Tetesi: TANESCO yadaiwa kusitisha malipo ya mwezi kwa IPTL na wengineo

Tetesi: TANESCO yadaiwa kusitisha malipo ya mwezi kwa IPTL na wengineo

Status
Not open for further replies.
Daaaah asante sana hawa wanyonyaji......

Magufuli akifanikisha hili nitamuunga mkono kwa Mara ya kwanza......

Sina utani katika vitu ambavyo vilikuwa vinaniuma ni huu mkataba wa kishenzi sana.

Tuungane kupinga hii mikataba ya kulinyonyaji katika taifa letu...

Ingia kote kabisa wafulumushe mafisadi hii nchi waliigeuza shamba lao pekee.....

Na kama wamefanikiwa wapunguze sasa bei ya UNIT moja ya umeme,,,kutoka mia tatu hadi 200.per unit,, na unit 100 kwa watumiaji wa chini kwa mwezi kutoka unit 75 ,,, ,maana iyo mikataba ya kinyonyaji ndio inachangia umeme kuwa expensive
 
Duh! Kagusa huko? Kama kweli mkono wake umefika hadi iptl basi hakuna litakalomshinda nchi hii.
Mkono huo unyooke hadi kule kwenye migodi kwenye ujinga mwingi wa kuandika mikataba yao kimcharazo hadi wanasheria wetu wanashindwa kuisoma na kuielewa.
Nimwombe awafungulie mashtaka ya kutumia nafasi zao vibaya kwa kushindwa kuitetea serikali kwani hawana uzalendo.
Magu fanya kama ya kule Nigeria ili wanasheria wawajibike ipasavyo. Anza na AG kwa kuwapeleka wanasheria mapoyoyo kuitetea nchi.
 
Katika vitu ambavyo nimekuwa naumia ndani kwa ndani ni pamoja na hili dudu la IPTL kama tetesi hizi ni kweli kuna haja watanzania kuungana kwa UMOJA wetu kumsapoti huyo aliyechukua maamuzi haya italeta tabasamu kwa Watanzania
 
Hongera TANESCO kwa hili serikali ikaze kamba kwa hili na hata wakienda mahakamani wakishinda kesi tusiwalipe wameiba vya kutosha.
 
Nadhani itabidi fedha hizo ziwekwe kwenye ESCROW ACCOUNT
Halafu wajanja waje wazile tena!!

Dawa siyo kusitisha kulipa bali ni kumalizana na IPTL na kuwashughulikia wote waliosababisha hili!! Kusitisha tu bila kufuata sheria kunaweza kutucost zaidi huko mbeleni.

Kwa nini wahusika hawachukuliwi hatua?? Kama JK aliwashughulikia akina Mramba na Yona kwa kulisababisha Taifa hasara vipi hawa wa IPTL na Escrow!!?

Usanii unaendelea hapa!!
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom