Tanganyika iiombe radhi Zanzibar?

Tanganyika iiombe radhi Zanzibar?

Kumbe inasemekana nilijua labda uhakika upo.
Tulichofundishwa shuleni kuhusu Muungano, ni tofauti na ninayoyasikia Sasa!

Inasemekana, Muungano wa Tanganyika na Zanzibar haikuwa takwa la wananchi, bali la Karume na Nyerere, lakini zaidi, Nyerere.

Inasemekana, hata yale yanayoitwa Mapinduzi Tukufu ya Zanzibar, yalikuwa ni mauaji katili, na yaliratibiwa na kusaidiwa, kwa sehemu kubwa, na Tanganyika. Hata silaha zilizotumika kwenye mapinduzi zilitoka Tanganyika.

Inasemekana, mapinduzi hayakulenga kumwondoa Mwarabu, bali Serikali halali kwa lengo la kukiweka madarakani Chama kilichokuwa kikiungwa mkono na Tanganyika.

Inasemekana, tokea mfumo wa Vyama vingi uanze, chama kinachoungwa mkono na Tanganyika kimekuwa kikishinda uchaguzi bila ridhaa ya wapiga kura. Kwamba kishinde kisishinde, lazima kiingie madarakani, maadam tu kinaungwa mkono na Tanganyika.

Inasemekana, hata huu Muungano uliopo kwa sasa si Muungano bali ni Ukoloni. Kwamba Tanganyika inaitawala nchi nyingine kimabavu.

Inawezekana, kama Zanzibar ingekuwa na uwezo, ingeshajitoa kwenye Muungano. Kuenedelea kwake kuwepo kwenye Muungano ni kwa sababu tu inalazimishwa na Tanganyika.

Yameshasemwa mengi na kuandikwa mengi.

Uungwana ni vitendo. Ikiwa hayo yote yanayosemwa ni kweli, basi Zanzibar wana haki ya kuulakamikia Muungano.

Kama ni kweli, nini kifanyike?

Mosi, Tanganyika iiombe radhi Zanzibar kwa yote inayoamini imeitendea Zanzibar ndivyo isivyo, na kwa yale ambayo Zanzibar inailalamikia.

Pili, kura ya maoni iitishwe kwa wananchi wa nchi ya Tanganyika na Zanzibar kuamua juu ya mustakabali wa Muungano.

Tatu, maamuzi ya wananchi yaheshimiwe.
 
kumbuka kuwa Dr. Ghasan amesema kuwa alizungumza na wahsika wenyewe na kuna sehemu kanukuu yaliyosemwa na kuna wakati kaparaphrase.
Japo kila anayejua kusoma na kuandika anaweza kusoma chochote na kuandika chochote, lakini kwa sisi tuliobahatika kusoma fasihi tunakwenda deep zaidi kidogo.
Taarifa zozote ziko za aina 3,
1. Witnessing, kuona, kushuhudia, kuona ni kuamini, kitu unachokishuhudia mwenyewe ndio ukweli.
2. Fast hand news ni taarifa kutoka kwa mashuhuda kuhadithia walichoshuhudia na hapa ndipo spinning zinapoanzia!. Inawezekana walimhadithia mwandishi ndio waliomdanganya, au mwandishi kahadhithiwa ukweli halafu yeye kaamua kudanganya.
3. Second hand news, hiki sasa ndio kitabu, mwandishi hakushuhudia, kaadithiwa na walioshuhudia na yeye kaandika kutuhadithia sisi, hivyo amei transforms fasihi simulizi kugeuka fasihi andishi, siku zote fasihi simulizi ina udhaifu wa accuracy.

Nilichokupa mimi sio cha kuhadithiwa bali unawasikia mashuhuda kwa masikio yako mwenyewe wakiahadithia na sio ahadhiwe mwandishi, aongopewe au aongope kisha aje kukuongepeeni nyinyi kwa kuandika urongo!.

Haya mambo ya urongo kuhusu yale Mapinduzi Matukufu, umeletwa humu urongo mwingi hadi video!.

