Tanganyika na Zanzibar zinatumia kikokotoo gani kugawana fedha?

Huu muungano natamani apatikane raisi chizi auvunjilie mbali.

Sent from my SM-J250F using JamiiForums mobile app
 
Tuseme Sawa Zanziba inapewa mao wa 4,5%, lakini katika Kuanzishwa Benki yenyewe (BOT) Zanzibar ilitowa Hisa ya 22% ni nyaraka zipo. Sasa Nania anyenyonwa?
 
Juzi nikasikia kuwa kwa zoezi la kuweka anuani za makazi Tanganyika imepewa sh. 1billion kila mkoa na Zanzibar sh. 500,000,000 (nusu bil.) Kila mkoa.
Kwa sasa kuna 'kaubabe flani' kanaendelea lakini kana mwisho, we fikiria idadi ya watu wa znz nzima hawafikii hata wilaya moja ya DSM lkn eti sasa wanapata mgao wote huo!
 
ivyo Hata kwenye meza ya majadiliano wako vizuri sana na ndio maana Zanzibar IPO na Tanganyika imekufa. Watu wa Bara hata kuingia mikataba ya madini Yao wanashindwa kupata faida.
Ktk meza za majadiliano wanachojua hawa watu ni kulalamika tu wanaonewa hawana lolote!
Mngekuwa mko mbali miaka nenda rudi shule zenu ndio zinaongoza kwa division zero, kaeni kimya mnabebwa sana!
 
Tuseme Sawa Zanziba inapewa mao wa 4,5%, lakini katika Kuanzishwa Benki yenyewe (BOT) Zanzibar ilitowa Hisa ya 22% ni nyaraka zipo. Sasa Nania anyenyonwa?
Hivi hiyo BOT mnayoisemea inazalisha sh ngapi kwa mwaka? Ina asset za sh ngapi inazomiliki?
 
Kwanza hakuna Watanganyika - kuna watanzania bara japo kuna Wazanzibar; anzia hapo
Hadi wanaotakiwa kuwa watanganyika watakapoamka. Kumbuka Warioba aliwahi kusema Wazanzibar katika suala la Zanzibar wanakuwa na msimamo mmoja.
Jiulize pia Je fedha zilizokuwa zinapelekwa Chato zilitumia formula gani, labda mama naye anatumia formula hiyo hiyo
 
Tuseme Sawa Zanziba inapewa mao wa 4,5%, lakini katika Kuanzishwa Benki yenyewe (BOT) Zanzibar ilitowa Hisa ya 22% ni nyaraka zipo. Sasa Nania anyenyonwa?
Sijui kama unajua hesabu
Kwanza, ukisema ilitoa kiasi hicho kuna maswali mengi.
Zanzibar inachangia nini katika kuendesha Wizara na Taasisi za muungano kuanzia wakati huo
Hivi unadhani Jeshi, Polisi n.k. vinajiendea tu, na gharama hizo unaziingiza wapi

Pili, Mishahara ya Zanzibar kwa miaka mingi sana imetoka Hazina Dar es Salaam, kawauliza Marais

Tatu, unajua ni kiasi gani bajeti ya Zanzibar inafidiwa na Tanganyika

Nne, hiyo 4.5% ni ya pato la Tanganyika si ya kuanzisha BoT.

Niishie hapo, nakusihi ukae kimya maana wewe ni wale wa vijiweni wa ''nchi ya kwanza kuwa na TV' ukimaliza hadithi unaingia baharini kujisetiri!
 
Hapo kwenye ajira ndo kuna shida inabidi zile taasisi za muungano ndo iwe hivyo ila hizi tasisi zisizokuwa za muungano zibaki kwa wabara. Lakini saiv ni tofauti wazenji wameajiriwa mpaka halmashauri

Sent from my SM-J250F using JamiiForums mobile app
Wazenj wote pia ni Watanzania wana haki zote za uraia wa JMT kama raia wengine wowote, ila Sisi Watanzania bara ndio hatuna haki Zanzibar.
Ajira, kumiliki ardhi, kuoa, etc, zote ni halali yao.
P
 
Huu muungano natamani apatikane raisi chizi auvunjilie mbali.

Sent from my SM-J250F using JamiiForums mobile app
Atakaeonyesha dalili ya kuvunja atapotelea kusikojulikana. Muungano huu umetia matatani wengi. Tanzania hii hakuna mkubwa kuliko muungano huu. Tukazane TU kuondoa kero ndogondogo TU za muungano. Hata kule kule Hispania wale wa waCataluhna (katalunya) nyumbani kwao Barcelona walijaribu kufanya ulevi wa kutaka kujitenga wakakiona chamoto, Kashmir kule India wanakiona Cha moto, Ireland kule UK, Taiwan, Hongkong na Tibet kule China wanahangaika bila mafanikio. Kuna majimbo kule Marekani kama California, Texas wanaona ni heri wawe huru lakini ni kama wanaota ndoto ya mchana. Mkuu muungano Haina demokrasia, ondoa mawazo ya kuuvunja muungano huu maana ni ngumu kuliko tembo kupanda juu ya mpapai.
 
Wazenj wote pia ni Watanzania wana haki zote za uraia wa JMT kama raia wengine wowote, ila Sisi Watanzania bara ndio hatuna haki Zanzibar.
Ajira, kumiliki ardhi, kuoa, etc, zote ni halali yao.
P
Pascal umesema kweli, lakini hili tatizo mumelisababisha nyinyi. Ifufueni Tanganyika yenu
 
Hivi hiyo BOT mnayoisemea inazalisha sh ngapi kwa mwaka? Ina asset za sh ngapi inazomiliki?
Wewe unajua BOT ililianzishwaje? sasa nakuueleza. Wakati wa East Africa Community Zanzibar ilikuwa mwanchama na Tanganyika Pia. Wakati ilipovunjika ndipo ulipoanzishwa Muungano. Pesa zilizokuwepo kwenye Benki ya East Afrika ziligawiwa kwa wanachama wote na Zanziba ilipata zake na Tanganyika ilipata zake. Nyerere alizichukua za Zanziba na Za Tanganyika ndio akaanzisha Benki kuu . Nyaraka zipo na Zinajuilikana Pesa za zanziba zilikuwa Pound Steling ngapi kwa wakati huo. Kwenye kuanzisha hio benki yenyewe Pesa za Zanzibar zilikuwa 22% ya Pesa zote zilizoanzishiwa BOT.
 
Sijakukatalia vyote. Swali language je BOT ina miliki nini Na nini? Faida yake kwa mwaka je ni tsh ngapi? Hayo ndiyo maswali yangu. Asilimia ishirini huo ni mtaji. Na je fedha zote mnazopewa tunapokopa ila Tanganyika tunalipa zimefika sh ngapi?
 
Wengine tumechoka kuonewa halafu malalamiko watoe wengine.
 
Nafikiri sisi watanganyika ni wajinga. Ipo siku ujinga utatuisha. Hawa watu wanatutawala toka enzi za Seyyid Said. Inakera tunawachangia halafu wanatuona mazuzu. Tuwape vihela vyao halafu tuwaambie ondokeni waende kwa hao waarabu wao. We want our identity of or else we all loose our identity
 
Punguza hasira kwenye hili, na uelewe basi kuwa hata kule Zanzibar watu wanaofikiria kama hivyo unavyofikiria wewe wapo pia, tena sio wachache, lakini wale wanaofikiria muungano uvunjike ni wale wasiochangamkia fursa za muungano, wale wa chips mayai na urojo baasi.

Dunia yote sasa hivi inatafuta njia za kuungana kuwa wengi walioshikana sio kutengana. Unaposikia Marekani ni muungano wa nchi 51. unapo sikia Uingereza ni muungano wa nchi nchi zisizopungua 3 kama sikosei, kuna EU, nk. Tanganyika bila Zanzibar ni ngumu kuilinda kutoka upande wa baharini. Faida kubwa kupita zote Tanganyika inayopata kwenye Muungano ni kujilinda dhidi ya Alshababu, Islam State, wa Wazungu ambao tunapakana nao kwa njia ya bahari.
 
Zanzibar hakuna chochote wanachochangia kwenye muungano. Sisi bara ndio tunaojipendekeza kwao. Ni kama tumewafuga. Kwa hiyo tunawalisha. Siupendi muungano hata nusu. Viongozi wa Tz mambo mengi hayako wazi,ila muungano umezidi. Hauko wazi
 
Nadhani wanatumia CASIO , citizen ni mbovu sana na zipo feki nyingi mno kutoka china
 
Zanzibar hakuna chochote wanachochangia kwenye muungano. Sisi bara ndio tunaojipendekeza kwao. Ni kama tumewafuga. Kwa hiyo tunawalisha. Siupendi muungano hata nusu. Viongozi wa Tz mambo mengi hayako wazi,ila muungano umezidi. Hauko wazi
Hata wewe kuna mambo mkeo hayajui, hauko wazi pia. Walioziunganisha Tanganyika na Zanzibar hawakuwa mazuzu kama unavyota kufikiria, kuna jambo kubwa lenye manufaa kwa pande zote mbili kwa wakati huo wa kuungana ambalo liliwasukuma watu wa pande zote kukubali muungano wa aina hii. Na nafikiri huenda mchakato wa muungano ili kufikia mwisho kabisa ilikuwa kuwa na Tanzania moja (Tan(Tanganyika Zan(Zanzibar) (a)) ndio maana hizi kero zinaonekana ni nyingi. Lakini kama Nyerere na Karume wangekuwa hai wote hadi mwaka 1977 huenda tungekuwa na Tanzania moja tu au tungekuwa serikali tatu au tungekuwa na Tanganyika na Zanzibar kama nchi mbili tofauti. Siri iko hapo na hakuna sasa hivi anaesema ukweli juu ya vision na mission ya Nyerere na Karume ilikuwa ni muungano wa aina ipi walikusudia na walikwama wapi na ni nani alikwamisha kwasababu zipi na kwanini huu wa sasa una kero na maswali mengi. Hizi sababu wanazotoa kujibu swali la kwanini kuna Zanzibar na hakuna Tanganyika ni sababu za kijinga kabisa kusema kwenye kizazi hiki cha sasa kilichoelimika sana, majibu ya hivi yanawatia vijanana wa sasa kuyasikia. Ni heri wakatoa majibu ya kweli ili watu na historia vikae sawa kuhusu taifa lao
 
Umepanick mzee?. Ndio nyie mnafaidika na muungano. Hakuna mahala nimekuambia walikuwa mazuzu kama unavyofikiria. Na tayari hata wewe umesema kuna jambo kubwa lenye manufaa kwa pande zote mbili “KWA WAKATI HUO”.

Hatuko nyakati hizo sasa zilizokuwa za kufikiria maadui wataingilia huko na Zanzibar kwamba ilikuwa haina nguvu kijeshi. Kifupi Kwa sasa Zanzibar wanahitaji kujitawala wenyewe sasa,hawahitaji huo muungano na Tanganyika pia hatuhitaji huo Muungano ksbb tuna uhakika unatunyonya kwa mambo mengi (nimesema kifupi).

Isitoshe Zanzibar mkiwaachie wajitawale wenyewe wangekuwa mbali sana kimaendeleo ksbb wasingekuwa tena na siasa hizi za bara za kipumbavu kuiba kura,kupitisha mtu kinguvu ambae hajachaguliwa na watu. Hayo mambo ya Jecha kufuta uchaguzi sijui,mmewafundisha nyie walafi wa madaraka kutoka bara
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…