Tanga: Milioni 21 waliyoiomba Wazee kwa ajili ya Tambiko yakwamisha Ujenzi wa Barabara

Tanga: Milioni 21 waliyoiomba Wazee kwa ajili ya Tambiko yakwamisha Ujenzi wa Barabara

Hii ndio Taarifa mpya kutoka Kijiji cha Kwa Msisi Mkoani Tanga ambapo imeombwa kwanza hela ya Tambiko mil 21 ili ujenzi wa barabara unaohusisha ukataji wa miti uendelee.

Tambiko la pili litafanyika baada ya barabara hiyo kukamilika ambapo wazee watafanya dua maalum. Juhudi za Mkuu wa Wilaya kuomba punguzo zinaendelea.

Habari kamili hii hapa

Wote tugawane keki ya taifa kila inapopatikana fursa
 
Hii ndio Taarifa mpya kutoka Kijiji cha Kwa Msisi Mkoani Tanga ambapo imeombwa kwanza hela ya Tambiko mil 21 ili ujenzi wa barabara unaohusisha ukataji wa miti uendelee.

Tambiko la pili litafanyika baada ya barabara hiyo kukamilika ambapo wazee watafanya dua maalum. Juhudi za Mkuu wa Wilaya kuomba punguzo zinaendelea.

Habari kamili hii hapa

LOoooh, maskini wazee hawajui kitu.

Yaani wamekaa chini na kuona milioni 21 ndiyo hela inayoendana na kazi hiyo muhimu? Kwa nini hawakuifanya iwe 21 bilioni angalawa!

Hivi hawa wazee wanajua jinsi serikali inavyochezea hela za wananchi!

Kwanza wajiulize tu, shughuli zingine za aina hiyo, kama zile za futari na nyakati za Kristmas, ni fedha kiasi gani hutumika huko!
Hawa wazee wanakosa uongozi wa kuwapanua mawazo waendane na hali halisi ya sasa. Bado hawa wazee wanaishi kwenye enzi za Mwalimu Nyerere.
 
Ndio maana kuna wakati tunasema hakuna demokrasia kwa mpumbavu, ona sasa watu wanakosa barabara eti kisa tambiko na mizimu..
Huku ni kukosa akili kwa upande wako, halafu unaona wengine ndio hawana akili.
Kuna kitu gani hapa cha kubeza, hilo tambiko?
Mbona hujahoji matumizi makubwa ya mali za wananchi kwenye shughuli za aina hiyo zinazohusu tamaduni za wazungu au waarabu?
 
Back
Top Bottom