Tanga: Mjamzito adaiwa kufa baada ya kuwekewa damu kimakosa, Watano wasimamishwa kupisha uchunguzi

Tanga: Mjamzito adaiwa kufa baada ya kuwekewa damu kimakosa, Watano wasimamishwa kupisha uchunguzi

TANGA: Mkuu wa Wilaya ya Tanga, James Kaji amemuagiza Mkurungenzi wa Jiji la Tanga Dk. Frederick Sagamiko kuwasimamisha kazi watumishi wa afya watano kutokana na uzembe uliosababisha kifo cha mama mjamzito muda mchache baada ya kujifungua.

Amewataja watumishi hao ni pamoja na wauguzi watatu ambao ni Fadhila Hoza, Restituta Deusdedit na Muya Mohamed, madaktari waliofanya upasuaji Andrew Kidee na Hamis Mohamed.

Akiongea na waandishi wa habari Mkuu wa Wilaya ya Tanga James Kaji amesema kuwa Marehemu Fatuma Suleiman (36) alifika katika kituo cha afya Mikanjuni Machi 27 saa 10 alfajiri kwa tatizo la uchungu na baada ya kujifungua ndipo alipoongezewa damu pasipo na uhitaji na kupelekea kupata mzio mkali ambao uliosababisha kifo chake.
 
Unajiuliza mbona sijafanya ngono ila nina ngoma ,kumbe uliumwa ukawekewa damu ya mtu mweny HIV +
Hujui chochote
Acha ujinga wako
Ukiona mtu ameongezewa damu jua hiyo damu imepiwa vipimo sio chini ya saba tena kwa mashine ambayo ni very sensitive

Hata kama ulipata HIV jana inaonesha

Ni mchakato mrefu hadi damu iwe salama mtu apewe sio zoez la siku moja kwamba unatoa hapo hapo na kuwekewa

Ungeuliza wataalamu wapo wengi humu kabla ya kuandika ulicho post

Sent from my Infinix X657 using JamiiForums mobile app
 
watano wa Kituo cha Afya Mikanjuni wamesimamishwa kazi kufuatia kifo cha mjamzito Fatuma Mussa Suleiman (36) mkazi wa Magaoni Jijini Tanga aliyefika kituoni hapo kwa ajili ya kujifungua na inadaiwa kuwa wahudumu wa zamu walifanya uzembe kwa kumuwekea damu ambayo hakustahili wala hakuwa na uhitaji nayo

Akitoa taarifa ya Serikali, Mkuu wa Wilaya ya Tanga Mhe. James Kaji amesema baada ya kutokea uzembe kwa marehemu kuwekewa damu ambayo hakuwa na uhitaji nayo alipata uzio mkali (Allergic Reaction) na kisha kupelekea kifo chake.

"Mgonjwa alifanyiwa upasuaji ambapo alifanikiwa kupata mtoto wa kike na hakukuwa na changamoto yoyote kwa mama wala kwa mtoto baada ya upasuaji na aliendelea na matibabu chini ya uangalizi wa madaktari na wauguzi wa zamu."

"Katika wodi hiyo alipolazwa kulikuwa na mgonjwa ambaye alikuwa na uhitaji wa kuwekewa damu na ilikuwa tayari imeandaliwa, kwahiyo muuguzi aliyekuwa zamu alimwekea damu marehemu baada ya mgonjwa aliyekuwa anatakiwa kuwekewa damu" amesema DC James Kaji

Aidha, amewataja watumishi waliosimamishwa kazi ili kupisha uchunguzi wa tukio hilo ni pamoja na wauguzi watatu ambao ni Fadhila Ally Hoza, Restituta Kasendo Deusdedit, pamoja na Muya Ally Mhando ambapo kwa upande wa madaktari ni Hamis Mohamed Msami pamoja na Andrew Eliasikia Kidee. #EastAfricaTV
Vipi hali ya mgonjwa,aliyetakiwa kuwekewa damu,hali yake iko vipi?Anaendelea vipi?Kwa kutoekewa damu?
 
TANGA:Mkuu wa Wilaya ya Tanga, James Kaji amemuagiza Mkurungenzi wa Jiji la Tanga Dk. Frederick Sagamiko kuwasimamisha kazi watumishi wa afya watano kutokana na uzembe uliosababisha kifo cha mama mjamzito muda mchache baada ya kujifungua.

Amewataja watumishi hao ni pamoja na wauguzi watatu ambao ni Fadhila Hoza, Restituta Deusdedit na Muya Mohamed, madaktari waliofanya upasuaji Andrew Kidee na Hamis Mohamed.

Akiongea na waandishi wa habari Mkuu wa Wilaya ya Tanga James Kaji amesema kuwa Marehemu Fatuma Suleiman (36) alifika katika kituo cha afya Mikanjuni Machi 27 saa 10 alfajiri kwa tatizo la uchungu na baada ya kujifungua ndipo alipoongezewa damu pasipo na uhitaji na kupelekea kupata mzio mkali ambao uliosababisha kifo chake
Aliyeatakiwa awekewe damu, anaendeleaje? Kwa vile hakuwekewa damu.
 
Ndio maana wanasiasa wakiugua wanakimbilia India, na ulaya, Mambo ya kupasuliwa kichwa wakati una shida ya mguu nani anataka,
Huko India ndipo walifanya upasuaji wa nyongo na kusababisha kifo cha shangazi yangu ambaye alienda huko akiwa mzima na kuamua kwenda kucheki afya yake.

