#COVID19 TANGA: Wanafunzi wakimbia shule kisa hofu ya kuchanjwa

#COVID19 TANGA: Wanafunzi wakimbia shule kisa hofu ya kuchanjwa

Leo Rais Wa Jamhuri Ya Muungano Wa Tanzania
Samia Suluhu Hassan Ameongoza Viongozi Wa Juu Wa Serikali
Kuchanjwa Chanjo Ya COVID 19 Aina Ya Johnson And Johnson


Sasa Huko Tanga Wanafunzi Wamekimbia Shule Hasa Hasa Wakihofia Kuchanjwa,Huku Wazazi Wakiwaambia Wasijekuchanjwa Maana
Wataambukiza Wengine Kwa Haraka Sana!!
Mwalim Alipoulizwa Anasema Hali Tete Sana

Wanafunzi Na Watanzania Wapate Elimu

CHANZO: TBC
Ila nimecheka balaa
 
Isije ikawa mnataka tu kutuchafua watu wa Tanga ili tuonekane ndiyo Washaamba!!

Ingawa inawezekana hiyo taarifa ikawa ya kweli maana hata miaka ya 80's tulikuwa tunawaogopa sana watu wenye ngozi nyeupe au magari yenye msalaba mwekundu kwa kuaminishwa eti ni ya wanyonya damu a.k.a Mumian
Ikundigwa itaikane "WASHAMBAA SIO WASHAMBA"
 
Hata Mimi chanjo za mashuleni zote nilikimbia lakini niko safi
 
Watu kumnukuu mtu haina maana ya kwamba hiyo misimamo yao imetokana kwa kumsikiliza huyo mtu tu, mitazamo ya watu wengi kuhusu chanjo inaanzia kwenye mitazamo yao kuhusu hiyo corona yenyewe. Tatizo ni utoaji wa elimu ukiangalia hata sasa ni kiasi gani cha elimu kilichotolewa hadi tuseme maneno ya Magufuli ndio inakwamisha hilo suala la chanjo? Hata waziri Gwajima jana amekiri kiwango cha elimu kinachotolewa ni kidogo.
Watu walianza kuwa serious na corona, barakoa zilianza kuvaliwa na maji tiririka na sabuni vilikuwa vinawekwa kila mahali penye mchangamano wa watu.

Lakini Rais Magufuli alipohutubia taifa kwa mara ya kwanza akiwa Chato baada ya kuwa na taharuki ya vifo vingi na taarifa za watu kuzikwa usiku alituambia kwamba corona si ugonjwa mkubwa kihivyo pia alituonyesha njia ya kupambana nao kwa maombi na nyungu.

Pia alionya watu kuhusu barakoa zinazotoka nje kwamba zinaweza kuwekewa virusi wakati ambapo MSD walikuwa na uwezo wa chini wa kutengeneza barakoa, mara kwa mara alionyesha kufurahia kukutana na umati wa watu ambao hawana barakoa.

Alituaminisha kuwa vipimo vya corona vilikuwa na hujuma maana hata mapapai, mbuzi na oil chafu zilipimwa na kukutwa na corona, hivyo hata takwimu zilizokuwa zinaonyesha ugonjwa kuongezeka kwa kasi zilionekana ni za uongo na hatimaye tukaambiwa ugonjwa umekwisha.

Alituaminisha ugonjwa ulikwisha kwa maombi hata pale ulipoonekana kurudi alikazia msimamo wake uliopelekea kuja kwa ugonjwa wa "changamoto za upumuaji" na nimonia kwa sababu alisema hakuba corona, rejea wataalamu walivyokuwa na lugha gongana kuhusu changamoto hizo, mpaka hali ilipokuwa mbaya ndio alisema waliochanjwa nje walituletea corona ya ajabu ajabu.

Na kupiga msumari, alisema chanjo ni mbaya na kuonyesha hila na nia mbaya za "mabeberu" kutudhuru kupitia chanjo. Hiyo kauli peke yake inatosha kubomoa imani waliyokuwa nayo wananchi juu ya chanjo. Na watumishi wake Prof. Mgaya, Dr. Molel, Gajima(s) and co. walitumia muda mwingi kutuonyesha mbadala wa chanjo na wengine waliiponda chanjo wazi wazi kutokana na maono na mtazamo wa kiongozi wao na uchu wa madaraka.

The Late (if not great) Magufuli was very smart in pushing his agenda, alikuwa anajua namna ya kujenga hoja ambayo wananchi wengi wataikubali, ukweli ni kwamba alichukua njia ambayo watanzania wengi wameikubali na ni ngumu sana kumtoa mtu kwenye hiyo njia regardless ya chochote kitakachotokea.
 
Back
Top Bottom