TANESCO yatangaza baadhi ya maeneo katika mikoa 17 itakayokosa umeme kwa siku mbili Oktoba 9 & 10, 2022

ahsante tunawashukuru sana kwa kutoa taarifa.
ni mategemeo yetu kuwa matengenezo yataleta tija kubwa.
 



Kama maofisa waliosoma na kupata kazi kiswahili kinawashinda vipi wanaojifunza kutoka kwetu, na hali ipoje huko mtaani na mashuleni?
 
Dah hapa naamka umeme hamna...

Hii nchi vita ya umaskini ni ngumu sana
 
Haya maboresho siku yakiisha tufanye tambiko.duh!
Preventive Maintenance hainaga mwisho..!! Ukiifikisha mwisho maana yake you are waiting for shutdown of which you will end up doing Breakdown Maintenance (BM). Usisahau, BM ina gharama...!!
 
Kweli mkuu hawasemi ukweli hawa.
Kwenye eneo langu Rau - Kilimanjaro hatuna umeme Toka asubuhi Hadi sasa hivi...!
Kabisa jana rau tumekosa umeme siku nzima wamerudisha karibia saa moja jioni
 
Ndugu zangu
Inafanyika maintenance kwenye line kubwa
Inabidi kua hivyo
Hakuna namana
 
Walianza na Schedule Maintenance, Wakaja mitambo chakavu, wakaja maji kina kimepungua, sijui nini na nini nk.Kwa kifupi wana badilisha magoli.

Kwa kifupi ndugu zangu tuizoee hii hali,tulishawahi kuipitia awamu ya nne,kama mfanyabiashara tafuta Generator kama una uwezo maisha ya endelee, kwa wale msiokuwa na uwezo .........tena ndio mkimbizane nao umeme huu wa kuvizia.

Mama nae hamtoi yupo mpaka 2025 cha msingi tuzoee tuu hamna jinsi.

RIP Magu.
 
Preventive Maintenance hainaga mwisho..!! Ukiifikisha mwisho maana yake you are waiting for shutdown of which you will end up doing Breakdown Maintenance (BM). Usisahau, BM ina gharama...!!
Preventive maintainance karibu 3/4 ya Tanzania kwa wakati mmoja? Very insane.

Hata nchi zilizoathiriwa na majanga kama kimbunga huwezi kuta huu upumbavu unless level of severity ni kubwa mnooo.
 
Ule ujenzi ulikuwa wa kujipatia pesa tu.
Zile pesa zingewekezwa kule Mtwara wajenge vituo vya kufua Umeme, afu umeme utokee huko huko kusambazwa mikoani
 
Labda treni za umeme tuwaachie wenzetu walioendelea, sisi bado.
 
Ni ukame au preventive maintenance? Hawa jamaa hawaaminiki. Utashangaa unaambiwa PM lakini Cha ajabu inakua endelevu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…