Medical negligence ni kila mahali. Ni kama ajali tu!
 
Akiongea na waandishi wa habari Mkuu wa Wilaya ya Tanga James Kaji amesema kuwa Marehemu Fatuma Suleiman (36) alifika katika kituo cha afya Mikanjuni Machi 27 saa 10 alfajiri kwa tatizo la uchungu na baada ya kujifungua ndipo alipoongezewa damu pasipo na uhitaji na kupelekea kupata mzio mkali ambao uliosababisha kifo chake
Wabobezi wanasemaje!?
 
Hujui chochote
Acha ujinga wako
Ukiona mtu ameongezewa damu jua hiyo damu imepiwa vipimo sio chini ya saba tena kwa mashine ambayo ni very sensitive

Hata kama ulipata HIV jana inaonesha

Ni mchakato mrefu hadi damu iwe salama mtu apewe sio zoez la siku moja kwamba unatoa hapo hapo na kuwekewa

Ungeuliza wataalamu wapo wengi humu kabla ya kuandika ulicho post

Sent from my Infinix X657 using JamiiForums mobile app
Kwa watu wasiokuwa makini dogo kama hao!?
 
I think ni Agglutination reactin Probably due to Antigen-Antibody Reaction
Hawa jamaa wangekuwa makini lazima damu ilipoanza kwenda mgonjwa alianza kuwashwa. Hydrocortisone on bedside wangemwahi huyo Mama angepona

All in all Daktari/ Tabibu hana kosa km ikionekana hajaandika mgonjwa aongezewe damu kwenye file bali ni confusion za Manesi.
 
Huko India ndipo walifanya upasuaji wa nyongo na kusababisha kifo cha shangazi yangu ambaye alienda huko akiwa mzima na kuamua kwenda kucheki afya yake.

Medical negligence ni kila mahali. Ni kama ajali tu!
India pia kuna uhuni mwingi plus below quality medicines. Km mtu una hela bora ukatibiwe Marekani though it's very expensive
 
I think Kosa sio La daktari Kosa ni umakini wa Manesi na kuchanganya Mafailu ya Wagonjwa..
Daktari anaandika but anayemuhudumia mgonjwa ni mwingine..

But hakukuwa na Njia yoyote ya kumsaidia hata kama wangetaka Reaction ikishaanza imeanza and hence Death
Inategemea na severity ya reaction. Angeweza kusaidika km Nesi angeweza kutambua reaction mapema na kusimamisha damu isiendelee kwenda na kumpa huduma ya kwanza na kum stabilize
 
Kuna wakati hawa watu wa afya wanazingua sana. Rest in peace Fatuma. Uzembe wa wenye dhamana ya kukusaidia kuishi, wameyakatisha maisha yako.

Kumbuka wewe ni sehemu tu ya wahanga wa huo uzembe.
 
Hawa jamaa wangekuwa makini lazima damu ilipoanza kwenda mgonjwa alianza kuwashwa. Hydrocortisone on bedside wangemwahi huyo Mama angepona

All in all Daktari/ Tabibu hana kosa km ikionekana hajaandika mgonjwa aongezewe damu kwenye file bali ni confusion za Manesi.
Yeah ni kweli kabisa
 
Kuongezewa damu pasipo na uhitaji? Hii taarifa ilitakiwa itolewe na mganga mfawidhi wa wilaya au hospitali mkuu wa wilaya hana uhalali wa kutoa ufafanuzi, kama mtu kaongezewa damu kimakosa hapo kuna mambo mengi yakuchunguza. Mtu aliyejifungua kwa upasuaji hana uhitaji wa damu? Kivipi? Je walichanganya damu ya mgonjwa A akapewa mgonjwa B? je damu iliyotoka maabara ni hiyo hiyo aliyowekewa mgonjwa? je aliyempima group la damu na kutoa matokeo alikuwa sahihi? je aliyechukua sample ni nani? hakufanya makosa? maswali ni mengi haitakiwi kukurupuka kusimamisha watu wasio husika hapo uchunguzi ufanyike. maana sometimes kuna ishu za damu ya mama na mtoto kujimix mambo ya rhesus positive na negative yanaweza kusababisha scenario kama hiyo.
 
Safi na huo ndo ukweli..
Maybe walipoweka walienda Nursung station kupiga story mpaka ikaisha na wakaongeza nyingine You never know
Always unaambiwa kuwa na very close observation ya mgonjwa anayeongezewa damu hasa mwanzo damu inapoanza. All in all tukubali kuwa tumempoteza Mama kwa uzembe wa watumishi wenzetu kufanya kazi kwa mazowea
 
Na huo ndo Ukweli Mchungu mwanzo kabisa ilibidi Kuadmitt nilipoona hii habari..
We Messed up..
We did A grave mistake that cost a life..
Tuombe msamaha kwa wananchi tu
 
Hili ni tatizo kubwa... Watumishi Wana msongo wa Mawazo Ndio , ndicho kinasababisha haya yote... Tuliambiwa Watanzania wengi hawana furaha, haya Ndio Matokeo yake!
 
Scenario yako ni tofauti sana. After all hiyo unayoongelea haiwezi kusababisha reaction na kumuua Mama bali itasababisha Recurrent Pregnancy Losses

Back
Top Bottom