Waufukweni
JF-Expert Member
- May 16, 2024
- 2,060
- 5,648
Waziri wa Maji Mhe. Jumaa Aweso amewataka wataalamu wa Sekta ya Maji kuhakikisha wananchi wa kata ya Mswaha, wilaya ya Korogwe mkoani Tanga wananufaika vya kutosha na chanzo cha maji cha Mswaha Darajani kilichopo katika kata yao.
Waziri Aweso amesema alipotembelea chanzo cha mradi huo unaotekelezwa kwa sasa na kutegemea kusambaza maji katika maeneo ya Pangani, Handeni, Muheza na Korogwe.
Amesema wananchi katika hilo wapatiwe maji ya kutosha kwani Rais wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan anatambua kuwa Wizara ya Maji inajenga miradi ya kimkakati.
Aidha, amewataka wananchi wa Mswaha kuwa walinzi wa mradi huo katika kuujenga na kuutunza kwa kutochafua mazingira
Waziri Aweso amewataka wakandarasi wanaojenga mradi huo wenye thamani ya zaidi ya Shilingi bilioni 170 kutumia vijana wa eneo hilo kufanya kazi mbalimbali, zenye kuhitaji ujuzi wa juu au wa chini, pamoja na hayo amewasihi vijana hao kuwa waaminifu pale wanapopata nafasi.