TANESCO yatangaza rasmi mgao wa umeme nchi nzima

TANESCO yatangaza rasmi mgao wa umeme nchi nzima

Shirika la Umeme nchini (TANESCO), limetangaza rasmi kuanza mgao wa umeme wa siku 10 kwa nchi nzima ili kuruhusu matengenezo ya mitambo ya kufua umeme kote nchini. Mgao huo utaanza Februari Mosi hadi 10 mwaka huu.

========

TANESCO KUFANYA MABORESHO KWENYE VITUO VYAKE VYA UZALISHAJI UMEME VYA KINYEREZI I NA UBUNGO III

Katika jitihada za kuboresha upatikanaji wa umeme nchini, Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO), linaendelea na maboresho kwenye vituo vyake vya uzalishaji umeme vya Kinyerezi I itakayozalisha megawati 185 na Ubungo III megawati 112.

Akizungumza na wanahabari leo Januari 28, 2022 Mkurugenzi mkuu wa Shirika hilo, Maharage Chande amesema mpaka sasa uzalishaji kutoka mitambo ya Ubungo III umefikia Megawati 60 ambazo tayari zimeunganishwa kwenye gridi ya Taifa.

Amesema kwa sasa kazi ya kupanua kituo cha Kinyerezi I inaendelea na megawati 70 za awali zitaingia kwenye mfumo wa gridi mwezi Aprili 2022 na ifikapo mwezi Agosti 2022 kazi hiyo itakuwa imekamilika na kupelekea Kituo cha Kinyerezi I ambacho sasa kinazalisha megawati 150 kuwa na uwezo wa kuzalisha megawati 335.

‘‘Mitambo hii inayoongezwa ili iweze kuzalisha umeme, inapelekea mahitaji ya gesi asilia kuongezeka ambapo inalazimu kufanya uboreshaji wa mfumo wa gesi kwenye mifumo ya TPDC (Tanzania Petroleum Development Company) na PAET (Pan African Energy Tanzania)’’ amesema Maharage.

Aliongeza kuwa zoezi la uboreshaji litafanyika kwenye visima vya gesi vilivyopo Songosongo kuanzia tarehe 01 hadi 10 Februari 2022, ambapo kukamilika kwake kutahakikisha gesi ya ziada inayohitajika inapatikana.

Hivyo utekelezaji wa maboresho hayo utapelekea mapungufu ya gesi kwenye mitambo ya kuzalishia umeme wa gesi asilia na kulazimika kuzimwa kwa baadhi ya mitambo ili kupisha zoezi hilo muhimu.

Sambamba na matengenezo hayo, hali hiyo itasababisha upungufu wa uzalishaji umeme na kuathiri baadhi ya maeneo, amesema wananchi watapata taarifa za makatizo ya umeme kama zitakavyotolewa na mikoa husika.

Maboresho hayo kwenye vituo vya vya uzalishaji umeme vya Kinyerezi I na Ubungo III yatasaidia kuimarisha hali ya upatikanaji umeme nchini na kupunguza malalamiko ya wateja ya kutokuwa na umeme wa uhakika na unaotabirika.

TANESCO
Sawa watengeneze ila baada ya hizo siku 10 hatutaki kusikia Mgao tena.
 
Kwani stock ya majenereta haikuisha wakati wa JPM?
Hakuna swala la genereta. Mafuta lita 1 ni zaidi 2500 utazalisha nini uwezu kutengeneza faida, ni makampuni machache yanayomudu majenereta
 
Trillions zilizokopwa zikawekwa kwenye bomba la gesi ina maana hazijaleta nafuu yoyote ? Imekuwa ni hasara tupu?!
Hilo mimi silijui. Ila naongelea mabadiliko ya hali ya hewa ambayo kwakweli ni tatizo
 
Watanzania mmejaa lawama hadi kero.
Mliletewa umeme mfululizo bila kukatika tena kwa ada yakuunganishiwa kwa sh 27000 mkasema hamtaki hayo mnataka democrasia.
Leo tena mnalalama. Chui jike, Kikwete, Makamba & co pigeni kazi achaneni na hawa kenge wasionajema!
 
Back in 2019 Arusha umeme haukuwa ukikatika hovyo na siku ukikatika ni haukai sanaa unarudi mpaka nikawa nawadodorishia home ‘Dar… ila sahivi cha moto tunakipata.

Huwa nashindwa kuelewa tunakwama wapi
 
Twenden tukaazime maluteni na na makanali wa jeshi huko BOKINA. FASO N MALI

Hawa waliopo ndio Hawa akina URIO wanaangalia yao yaende s ya wananchi

Kuanzia leo SITAMTUSI MAGUFULI NISAMEHE SANA MAGUFULI NILIKUTWEZA SANA LEO NIMEJIONEA

Sent from my TECNO F1 using JamiiForums mobile app
Kaombe msamaha kwenye kaburi lake.
Nyie ndio mlishiriki kuirudisha hii nchi nyuma.
Mlimsimanga mwendazake na kumzushia uongo na mwisho alipofariki mkafanya sherehe mkagonga mivinyo na kuchoma minyama leo mnalialia nini? Mmeendelea kumtukana hadi akiwa marehemu, Mungu hataacha hili lipite lazima lilipwe.
Tuacheni wanyonge tuendelee kumkumbuka Jembe letu.
Mungu akupumzishe kwa amani JPM
Hakika vita ulipigana. Kumbukumbu lako halitatoka kwetu daima.
 
Kinachokeraa hasa nchi hii ni kitendo cha walio madarakani kudharau wananchi pasi na uoga wowote. Yani wamejiamini kuwa hawawezi fanywa chochote kiasi cha kufanya kila upuuzi bila hata chembe ya hofu.

Watanzania tulivyoaminishwa kuwa amani ni kila kitu tuligubikwa na ujinga wa kufikiria kuwa upumbavu ndio amani yenyewe. Mungu atusimamie.
Na bado 2025 tunaeachagua tena watuongoze. Watanzania kama tuna laana hivi[emoji3064]
 
Wajanja wapo kazini, Majenereta ya TANESCO yanayotumia mafuta yaliyopigwa marufuku enzi za Magufuli nasikia yameshaanza kuwashwa tayari.
 
Back
Top Bottom