Tanga: Adaiwa kujinyonga baada ya kusikiliza Wimbo wa Dear Ex mara 60

Tanga: Adaiwa kujinyonga baada ya kusikiliza Wimbo wa Dear Ex mara 60

Ukishindwa kuweka balance katika Maisha yako lazima utajiumiza au utaumiza watu .

Ukitaka watu ndo wakupe kitu ambacho wewe unaweza kukipata Bure Kama furaha ,Amani ya moyo na upendo Basi utaishi kwa kutokujua thamani yako na hii ndo karata kubwa waliyonayo wanawake wa Tz wanachofanya wanakufanya kukufanya usijue thamani yako. So tuendelee kujifunza MAARIFA ni utajiri
 
View attachment 2791565
Huduma za afya ya akili hapa kwetu ni kama hazipo; na watu hudhani kuwa mtu kuwa "kichaa" ni mpaka aokote makopo au atembee uchi na kuchokora majalalani. Watu wengi wana msongo wa mawazo, kukata tamaa na wako suicidal lakini hakuna anayejali.

Ishu za mapenzi hizi; na zinginezo mara nyingi ni trigger tu lakini kunakuwa na sababu za ndani ambazo mtu anakuwa amehangaika nazo kwa muda mrefu peke yake gizani bila msaidizi. Halafu akijiua ndiyo tunaanza kumlaumu na hata kumcheka kwamba hakuwa na kifua. Kumbe ni mgonjwa wa akili wa muda mrefu. Sad!
too sad hakika Bro,
mtu mpaka akifikia hatua ya kujitoa uhai hakuamka hapo tu na hilo wazo, lilianzia mbaaali mno,
then anakuja kupata 'trigger' as you said, shida yetu watanzania tupo too judgemental, huwa tunaishia kulaumu matokeo hatujawahi kuwa concerned na chanzo hata siku moja..!!
 
Ngoja namimi niufute huo wimbo kwenye kifaa changu.

Nisije kuusikiliza mara 60 kama mwenzangu then nikafanya maamuzi magumu 😅

Kweli Bongo Nyoso 🙌
 
Mambo km hya kwenye vikao vyetu huwa hayajadiliwi hili ni tatzo lazima mijadala iwe mipana maana changamoto ni nyingi ili fumbuzi ziwe znapatikana mapema sio kuegemea kwenye masuala ya kutuma nauli na mambo za single mother mf:ni muhimu mtu kufahamu nyimbo km hii ya dear x uisikilize mara ngapi! Ili kuepuka mambo km haya.
 
Tajiri na wewe unateswa na mapenzi😁😁
Mapenzi hayaangalii kipato, yakiamua kukutesa yatakutesa hadi ukonde uwe kama namba 1.

Binafsi nashukuru sijabahatika kuteswa nayo, Mungu huwa ananisaidia Mahusiano yangu yote huwa nainjoi tu 🤗
 
#HABARI Jumaa Khamisi (32), aliekuwa mkazi wa kijiji cha Kipumbwi Mji Mkuu Wilayani Pangani Mkoani Tanga amejinyonga mpaka kufa huku chanzo kikihisiwa kuwa ni msongo wa mawazo uliosababishwa na kuachana na mpenzi wake ambapo kabla ya kufanya tukio hilo alisikiliza wimbo wa Dear Ex wa Mario takribani mara 60.
Mwenyekiti wa Kitongoji cha Kipumbwi Mji Mkuu, Mwanaidi Abbasi amesema kabla ya tukio hilo Jumaa alifika nyumbani kwake majira ya saa moja asubuhi kufata vitafunio ndipo baadaye jioni alipopata taarifa za tukio hilo la kujinyonga kwa kijana huyo.
Haji Said ambaye ni Rafiki wa marehemu amesema mara ya mwisho kuachana na Jumaa alimuaga anaenda kupumzika lakini hakumueleza changamoto yeyote ambayo inamkabil.
Jeshi la Polisi Mkoa wa Tanga kupitia kwa Kamishna Msaidizi wa Polisi ACP Maketi Msangi amethibitisha kutokea kwa tukio hilo ambapo amesema limetokea October 22,2023 ambapo Jumaa alijinyonga na chandarua kwenye chumba cha mdogo wake hadi kupelea kufariki
#EastAfricaTvView attachment 2791674
😆😆😆😆
 
Kila wimbo una roho nyuma yake. Yaweza kuwa roho ya furaha, huzuni, mapenzi makali, amani, utulivu, hasira uchangamfu uliopitiliza, kumuabudu Mungu, na hata mauti.
Kuna nyimbo ukisikiliza unapata nguvu za ajabu za kufanya kazi, mwingine unakupa hisia kali za mapenzi, mwingine unakufanya upate huruma sana kama zile za Sarafina. Hizo zote ni roho zilizo nyuma ya nyimbo. Kipindi namsikiliza sana Bob Marley nilikua napata mzuka sana wa kuvuta bangi. It was the spirit behind the songs.
Inasemekana black Americans wengi wanao shoot watu, hukutwa kabla ya tukio alikuwa anasikiliza muziki wa Rap.
Leo tumejua kwamba wimbo wa dear Ex umebeba roho ya mauti hasa kutokana na ule ukiri wa "bora kufa" . Sikiliza at your own risk.
 
Back
Top Bottom