Tanga: Adaiwa kujinyonga baada ya kusikiliza Wimbo wa Dear Ex mara 60

Tanga: Adaiwa kujinyonga baada ya kusikiliza Wimbo wa Dear Ex mara 60

Mtu hajiui kwakua ni kichaa.

Notice hapa

Alivyoambiwa imetosha akachukia akaondoka akaenda kujiua.

Huyu amejiua kisa mapenzi na huo wimbo au kisa kakatazwa kusikiliza wimbo?
 
Mapenzi sometimes ni ufala
FB_IMG_1698206826010.jpg


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Sheikh jumaa ameumaliza mwendo

Angekuja kwangu, kusikiliza Mara 3 tu ningemuambia inatosha
Mara 60 ni nyingi Sana jamani

Wimbo una dakika 3, zidisha mara 60
 
Kijana anayefahamika kwa jina la Jumaa Khamisi (32) mkazi wa wilaya ya Pangani mkoani Tanga, amekutwa amejinyonga kwa kutumia chandarua muda mfupi baada ya kutoka kutazama wimbo wa msanii wa muziki Marioo unaoitwa Dear Ex wenye mashairi yanayosema '...Utamrudia Ex wako ama bora kufa, bora kufa...'.

"Chanzo cha Jumaa kufikia hivyo hakueleza, Chanzo tunachohisi sisi ni mapenzi, alikuwa na mtu wake, wakapanga mipango yao mpaka wamefika kumaliza lakini kuliingia 'mdudu mtu' kati kukawa kama kavuruga" Rafiki wa Marehemu, Miraji Said.

Jeshi la polisi mkoa wa Tanga limethibitisha kutokea kwa tukio hilo, na kusema linaendelea kufanya uchunguzi.

Source : GAD Tv

Je, wakuu nini maoni yenu kufatia kifo cha ndugu yetu hapa ?
FB_IMG_1698210465634.jpg
 
Boraa Kufaaaa 🤣 🤣🤣🤣🤣

Qmmmmk, kafa kweli
 
Kwa niaba ya da donatila , " Hizo nyimbo zina nguvu za kishetani ,na wana miziki wengi wa kidunia wameingia maagano kwenye madhabau za kipepo ,ukiwa hauna Yesu ndani yako lazima shetani akuvae ukizisikiliza hizo nyimbo".[emoji1787][emoji1787][emoji1787]
😂😂😂😂😂😂🙌🙌🙌🙌
Kw upande wako min -me umejifunza nini hapo...?
Unazani kingetokea nini kama angesikiliza mara 90 😂😂😂😂🙌
 
😂😂😂😂😂😂🙌🙌🙌🙌
Kw upande wako min -me umejifunza nini hapo...?
Unazani kingetokea nini kama angesikiliza mara 90 😂😂😂😂🙌
Nguvu ya kusikiliza inaweza kuwa na athari kubwa kwenye utendaji wa mtu kwa njia kadhaa:

1. Kutoa ufahamu bora: Kusikiliza kwa makini husaidia mtu kuelewa na kufahamu habari, maelekezo, au maoni kutoka kwa wengine. Hii inaweza kuboresha uwezo wa kufanya maamuzi sahihi na kuchukua hatua zinazofaa.

2. Kuimarisha uhusiano: Kusikiliza kwa uangalifu inaweza kuimarisha uhusiano na watu wengine. Watu wanapohisi kusikilizwa na kueleweka, wanajisikia kuheshimiwa na wanajenga uhusiano mzuri.

3. Kuzuia makosa: Kusikiliza kwa uangalifu inaweza kusaidia kuepuka makosa au kutoelewa vibaya maelekezo au taarifa. Hii inaweza kuokoa muda na rasilimali.

4. Kujifunza na kukua: Kusikiliza ni njia bora ya kujifunza. Kwa kusikiliza wenzako au wataalamu katika eneo fulani, unaweza kujifunza mambo mapya na kuendeleza ujuzi wako.

5. Kuongeza ubunifu: Kwa kusikiliza kwa makini kwa mitazamo na maoni tofauti, unaweza kuongeza ubunifu wako na kutafuta suluhisho mpya kwa changamoto.

Kwa hiyo, uwezo wa kusikiliza vizuri unaweza kuwa na athari kubwa katika kuboresha utendaji wa mtu katika maeneo mengi ya maisha yao, iwe kazini, shuleni, au katika mahusiano ya kibinafsi.

Sasa apo inategemea wewe una sikiliza nini na afya yako ya akili ina hali gani katika kutafsiri jambo .
 
Kijana Jumaa Khamisi (32) amefariki dunia mara baada ya kujinyonga katika kijiji cha Kipumbwi Mji Mkuu Wilayani Pangani Mkoani Tanga huku ikihisiwa kuwa chanzo ni stress za kimapenzi kwakuwa Jumaa aliachana na Mpenzi wake na saa kadhaa kabla ya kujinyonga alisikiliza wimbo wa Dear X kwa takribani mara 60 na alipoambiwa inatosha akachukia na kuondoka.

Mwenyekiti wa Kitongoji cha Kipumbwi Mji Mkuu, Mwanaidi Abbasi amesema kabla ya tukio hilo Jumaa alifika nyumbani kwake majira ya saa moja asubuhi kufata vitafunio ndipo baadaye jioni alipopata taarifa za tukio hilo la kujinyonga kwa kijana huyo, “Wakati namwandalia vitafunio aliingia ndani kwangu akawa anaangalia TV na nyimbo ambayo alichagua ni Dear X, alisikiliza kariba mara 60 ile ambayo Msanii inaimba nikimrudia EX wangu bora kufa.”

Kwa upande wake Haji Said ambaye ni Rafiki wa marehemu amesema mara ya mwisho kuachana na Jumaa alimuaga anaenda kupumzika lakini hakumueleza changamoto yeyote ambayo , “Sisi tunadhani chanzo ni mapenzi maana alikuwa na Mtu wake kwakweli wakapanga mipango yao hadi wanamaliza aliingia kidudu mtu kati ndio akakavuruga fulani hivi nadhani hicho ndo chanzo kikubwa.’’

Jeshi la Polisi Mkoa wa Tanga kupitia kwa Kamishna Msaidizi wa Polisi ACP Maketi Msangi amethibitisha kutokea kwa tukio hilo ambapo amesema limetokea October 22,2023 ambapo Jumaa alijinyonga na chandarua kwenye chumba cha mdogo wake hadi kupelea kufariki.”

Hata hivyo Kaimu Kamanda wa Polisi amesema Jumaa alikuwa Mtumiahi mkubwa wa dawa za kulevya kama vile heroin na pombe kali na hivyo Polisi inaendelea na uchunguzi kuweza kufahamu chanzo cha tukio hilo.
Huyo jamaa sijamuelewa kwahiyo alikuwa anahesabu mpaka ikafika 60!!
 
Jamaa aliona Kuna dalili za kurudiana na mpenzi wake hivyo kaona bora kufa kuliko kuingia aibu aisee...
 
Na wamejuaje kama kasikiliza Hadi mara sitini (60)?...ina maana Kuna mtu alikuwa anahesabu au marehemu ndo alisema mwenyewe before hajajiua?...maswali ni mengi.
 
Back
Top Bottom