Unawatania watani zetu kwa kuwa kule Iringa hamjaathiriwa na mifumo ya manamba wa kikoloni lakini sijui ni kipi kilichopelekea muwe na athari ya mabinti wa huko kuwa wasaidizi wa kazi za ndani huku mijini.....
Well...
UMASKINI ni fikra kabla ya mali....
Hayati JPM(resty easy ) aliwahi kuwasema ndugu zake wasukuma kuwa wao si masikini...pale ambapo mzee mmoja alipodai yeye ni maskini na maswali ya hayati JPM yakamfunua kuwa anamiliki ng'ombe 200....
Kwa hiyo UMASKINI ni fikra tu na wako waitwao MASKINI wa kipato labda kwa kutokuwa na nyumba za kisasa na mengineyo lakini ukweli unabaki ni "mentalities" zao tu.....
Hao wakazi wa Handeni wanapenda tu kuishi katika nyumba za matope na makuti.....
Serikali ya CCM imejenga miundombinu ya barabara na mengineyo ili kurahisisha huduma kwa wananchi sasa kama mwananchi anafanyiwa yote hayo na bado akabaki katika nyumba za udongo na nyasi sijui UMBADILISHE VIPI ?!!
N.B Wengi wa Manamba wa mjerumani walitokea mikoa ya bara ,wangoni ,wakurya ,wanyakyusa ,wanyamwezi , wasukuma ,wabena,waha n.k
Ukitaka kulijua hilo hebu zungukia vijiji vilivyokuwa na mashamba makubwa ya Mkonge(estates) mathalani Mwera ,Sakura ,Mikinguni ,Saadani ,Pangani na kwengineko utamaizi KIZAZI CHA MACHOTARA WA HAYO MAKABILA YA BARA NA WAZIGUA ,WABONDEI ,WADIGO ,WASEGEJU NA WASAMBAA...
#Mtu Hujikomboa Na Kuwa Bora Akitaka Ukombozi Na huo Ubora !!
#JMT milele dumu !