Mkazi wa Kijiji cha Mafisa mkoani Tanga, Juma Hamisi Msilagi (69) amezawadiwa shilingi 20,000 baada ya kusalimisha kwa hiari silaha haramu aina ya gobore aliyokuwa akiimiliki kinyume cha sheria.Msilagi amekabidhi silaha hiyo kufuatia wito wa kusalimisha silaha haramu uliotolewa na Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Patrobas Katambi katika juhudi za kuimarisha usalama nchini.
Zawadi hiyo imetolewa na Mkuu wa Upelelezi Wilaya ya Kilindi, ASP Mtera ikiwa ni sehemu ya kampeni ya Jeshi la Polisi kuhamasisha wananchi kusalimisha silaha haramu kwa hiari na kushiriki katika kulinda usalama wa jamii.#AzamTVUpdatesMhariri | John Mbalamwezi