Sasa kama hayo unayosema ni ya kweli, kwanza ifufuke hio Tanganyika. Halafu tuweke wazi matumizi na Mapato ya Muungano, ya Zanzibar na Ya Tanganyika ni yepi. Hapo ndio utajuilikana ukweli
Hakuna cha mapato ya muungano, kilichopo ni mapato ya Tanganyika.
Hivi unajua Bajeti ya Zanzibar? Hivi unajua kuwa makusanyo ya kodi Zanzibar kwa siku au mwezi ni madogo kuliko baadhi ya Kampuni nchini.
Unachosema ni kweli, tunaitaka Tanganyika ili isimamie shughuli zake za sasa kama Tanganyika.
Mambo ya Tanganyika ni ya muungano na Tanganyika haina kauli juu yake kwasababu hainonekani japo ipo.
Mfano; kuna mamlaka ya anga Tanzania (TAA) halafu mamlaka ya anga Zanzibar (ZAA)
Kuna sababu gani za Wajumbe wa bodi ya TAA kuwa na Wazanzibar?
Kwanini Wazanzibar wanashughulikia mambo yasiyowahusu! Je, hii ni kwa ajili ya ajira?
Orodha inaendelea
Mamlaka ya bandari Tanzania( TPA), Mamlaka ya bandari Zanzibar (ZPA)
Shirika la viwango Tanzania (TBS), shirika la viwango Zanzibar (ZBS)
Mamlaka ya chakula na Dawa(TDMA), Mamlaka ya Dawa Zanzibar (ZFDA)
Malaka ya usafiri Tanzania (SUMATRA), Mamlaka ya Usafiri Zanzibar
Taasisi ya kuzuia rushwa Tanzania(TAKUKURU), Mamlaka ya kuzuia rushwa Zanzibar
Bodi ya mikopo ya wanafunzi Tanzania( HESLB), Bodi ya mikopo Zanzibar (ZHESLB)
Mamlaka ya mawasiliano Tanzania (TCRA), Mamlaka ya mawasiliano Zanzibar
etc
Hizo ni baadhi tu ya Taasisi, swali la kujiuliza hizi za Taasisi za Tanzania ni za nani kama si za Tanganyika? Ikiwa sivyo zile za Zanzibar ni za nani na zinasaidiaje muungano?
Kumbuka hakuna Mtanganyika anayeajiriwa katika taasisi za Zanzibar
Kuna asilimia 21 imetengwa kwa Zanzibar kwa Taasisi za Tanganyika kwa jina la Tanzania
Lakini pia hizi Taasisi za Tanzania ambazo wamo Wazanzibar wengi kwa asilimia 21% zinagharamiwa na kodi za Watanganyika, Zanzibar haina mchango!
Hapo hazitajwa Wizara zinazogharamiwa na Tanganyika kwa jina la Tanzania
Ikifika hapo Watanganyika na hasa vijana wakiwemo wa CCM wajiulize!