Kwanza, tume ya pamoja ya fedha ni moja ya kero za muungano. Hivi karibuni zimeshughulikiwa baada ya Rais SSH kuingia madarakani. Kinachoshangaza ni usiri uliotanda na kwanini kuna usiri.
Hakuna usiri wowote isipokuwa ni utaratibu wa kawaida wa Tume zote, hufanya kazi zake in strictly confidential halafu jambo likiisha kamilika ndipo ripoti hutolewa.
Hata uendeshaji wa familia kuna mambo ya wazi kama mambo ya jikoni, sebuleni, kiambazani etc na kuna mambo ya faragha, yale ya chumbani, mfano huwezi kutangazia ulimwengu " Leo tulikuwa busy kutengeneza mtoto", mtatengeneza mtoto kimya kimya, akiisha tengenezeka, pia husemi, bali watu wataona mtu anaumuka, watajua hapa tayari mtoto ametengenezwa, ila siku akizaliwa ndipo unatangazia watu wa karibu ujio wa Mgeni na siku ya Arobaini unapomtoa nje, ndipo unatangazia umma.
Hivyo siku mtoto wa Tume ya Pamoja ya Fedha akizaliwa, tutatangaziwa.
Pili, kwamba, lazima tuwe na serikali 3 nakubaliana nalo. Kwasasa taasisi za muungano ni za Tanganyika kwa kubeba gharama, katika faida kama ajira ni za Muungano.
Hakuna taasisi iliyopo bara isiyo na mbdala Zanzibar. Ikiwa ni hivyo, kwanini taasisi za Bara ziitwe za muungano?.
Sii kweli, Taasisi za muungano ni zile Taasisi za mambo ya muungano ambapo ni Taasisi moja hiyo hiyo iko Bara na Visiwani, mfano BOT, tena muundo wa Taasisi hizi ulipaswa kuwa wa kimuungano, mfano top akitoka upande mmoja, deputy atoke upande wa pili kama ilivyo kwa Rais na VP.
Taasisi za muungano zenye muundo huu ni BOT tuu na Wizara za muungano, Waziri akitoka upande mmoja, naibu Waziri anatoka upandewa pili, This should have been done to Police kuwe na deputy IGP, CDF kuwa na deputy CDF, and do the same kwa Taasisi zote za muungano likiwemo shirika la Posta, TCRA, TCAA, Sumatra etc, tena tumewadhulumu sana Zanzibar kwa miaka yote tangu tumeungana,
Taasisi zote za muungano zinaongozwa na watu kutoka bara pekee as if Zanzibar hakuna watu wenye uwezo huo. this is not fair. . Sasa ni wakati wa kuwa na gavana wa BOT kutoka Zanzibar, CDF kutoka Zanzibar, IGP kutoka Zanzibar
Nakubaliana nawe kabisa na ndio msingi wa kutaka uwepo mpaka.
Hili ni kwa faida ya Watanganyika. Kwa mfano, Tanganyika imebeba gharama zote za muungano
Katika hilo imeibeba Zanzibar 100% na hivyo Zanzibar kwa kupitia Tanganyika ipo vizuri tu
Kwa mfano Zanzibar wanalipa Wazee Pensheni hata kama hawakuwahi kufanya kazi. Si kwamba wana uchumi mkubwa kiasi hicho bali hawana gharama zozote za kuendesha nchi.
Ulinzi na usalama, mambo ya ndani, nje, Wizara na Taasisi za muungano na hata, 4.5% ya pato la Tanganyika , mikopo inayolipwa na machogo , mambo hayo yantosha kabisa kuwa na ziada.
Mgao wa 4.5% sio mgao wa GDP ya Tanzania, bali ni mgao wa fedha za mikopo na misaada kutoka nje.
Na kwenye mikopo, Zanzibar ina haki ya kukopa kwa udhamini wa JMT, lakini sio kweli kuwa wanalipa mkopo huo ni machogo, Zanzibar ikikopa, JMT inawadhamini tuu kwasababu Zanzibar sio nchi, haiwezi kukopa mikopo ya kimataifa, Tanzania ndio nchi, hivyo Zanzibar ina haki ya kukopa ila ni kwa kudhaminiwa na JMT lakini kwenye kulipa huo mkopo, Zanzibar wanalipa wenyewe, ila endapo Zanzibar akishindwa kulipa, ndipo mdhanini anaingilia kati na kumlipia, Zanzibar haijawahi kushindwa kulipa mikopo yake
Hapana, kama ina haki ya kugomea gharama zisizojulikana, je, gharama za kuendesha Wizara ya ulinzi, Mambo ya ndani, Nje na Taasisi za muungano hawajui gharama zake?
Kama hawajui, kwanini kuna formula ya kugawana kodi za Watanganyika ?
Kama hawajui kwanini wanachotewa 4.5% ya pato la kodi za Watanganyika?
Kama hawajui kwanini wanakopa na hakuna formula ya kurudisha bali zigo kwa Mtanganyika?
Kwanini Zanzibar ni wazuri wa kugawana lakini hawajui kuchangia?
Hili la mgao wa 4.5% niliisha lifafanua sio 4.5% ya kodi za Watanzania au pato la taifa, mgao wa 4.5% ni pato la mikopo na misaada ya kimataifa ya kimaendeleo.
Wizara zote za muungano, mfano Mambo ya Ndani, Nje, Ulinzi, etc, zote ndani yake kuna mambo ya muungano,at the same time ndizo be Wizara za Bara. hakuna dermacation za kibajeti kuwa ndani ya wizara ya MFA, Jeshi au Polisi , this sum is gharama za muungano na this sum sio za muungano.
Tuiachie Tume ya pamoja ya fedha iendelee na mchakato chakula kikiiva kitapakuliwa na kuletewa mezani tayari kwa mlo.
Kuna tatizo na Watanganyika kwa bahati nzuri Watanganyika a.k.a Machogo hawajui !
Hakuna tatizo na Watanzania, Zanzibar ni sehemu yetu, na muungano ni kama ndoa, jee unatatizo lolote iwapo mwenza wako atakufaidi kwa namna yoyote?. Kama una upendo wa kweli, mwenza akifaidi, ndio umefaidi wewe!.
Mkiungana wawili nyie mnakuwa wamoja, Tanzania ni nchi moja.
P