Tetesi: TANESCO yadaiwa kusitisha malipo ya mwezi kwa IPTL na wengineo

Tetesi: TANESCO yadaiwa kusitisha malipo ya mwezi kwa IPTL na wengineo

Status
Not open for further replies.
Kampuni ya Uzalishaji na Usambazi wa Umeme nchini (TANESCO) imesitisha malipo ya kila mwezi kwa kampuni ya kufua umeme ya IPTL na zinazofanana na hizo.

Hiyo inafuatia,pamoja na maagizo toka juu, utata unaoigubika mikataba ya makampuni hayo na hasa katika utekelezaji wake. IPTL imekuwa kiini cha migogoro ihusuyo TANESCO kwa miaka kadhaa sasa.

Mzee Tupatupa wa Lumumba,Dar es Salaam

Isije ikawa baada ya siku kadhaa akatengua uamuiz wake,lakini mkumbushe pia afilisi zile mashine ni zetu
 
kama ni kweli naanza kunpongeza bwana mdogo zito kwa kulipigia kelele kila siku.
 
Daaaah asante sana hawa wanyonyaji......

Magufuli akifanikisha hili nitamuunga mkono kwa Mara ya kwanza......

Sina utani katika vitu ambavyo vilikuwa vinaniuma ni huu mkataba wa kishenzi sana.

Tuungane kupinga hii mikataba ya kulinyonyaji katika taifa letu...

Ushauri tushushe pia bei ya umeme....

Ingia kote kabisa wafulumushe mafisadi hii nchi waliigeuza shamba lao pekee.....
Kina miraj watalia na mbele ya Magu wataona/pata cha mtema kuni, hana simile na open mafisadi!!!!!!---- waliofaidi kutoka Stanbic.
 
Kampuni ya Uzalishaji na Usambazi wa Umeme nchini (TANESCO) imesitisha malipo ya kila mwezi kwa kampuni ya kufua umeme ya IPTL na zinazofanana na hizo.

Hiyo inafuatia,pamoja na maagizo toka juu, utata unaoigubika mikataba ya makampuni hayo na hasa katika utekelezaji wake. IPTL imekuwa kiini cha migogoro ihusuyo TANESCO kwa miaka kadhaa sasa.

Mzee Tupatupa wa Lumumba,Dar es Salaam
Si kweli kuwa iptl ni kiini cha mgogoro, bali ni chuma ulete la ccm.
 
Mhm maamzi hayo ni magumu lakini hakuna namna ila inabidi kujiridhisha na sheria za mikataba zinasemaje tusije kulipa mara mbili.
Putin mbona alipitia upya mikataba yote ya mangumashi iliyoingiwa na watangulizi wake na sasa Urusi inadunda tu! ? Tunaweza bila kuwezeshwa!
 
Dah!! Afadhali, maana hawa jamaa walikua ni zaidi ya 'Scorpion'.
Ila hii habari haiwezi kuwa faraja kwa sasa hadi nijue tahadhari zilizochukuliwa kisheria.
Tusije tukatumia mabavu na kuishia kutoa hekali nyingine 10,000 kama 'samahani.'
 
Kampuni ya Uzalishaji na Usambazi wa Umeme nchini (TANESCO) imesitisha malipo ya kila mwezi kwa kampuni ya kufua umeme ya IPTL na zinazofanana na hizo.

Hiyo inafuatia,pamoja na maagizo toka juu, utata unaoigubika mikataba ya makampuni hayo na hasa katika utekelezaji wake. IPTL imekuwa kiini cha migogoro ihusuyo TANESCO kwa miaka kadhaa sasa.

Mzee Tupatupa wa Lumumba,Dar es Salaam
Link Jinsi Kampuni ya PAP ilivyoichukua IPTL bure na kujichotea Dola za Marekani 128M kutoka BoT

Link2. Canadian lawyer calls for probe on IPTL

Link3. TANESCO in yet another woe

Link4. Mh Rais naomba tuma mamlaka zako zifanye uhakiki upya mikataba ya madini na biashara nchini
"Aidha, tunamkumbusha Rais kwamba kuna viporo vya ufisadi ambavyo anapaswa kuvishughulikia. Viporo hivi ni pamoja suala la Tegeta Escrow. Bado mtambo wa kufua umeme wa IPTL upo chini ya matapeli na kila mwezi Serikali inawalipa matapeli hao zaidi ya shilingi bilioni 8 (wazalishe au wasizalishe umeme).

