Tanga: Adaiwa kujinyonga baada ya kusikiliza Wimbo wa Dear Ex mara 60

Tanga: Adaiwa kujinyonga baada ya kusikiliza Wimbo wa Dear Ex mara 60

"Utamrudia x wako oh, ama bola kufa?..... bola kufa"

Jamaa akaona bola achague kufa kuliko kumrudia x wake.

Kiufupi jamaa kamkomoa x wake.
 
Kama nyimbo ni dk3 na alisikiliza mara 60 ina maana alitumia dk180 ambazo ni sawa na masaa3. Stress is real
 
Watu
Kijana Jumaa Khamisi (32) amefariki dunia mara baada ya kujinyonga katika kijiji cha Kipumbwi Mji Mkuu Wilayani Pangani Mkoani Tanga huku ikihisiwa kuwa chanzo ni stress za kimapenzi kwakuwa Jumaa aliachana na Mpenzi wake na saa kadhaa kabla ya kujinyonga alisikiliza wimbo wa Dear X kwa takribani mara 60 na alipoambiwa inatosha akachukia na kuondoka.

Mwenyekiti wa Kitongoji cha Kipumbwi Mji Mkuu, Mwanaidi Abbasi amesema kabla ya tukio hilo Jumaa alifika nyumbani kwake majira ya saa moja asubuhi kufata vitafunio ndipo baadaye jioni alipopata taarifa za tukio hilo la kujinyonga kwa kijana huyo, “Wakati namwandalia vitafunio aliingia ndani kwangu akawa anaangalia TV na nyimbo ambayo alichagua ni Dear X, alisikiliza kariba mara 60 ile ambayo Msanii inaimba nikimrudia EX wangu bora kufa.”

Kwa upande wake Haji Said ambaye ni Rafiki wa marehemu amesema mara ya mwisho kuachana na Jumaa alimuaga anaenda kupumzika lakini hakumueleza changamoto yeyote ambayo , “Sisi tunadhani chanzo ni mapenzi maana alikuwa na Mtu wake kwakweli wakapanga mipango yao hadi wanamaliza aliingia kidudu mtu kati ndio akakavuruga fulani hivi nadhani hicho ndo chanzo kikubwa.’’

Jeshi la Polisi Mkoa wa Tanga kupitia kwa Kamishna Msaidizi wa Polisi ACP Maketi Msangi amethibitisha kutokea kwa tukio hilo ambapo amesema limetokea October 22,2023 ambapo Jumaa alijinyonga na chandarua kwenye chumba cha mdogo wake hadi kupelea kufariki.”

Hata hivyo Kaimu Kamanda wa Polisi amesema Jumaa alikuwa Mtumiahi mkubwa wa dawa za kulevya kama vile heroin na pombe kali na hivyo Polisi inaendelea na uchunguzi kuweza kufahamu chanzo cha tukio hilo.
Kila mtu anasumbuliwa na tatizo la afya ya akili, isipokuwa viwango vya athari tu ndiyo hutofautiana. Ni vyema pale mtu anapoanza kuonyesha dalili fulani za uwepo wa tatizo, kwa maneno ama matendo akashauriwa mara moja kwenda kumuona daktari.

Matamshi ama matendo ya aina fulani, na tena yanapojirudia mara kwa mara, hudhihirisha kuwa muhusika anahitaji msaada wa kisaikolojia.

Mathalani huyu mtu aliyetajwa hapo juu, imeelezwa ametoka kutengana na mpenzi wake, alikuwa anasikiliza muziki wenye kuendana na hisia kali za maisha ya utengano, kisha akawa unausikiliza wimbo huo mara nyingi mno (X60), hapo ni dhahiri kabisa utengano huo ulimpelekea kuwa na athari hasi za afya ya akili kwake.

Sote tuna wajibu wa kupima afya za akili zetu mara kwa mara. Siyo kwamba ukiwa upo salama kwenye viungo vingine vya mwili mbali ya ubongo ndiyo ujiamini na useme kuwa upo salama katika mwili wako wote. Afya ya ubongo ndiyo muhimu kuliko viungo vyote katika mwili wako.

Afya ya akili ndiyo hutufanya kwa namna gani tuwe "reactive" katika mazingira yetu tunayoishi na hata uamuzi wa kile unachotaka kukifanya. Hata nyuzi tuzitupiazo humu jukwaani pamoja na maudhui ya "reply" zetu hudhirisha athari zilizopo kwa muhusiika 😜
 
Back
Top Bottom