Ushauri wangu ni maadam mashuhuda wapo na wamehojiwa, mimi nawaaminia hawa niliowasikia kwa masikio yangu na sio kusikiliziwa na kuandikiwa urongo!. Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar: Kumbe Waarabu Hawakufukuzwa! Walikimbia Wenyewe - Mzee Sukari
P
 
Kauli hii ikitoka kwa mwandishi wa habari tena aliyesoma TSJ na kufundishwa na wahadhiri mahiri inafanya mtu afikirie mara mbili. Hivi nasema taarifa wanazotoa waandishi wa habari kama wewe ni za uongo! Kuhusu huyu aliyesimulia kuhusu mapinduzi ambaye wewe nasema nimwamini yeye jee hawezi kusema uongo? Kama Dr. Ghassan anaweza kuwa kasema uongo huyu wako anashindwa nini?
Haya mambo ya urongo kuhusu yale Mapinduzi Matukufu, umeletwa humu urongo mwingi hadi video!.
Huu uongo sio umeletwa Humu bali umeenea maeneo yote kutoka pande zote.
Ushauri wangu ni maadam mashuhuda wapo na wamehojiwa, mimi nawaaminia hawa niliowasikia kwa masikio yangu na sio kusikiliziwa na kuandikiwa urongo!. Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar: Kumbe Waarabu Hawakufukuzwa! Walikimbia Wenyewe - Mzee Sukari
Huu ni msi
mamo na maoni yako na sio ushauri, nami naheshimu ila bado maoni yangu yanabaki palepale kwamba uchambuzi wowote unaofanywa huwa nategemea matazamo na maoni ya mfanyaji.
 
Kauli hii ikitoka kwa mwandishi wa habari tena aliyesoma TSJ na kufundishwa na wahadhiri mahiri inafanya mtu afikirie mara mbili. Hivi nasema taarifa wanazotoa waandishi wa habari kama wewe ni za uongo!
Tena sio ni mwandishi tuu wa habari, bali pia ni mhitimu wa sheria LL.B wa UDSM na wakili wa kujitegemea.

Kinachofanyika kwenye habari na waandishi wa habari ni kile kile kinachofanywa kwenye kitabu na waandishi wa vitabu,
1. Witnessing news za kuushuhudia ukweli mtupu ni pale TV/Radio na online zinapokuwa Mubashara.
2. First hand news ni pale ripota anappkuwekea activities ya kilichotokea
3. Secondhand news ni pale msoma habari anapokusomea kilochotokea na magazeti kuandika kile mwandishi anachotaka.

Mfano mzuri ni hili tukio Je, leo inaweza kuwa ndio ile siku? Ukweli halisi ni upi? Nini hasa kilitokea na kwanini tulijulishwa baada ya siku 5? hivyo possibility ya urongo ipo kwa chochote unachoambiwa kama hujashuhidia mwenyewe kwa macho na kusikia mwenyewe kwa masikio yako.
P
 
hivyo possibility ya urongo ipo kwa chochote unachoambiwa kama hujashuhidia mwenyewe kwa macho na kusikia mwenyewe kwa masikio yako.
Kwa maana hii hatupaswi kuamini chochote unachosema au kuandika na hivyo haina maana yoyote kusoma na kuikiliza unayosema kwani ni uongo au kuna uwezekano mkubwa ukawa ni uongo na hii ni kinyume na maadili ya uandishi wa habari ambao nguzo zake kuu ni ukweli na usahihi (truth and accuracy). Hivyo basi watu wasikuamini kwa unayosema au kuanika.
Kwa maana hiyo pia sisi tuamini kwamba haya yote uliyochangia ni uongo. Ikitokea kuwa hivyo ndivyo ilivyo, nasikitika kwamba tumepoteza muda wetu bure.

Natamani sana isiwe hivyo.

Zawadini
 
Viongozi kutoka Zanzibar hata rais wa Zanzibar ndio wanaojua madhara ya kuvunja muungano, hao wengine wanajisemea tu. Zanzibar haijaweza bado kujitegemea kifedha siku wakiweza muungano utavunjika hapo hapo!
Ndiyo kusema Tanganyika inailea Zanzibar?

