Tanga ilitakiwa uwe mkoa wa pili kwa uchumi baada ya Dar Es Salaam

Tanga ilitakiwa uwe mkoa wa pili kwa uchumi baada ya Dar Es Salaam

Kinacho isaidia sana Tanga kwenye stat za mapato TRA ni bandari na mpaka wa kenya ambao ndio unavusha asilimia kubwa ya bidhaa za kenya zinazo ingia Tz na kutoka
Ikizingatiwa kwamba Kenya ndio nchi ya pili duniani tunayofanya nayo sana biashara ukiondoa uchina
Nimeshaweka link juu, hayo mapato Hayamo ama kama yamo ni kwa wafanyabiashara wa hapo hapo, hio figure ya 300B ni ndogo sana uki include bandari ambayo inakusanya kama Bilioni 200.

Tanga kuna maviwanda Makubwa sana unakuta Kiwanda Kimoja Mapato Bilioni 100 ama 200 humo ndio source ya hayo Mapato, Tanga Cement Mara kwa mara inaingia Top 10 ya wa lipa kodi wakubwa Nchi hii,


Bilioni 40 miaka hio kwa mwaka.
 
Bandari ya Tanga iko strategicalky,Tanga juna reki,Tanga ni karibu na arusha,moshi,uganda na nairobi,bagamoyo ni karibu na waoi?
Bandarii ya Tanga ni natural.
Wakoloni hawakua wajinga kuiendeleza Tanga,ipo kimkakati
Handeni panafaa kwa kikimo na ufugaji
Lushoto utalii na kilimo,korogwe panafaa kwa kilimo,utalii pia si haba
Hivi kweli tujenge bandari ya Tanga kwa kuwa Nairobi ipo karibuli!!

Nairobi haiwezi kutegemea bandari ya Tanga vyovyote iwavyo.

Vinginevyo Dar es salaam na Bagamoyo zimekaribiana, miundombinu ya kuondoa shehena kwenye bandari ya Dar ndiyo itakakayotumika kuondoa shehena bandari ya Bagamoyo itakapojengwa. (Kama ipo haja ya kufanya hivyo).

Reli ya Tazara, Reli ya kati na Barabara Kuu zote zipo tayari kuelekea kwenye boda zinazopokea mizigo kwa wingi za Tunduma, Kasumulu, Mnanila
Kabanga, Mtukula na boda nyingine ndogo ndogo za Mabamba, Murusagamba, Ileje, Mbambabay nk.

Mpango wowote wa kupanua gati ya bandari ya Tanga lazima uende sambaba na ujenzi wa miundombinu ya usafirishaji.
Nadhani kwa sasa serikali haiwezi kufanya hivyo, labda miaka ijayo kama kutakuwa na sababu.

Bahati mbaya pia ukanda huo wa kaskazini hauna mazao ya kimkakati kama Shaba, Makaa ya mawe, Chuma nk.
Na pia hakuna jirani kwa sasa wenye mahitaji ya huduma ya bandari hiyo.
Hivyo kuipanua ni kujiingiza kwenye hasara.

Bandari ya kimkakti kwa sasa ni Mtwara.
Makaa ya Mawe, Chuma, Korosho. Mbaazi, Soya Mahindi nk, kutoka mikoa ya ukanda wa kusini na kusini magharibi, vinashawishi kupanua gati ya Mtwara.
Miaka michache ijayo Mtwara utakuwa mji mkubwa wenye shughuli nyingi zitokanazo na bandari hiyo.
Tanga tunaipenda lakini kwa sasa mtatusamehe😂
 
Back
Top Bottom