Upo pia ufisadi mkubwa kuhusu HatiFungani ya dola za kimarekani 600 milioni (sawa na trilioni 1.3) uliotokea katika Benki ya Standard ya Uingereza. Tunatambua kuwa kuna watu tayari wamefikishwa mahakamani kwa rushwa ya dola 6 milioni (sawa na shilingi 13 bilioni). Lakini Serikali imefikisha mahakamani inaowaita madalali wa rushwa hiyo tu. Walioitoa rushwa hiyo - Benki ya Standard ya Uingereza haipo mahakamani. Waliopokea rushwa hiyo - maafisa wa Wizara ya Fedha na Uchumi hawapo mahakamani. HatiFungani hii ambayo Serikali imeanza kulipa riba yake ni ghali mno na imeongeza Deni la Taifa kwa kiwango cha shilingi 1.3 trilioni bila ya riba. Itakapofika mwaka 2020 ambapo tutakuwa tumemaliza kulipa deni hili, tutakuwa tumelipa zaidi ya shilingi 1.9 trilioni, shilingi bilioni 600 zaidi!

Tunamshauri Rais wetu atuongoze Watanzania kukataa mikopo ya namna hii ambayo inafukarisha nchi. Ni muhimu kabisa TAKUKURU wawachukulie hatua watu wote waliofaidika na bilioni 600 zaidi tutakazolipa katika deni hili. Kwa mifano hii miwili utaona kwamba, pamoja na nia na juhudi kubwa zinazoendelea katika kupambana na ufisadi, bado serikali inapapasa na haijagusa ufisadi ulioitesa nchi kwa muda mrefu, hasa katika kupambana na mafisadi wenyewe. Hadi sasa juhudi za Rais zimeishia kupambana na mawakala wa ufisadi waliopo serikalini lakini bado hajaanza kupambana na mafisadi wenyewe." source link5.

Link5. Hotuba ya Zitto Kabwe kuhusu Hali ya Nchi - Adai Siasa ni Maendeleo
 
Kampuni ya Uzalishaji na Usambazi wa Umeme nchini (TANESCO) imesitisha malipo ya kila mwezi kwa kampuni ya kufua umeme ya IPTL na zinazofanana na hizo.

Hiyo inafuatia,pamoja na maagizo toka juu, utata unaoigubika mikataba ya makampuni hayo na hasa katika utekelezaji wake. IPTL imekuwa kiini cha migogoro ihusuyo TANESCO kwa miaka kadhaa sasa.

Mzee Tupatupa wa Lumumba,Dar es Salaam
wakiamua kuzima mitambo yao na kukimbilia Mahakama ya kmataifa ya uhusuluhi, si tutawalipa mihela kibao. tutakosa hela ya kununua ndege ingine
 
Kabisa mkuu...na nadhani kama kuna usitishaji wa malipo inawezekana kuna kamgogoro ila umma haujawekwa wazi.. Na hyo pesa itawekwa escrow account...mashaka yangu isije ikaja kwapuliwa kama ile nyingine tu...isije ikawa ni hela ya kampeni 2020 inaanza kukusanywa mapema mapema...

Nadhani itabidi fedha hizo ziwekwe kwenye ESCROW ACCOUNT
 
Kampuni ya Uzalishaji na Usambazi wa Umeme nchini (TANESCO) imesitisha malipo ya kila mwezi kwa kampuni ya kufua umeme ya IPTL na zinazofanana na hizo.

Hiyo inafuatia,pamoja na maagizo toka juu, utata unaoigubika mikataba ya makampuni hayo na hasa katika utekelezaji wake. IPTL imekuwa kiini cha migogoro ihusuyo TANESCO kwa miaka kadhaa sasa.

Mzee Tupatupa wa Lumumba,Dar es Salaam
Kampuni ya Uzalishaji na Usambazi wa Umeme nchini (TANESCO) imesitisha malipo ya kila mwezi kwa kampuni ya kufua umeme ya IPTL na zinazofanana na hizo.

Hiyo inafuatia,pamoja na maagizo toka juu, utata unaoigubika mikataba ya makampuni hayo na hasa katika utekelezaji wake. IPTL imekuwa kiini cha migogoro
Isije ikawa ni mihemko ndiyo imewatuma kufanya hivyo. Maana sitegemei kuwa IPTL wanazalisha umeme wa bure. Viwango vya kisheria vinapaswa kuwa vimezingatiwa.!
 
Not to play devil's advocate
ila wamesitisha kwa utaratibu upi? hii ya kufuata maagizo tu isije ikawacost huko mbeleni
Sasa mnataka utaratibu uliotumika wakati mlipiga kelele mkataba huo usitishwe?

Kwani mlivyokuwa mkitaka mkataba usitishwe mlipendekeza njia gani kutumika?
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom