Tanganyika iiombe radhi Zanzibar?

Kitabu hicho kililetwa humu na tukakichambua kuuonyeshea urongo wake wa wazi mchana kweupe!. Mapinduzi ya Zanzibar: Ukweli ni Upi?
P
Pamoja na kukichambua, bado ukweli uliomo kweye vitabu hivyo utabakia kuwa ukweii. Sifa moja kuu ya uchambuzi wa Mapinduzi huwa unategemea mtazamo wa mchambuzi husika na huu ndio utaratibu wa uchambuzi.
 
Pamoja na kukichambua, bado ukweli uliomo kweye vitabu hivyo utabakia kuwa ukweli.
Kwanza nakubaliana na wewe, uongo ulioandikwa kwenye kitabu, utabakia kuwa ndio ukweli mpaka kitabu kingine kitakapo kosoa na kuusema ukweli wenyewe halisi kuukosoa huo uongo.
Sifa moja kuu ya uchambuzi wa Mapinduzi huwa unategemea mtazamo wa mchambuzi husika na huu ndio utaratibu wa uchambuzi.
Naunga mkono hoja, ila uchambuzi wa historia unaotegemea fasihi simulizi kuigeuza fasihi andishi, siku zote una udhaifu wa kuchomekewa urongo!.

Mwandishi Dr. Ghasani hakuyashihidia Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar bali amehadithiwa kwa fasihi simulizi na mashuhuda wa Mapinduzi Matukufu yale, na kuuageuza fasihi andishi akaandika kitabu chenye urongo. Mimi nimekupa fursa ya kusikiliza shuhuda wa Mapinduzi Matukufu yale, na wewe kumsikia kwa masikio yako akielezea ukweli wa Mapinduzi Matukufu yale, wewe utamwamini nani?.

Nakushauri mwamini shuhuda unayemsikiliza kwa masikio yako na sio mrongo aliyesimuliwa urongo, akaandika urongo bila kuwa na uhakika mrongo ni nani kati ya aliyemsimulia, au aliyeandika, anaweza kabisa kuwa alisimuliwa ukweli, lakini mwandishi akaandika urongo kwa malengo yake. Msikilize shuhuda huyu
P
 
Mkuu Mayalla, unaonaje ukaandika na wewe kitabu kitakachoeleza KWELI TUPU za MAPINDUZI NA MUUNGANO?

Nishazisoma bandiko zako kadhaa. Ni wazi kuwa unayafahamu mengi, na umekuwa ukiyawasilisha, wakati mwingine, kimafumbo.

Unaonaje ukiweka kila kitu wazi kwa njia ya kitabu?

Najua wewe ni mtu "mkubwa!" Huogopi.

Mwaka 2016, ulithubutu kumwuliza Amiri Jeshi Mkuu swali ambalo wenzako, pengine wasingethubutu kuliuliza!

Mwaka 2018, ulidiriki kuandika kile unachokiamini ni sahihi bila kujali kuwa kutamkasirisha mkuu wa moja ya mihimili nchini!

Bila shaka, uliyafanya hayo yote kwa maslahi mapana ya Taifa!

Unaonaje ukaandika na kitabu kitakachokuwa na KWELI TUPU, tena bila mafumbo, kuhusu MAPINDUZI NA MUUNGANO?

Ukifanya hivyo, utakuwa umetoa zawadi kubwa sana kwa vizazi vya sasa na vya baadaye!

Tafadhali mkuu, andika kitabu, na usiweke mafumbo! Tafadhali 🙏🙏🙏
 
Kinanachosikitisha ni hao CCM kuuza nchi mchana kweupe kwa waarabu!

lakini si ndio tunaambiwa CCM kwa kupitia vyama vyao viliotangulia ndio waliwafukuza waarabu? Sasa ni kuwa wanawarejesha tu walipowakuta.
 
Viongozi kutoka Zanzibar hata rais wa Zanzibar ndio wanaojua madhara ya kuvunja muungano, hao wengine wanajisemea tu. Zanzibar haijaweza bado kujitegemea kifedha siku wakiweza muungano utavunjika hapo hapo!

kwahiyo Tanganyika ndio inaweza kujitegemea ama?
 
Serikali 1 ✓

Serikali 2 = No

Serikali 3 ✓
 
Kama inaitegemeza Zanzibar sio haba ila haitegemei fedha kutoka Zanzibar.

Sasa kwanini munainyonya Zanzibar? kwanini mpaka leo mnagoma kuipa mgao wake kutoka BOT? kwanini kwa miaka mingi mumekuwa hamuwapi mgao wao wa pato la muungano wa 4.5%?
 
Sasa kwanini munainyonya Zanzibar? kwanini mpaka leo mnagoma kuipa mgao wake kutoka BOT? kwanini kwa miaka mingi mumekuwa hamuwapi mgao wao wa pato la muungano wa 4.5%?
Zanzibar ndio kupe kwa Tanganyika. Jana tu shs trillion 1 zinakwenda kujenga uwanja wa ndege wa kimataifa Pemba na barabara kilometer 800 Zanzibar yote. Fedha hizo zinatoka Tanganyika. Huu muungano hauwafai watanganyika kabisa.
 
Zanzibar ndio kupe kwa Tanganyika. Jana tu shs trillion 1 zinakwenda kujenga uwanja wa ndege wa kimataifa Pemba na barabara kilometer 800 Zanzibar yote. Fedha hizo zinatoka Tanganyika. Huu muungano hauwafai watanganyika kabisa.

acha mihemko mkuu.
 
Serikali 1 ✓

Serikali 2 = No

Serikali 3 ✓
Sawa. Lakini ukweli ni kwamba serikali 3 kiuhalisia ni kuuvunja muungano; itakuwa ni kuthibitisha hatuna nia ya kuungana. Rais wa JMT ataishia kuwa a lame duck president!

Fikiria. Zanzibar hadi leo wanatambua katiba yao ndiyo yenye nguvu juu ya ile ya JMT! Muungano wa kweli unahitaji kukubaliana katiba moja na serikali moja tu. Nje ya hapo tutaendelea kupigiwa porojo za “kero za muungano” zikiambatana na “kamati za usuluhishi” zikitengewa posho za mabilioni ya walipa kodi mazuzu.
 
Muungano ulikuwa 'CIA' project ya kuimeza Zanzibar ndani ya Tanganyika kama njia ya kuua ukomunisti huko Visiwani.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…