Tangawizi, limao, apple vinegar na vitunguu swaum vimeniletea shida

Tangawizi, limao, apple vinegar na vitunguu swaum vimeniletea shida

Mbunifu 11

Senior Member
Joined
Mar 20, 2015
Posts
104
Reaction score
52
Hbr zenu wakuu,

Nisaidieni kuelewa haya yaliyonikuta; leo nimeamka asubuhi nikachemsha tangawizi kali, kiasi cha kikombe kile kikubwa then nikachanganya na vitu vifuatavyo nusu limao na apple vinegar kiasi cha kijiko kimoja cha chakula nikanywa halafu nikachukua punje 8 zile nene za vitunguu swaumu nikavikatakata nikanywa kwa kusukumizia maji kidogo, jamani jamani baada kama ya dk 40 nimejisikia vibaya sana yaani kama vile nikawa nawasiwasi iliyopitiliza halafu siwezi kutulia, pia nikawa mdhaifu ghafla na kakizunguzungu kwa mbaliii, yaani kama nimelewa hivi halafu pumzi nikawa nahisi kama inabana kwa mbaliii.

Haraka nikanywa maji mengi kidogo nikajisikia afadhali ingawa ingawa ka udhaifu ka Mwili nakahisi kwa mbalii bado kapo hii ni mini jamani? Au huo mchanganyiko haufai kiafya?
 
Kawaida vitunguu swaumu na tangawizi vina tabia ya kuongeza kasi ya mzunguko wa damu, pia zina interact na baadhi ya dawa, hapo ungeenda kupima hata pressure yako ingeonyesha iko juu, usisikilize baadhi ya shauri humu JF kama lengo lilikuwa ni kuongeza nguvu za kiume, tutakupoteza wakati bado kijana mdogo.
 
Back
Top Bottom