Kama ndivyo, Tanganyika imejiweka kwenye nafasi ya baba mwenye huruma au kubwa jingwa?
 
Kwa hiyo john okello alitumwa na akina nyerere au?
Oscar Kambona alikuwa anajua kila kitu.Ilibidi aondoshwe na achafuliwe ili asije kuharibu.Silaha pamoja na wamakonde katili walipitishwa pwani ya Kipumbwi.Victor Mkelo na Mtu mmoja akiitwa Mkwawa Walimueleza Dr Ghassany na kaandika vyote hivyo katika Kwaheri ukoloni ,Kwa heri uhuru.
 
Baada ya nchi ya Tanganyika kukabidhiwa Kwa Kanisa pekee la mitume,Kuna maagano yaliwekwa.Kwanza ni kukamilisha mradi ulioanza zamani wa kumuondosha Sultan na kuifutilia mbali familia ya Bhu Said Zanzibar.Pili kuhakikisha Zanzibar haifurukuti na kuzima Pan Arabism na Islamism lakini pia ukomunist.Huko twendako Zanzibar itakuwa mkoa.Haya mambo yalianzia Berlin,yakaja 1886 na baadaye Heligoland.Himaya ya Ottoman iliwindwa sana na baadaye vita ya kwanza ya dunia ikamalizia kazi.
 
Nilimsikia Muungwana kabla ya muungano akihutubia machogo wenzake kwamba"visiwa hivi vitatusumbua sana huko twendako,ningekuwa na uwezo ningevisukumia mbali baharini" Mwaka 1964 Nini kilitokea kizuri hata akaamua kuviunganisha na Tanganyika?
 
Tulichofundishwa shuleni kuhusu Muungano, ni tofauti na ninayoyasikia Sasa!

Inasemekana, Muungano wa Tanganyika na Zanzibar haikuwa takwa la wananchi, bali la Karume na Nyerere, lakini zaidi, Nyerere.

Inasemekana, hata yale yanayoitwa Mapinduzi Tukufu ya Zanzibar, yalikuwa ni mauaji katili, na yaliratibiwa na kusaidiwa, kwa sehemu kubwa, na Tanganyika. Hata silaha zilizotumika kwenye mapinduzi zilitoka Tanganyika.

Inasemekana, mapinduzi hayakulenga kumwondoa Mwarabu, bali Serikali halali kwa lengo la kukiweka madarakani Chama kilichokuwa kikiungwa mkono na Tanganyika.

Inasemekana, tokea mfumo wa Vyama vingi uanze, chama kinachoungwa mkono na Tanganyika kimekuwa kikishinda uchaguzi bila ridhaa ya wapiga kura. Kwamba kishinde kisishinde, lazima kiingie madarakani, maadam tu kinaungwa mkono na Tanganyika.

Inasemekana, hata huu Muungano uliopo kwa sasa si Muungano bali ni Ukoloni. Kwamba Tanganyika inaitawala nchi nyingine kimabavu.

Inawezekana, kama Zanzibar ingekuwa na uwezo, ingeshajitoa kwenye Muungano. Kuenedelea kwake kuwepo kwenye Muungano ni kwa sababu tu inalazimishwa na Tanganyika.

Yameshasemwa mengi na kuandikwa mengi.

Uungwana ni vitendo. Ikiwa hayo yote yanayosemwa ni kweli, basi Zanzibar wana haki ya kuulakamikia Muungano.

Kama ni kweli, nini kifanyike?

Mosi, Tanganyika iiombe radhi Zanzibar kwa yote inayoamini imeitendea Zanzibar ndivyo isivyo, na kwa yale ambayo Zanzibar inailalamikia.

Pili, kura ya maoni iitishwe kwa wananchi wa nchi ya Tanganyika na Zanzibar kuamua juu ya mustakabali wa Muungano.

Tatu, maamuzi ya wananchi yaheshimiwe.
Hiyo Tanganyika yenyewe iko wapi sasa ?
 
Back
Top Bottom