lkn kumbukeni hawa watu awaingiii mikataba ya kizembe... Naona km tumewapa penalt hawa watu si mnajua wanakwendaga mahakama za huki icc sijui nafikiri lingetazamwa kisheria zaidi maana lisiwe na asari kubwa.... Napenda sana tuachane na hii mikataba ya hovyo lkn jinsi ya kuachana nayo iwe kisheria isilete athari.
 
Mikataba ifumuliwe, tuanze moja au tuitaifishe IPTL mazima!
 
Maamuzi haya kwa kwetu yanaweza kuwa na faida lkn kumbukeni hawa watu awaingiii mikataba ya kizembe... Naona km tumewapa penalt hawa watu si mnajua wanakwendaga mahakama za huki icc sijui nafikiri lingetazamwa kisheria zaidi maana lisiwe na asari kubwa.... Napenda sana tuachane na hii mikataba ya hovyo lkn jinsi ya kuachana nayo iwe kisheria isilete athari.
usiogope kukataa kuibiwa kwa sababu ya kuogopa kusimamishwa kizimbani.
 
Kwa hiyo wamefungua account nyingine ya escrow ?
 
wasiwasi wangu.

BAADA YA KUSITISHA HAO JAMAA WASIJE KWENDA MAHAKAMANI NA KUSHINDA KESI KISHA TAIFA LIKAINGIA GHARAMA ZA KULIPISHWA MABILIONI YA SHILINGI. NI HAYO TU
Hata wakienda mahakani wakashinda kesi
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom