Tanga: Mjamzito adaiwa kufa baada ya kuwekewa damu kimakosa, Watano wasimamishwa kupisha uchunguzi

Tanga: Mjamzito adaiwa kufa baada ya kuwekewa damu kimakosa, Watano wasimamishwa kupisha uchunguzi

Kuna muda unampeleka mgonjwa wako hospital ila ukifika ule wakati daktari anakwambia hebu tupishe tumfanyie vipimo mgojwa unatamani umkatalie ubaki ukitazama ili ukiona walakini umuulize maswali ya msingi kwamba nini kinaendelea hapo, kwann unampa hiyo dawa, kwann unafanya hicho?

Maana madaktari na wauguzi wa sasa wamekuwa kama fundi shabani ukimuachia gari yako inakuwa ndio mwanzo wa magonjwa yasiyokuwa na mwisho.
Hiyo ni haki yako Mkuu..
Someni haki za Wagonjwa According to WHO Mkataba wa Huduma kwa wateja Afya..

Unaruksa kuuliza kila steps na hata kukataa matibabu pia usitishwe ni Haki yako
 
Wauguzi Tanga ni changamoto sana, kuna kituo cha Afya kinaitwa Duga hapo ni mabingwa wa kupoteza vichanga, wajawazito wengi sana wamepoteza watoto pale kwa uzembe wa wauguzi na hakuna hatua zozote zimechukuliwa.
 
Watumishi watano wa Kituo cha Afya cha Mikanjuni kilichopo Jijini Tanga wamesimamishwa kazi kupisha uchunguzi baada ya kufanya uzembe uliosababisha kifo cha Mama mjamzito Fatuma Mussa Suleiman (36) Mkazi wa Magaoni, aliyefariki baada ya kuwekewa damu ambayo hakustahili kupewa na hakuwa na uhitaji nayo kwa wakati huo.

Mkuu wa Wilaya ya Tanga, James Kaji amesema kuwa Mama huyo alilazwa katika Kituo cha Afya Mikanjuni March 27, 2204 saa kumi alfajiri kwa tatizo la uchungu ambapo damu aliyowekewa Marehemu ilikuwa ni ya Mgonjwa mwingine ambaye alikuwa amelazwa kwenye kituo hicho akipatiwa matibatu ambapo baada ya kupatiwa damu hiyo Fatuma alianza kuonesha dalili za Mtu mwenye mzio mkali (Allergic reaction) kisha akafariki.

Watumishi hao waliosimamishwa kazi kupisha uchunguzi ni pamoja na Wauguzi watatu Fadhila Ally Hozza aliyekuwa zamu ya mchana, Restitua Kasendo Deusdedit na Muya Ally Mohamed walioingia zamu ya usiku na pia Madaktari waliomfanyia upasuaji Andrew Eliasikia Kidee na Hamis Mohamed Msami.

“Mgonjwa alifanyiwa upasuaji ambapo alifanikiwa kupata Mtoto wa kike wa kilo 3.4 na hakuwa na changamoto yeyote na baada ya upasuaji na aliendelea kupatiwa matibabu chini ya uangalizi wa Wauguzi na Madaktari wa zamu, katika wodi aliyokuwa amelazwa marehemu kulikuwa na mgonjwa ambaye alikuwa anahitaji kuwekewa damu na damu yake ilikuwa tayari imeandaliwa, Muuguzii aliyekuwa zamu alimuwekea Marehemu damu ambayo hakustahili kupewa na hakuwa na uhitaji huo, baada ya kuwekewa damu marehemu alipatwa na mzio mkali (Allergic reaction) iliyopelekea kifo chake”
Ajira za Connection hizo 😁😁 hivi unaanzaje kumpa mgonjwa huduma ya bt(blood transfusion) bila kufanya kwanza assessment......
 
Ndio maana wanasiasa wakiugua wanakimbilia India, na ulaya, Mambo ya kupasuliwa kichwa wakati una shida ya mguu nani anataka,
Daaahh, hatukujifunza kwenye lile tukio, hatimaye limejirudia tena
 
Sasa vyuo vya nursing vimejaa kila kona uswazi huko na wanaosomea ndio walewale waliofeli lasaba au form four na kukosa option kabisa unategemea nini.

Hilo ndio ambalo limejulikana yapo madhara mengi mahospitalini huko na mamia ya watu wanakufa na wengine kupata vilema.
 
watano wa Kituo cha Afya Mikanjuni wamesimamishwa kazi kufuatia kifo cha mjamzito Fatuma Mussa Suleiman (36) mkazi wa Magaoni Jijini Tanga aliyefika kituoni hapo kwa ajili ya kujifungua na inadaiwa kuwa wahudumu wa zamu walifanya uzembe kwa kumuwekea damu ambayo hakustahili wala hakuwa na uhitaji nayo

Akitoa taarifa ya Serikali, Mkuu wa Wilaya ya Tanga Mhe. James Kaji amesema baada ya kutokea uzembe kwa marehemu kuwekewa damu ambayo hakuwa na uhitaji nayo alipata uzio mkali (Allergic Reaction) na kisha kupelekea kifo chake.

"Mgonjwa alifanyiwa upasuaji ambapo alifanikiwa kupata mtoto wa kike na hakukuwa na changamoto yoyote kwa mama wala kwa mtoto baada ya upasuaji na aliendelea na matibabu chini ya uangalizi wa madaktari na wauguzi wa zamu."

"Katika wodi hiyo alipolazwa kulikuwa na mgonjwa ambaye alikuwa na uhitaji wa kuwekewa damu na ilikuwa tayari imeandaliwa, kwahiyo muuguzi aliyekuwa zamu alimwekea damu marehemu baada ya mgonjwa aliyekuwa anatakiwa kuwekewa damu" amesema DC James Kaji

Aidha, amewataja watumishi waliosimamishwa kazi ili kupisha uchunguzi wa tukio hilo ni pamoja na wauguzi watatu ambao ni Fadhila Ally Hoza, Restituta Kasendo Deusdedit, pamoja na Muya Ally Mhando ambapo kwa upande wa madaktari ni Hamis Mohamed Msami pamoja na Andrew Eliasikia Kidee. #EastAfricaTV
 
Hapo unaweza kuta alikuwa anaongeza damu huka anazungumza na simu "shoga angu... we acha tu"
Pathetic.
 
Back
Top Bottom