Tanga: Adaiwa kujinyonga baada ya kusikiliza Wimbo wa Dear Ex mara 60

"Utamrudia x wako oh, ama bola kufa?..... bola kufa"

Jamaa akaona bola achague kufa kuliko kumrudia x wake.

Kiufupi jamaa kamkomoa x wake.
 
Kama nyimbo ni dk3 na alisikiliza mara 60 ina maana alitumia dk180 ambazo ni sawa na masaa3. Stress is real
 
Watu
Kila mtu anasumbuliwa na tatizo la afya ya akili, isipokuwa viwango vya athari tu ndiyo hutofautiana. Ni vyema pale mtu anapoanza kuonyesha dalili fulani za uwepo wa tatizo, kwa maneno ama matendo akashauriwa mara moja kwenda kumuona daktari.

Matamshi ama matendo ya aina fulani, na tena yanapojirudia mara kwa mara, hudhihirisha kuwa muhusika anahitaji msaada wa kisaikolojia.

Mathalani huyu mtu aliyetajwa hapo juu, imeelezwa ametoka kutengana na mpenzi wake, alikuwa anasikiliza muziki wenye kuendana na hisia kali za maisha ya utengano, kisha akawa unausikiliza wimbo huo mara nyingi mno (X60), hapo ni dhahiri kabisa utengano huo ulimpelekea kuwa na athari hasi za afya ya akili kwake.

Sote tuna wajibu wa kupima afya za akili zetu mara kwa mara. Siyo kwamba ukiwa upo salama kwenye viungo vingine vya mwili mbali ya ubongo ndiyo ujiamini na useme kuwa upo salama katika mwili wako wote. Afya ya ubongo ndiyo muhimu kuliko viungo vyote katika mwili wako.

Afya ya akili ndiyo hutufanya kwa namna gani tuwe "reactive" katika mazingira yetu tunayoishi na hata uamuzi wa kile unachotaka kukifanya. Hata nyuzi tuzitupiazo humu jukwaani pamoja na maudhui ya "reply" zetu hudhirisha athari zilizopo kwa muhusiika 😜
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…