Tangazo la kifo cha Benjamin Mkapa, Kurungenzi ya Mawasiliano Ikulu lawamani. Inahitaji kusaidiwa kumsaidia Rais - Jicho Letu Ndani ya Habari

Huwaga unakuwa na Point za kisomi sema tatizo wajumbe wengi wa CCM hawana elimu wao hawajui chambua code kabisa.

Nafasi nzuri ni Mzee baba akuteuwe ndo waeza julikana
Huyu nakuapia hata akiteuliwa akae yeye kuandaa mambo km hayo hataweza. Hapa yuko katika kujipendekeza lkn akishateuliwa akili zote zinapuputika. Rejea Mr Slowslow kabla na baada ya teuzi.
 
Mimi naona wangesubiri kukuche ndo watangaze maana hata aliyechukua hyo video ilikuwa na Giza Giza, Pasco umetoa ushauri mzuri.
 
Aliyefariki aliwahi kuwa rais wa Tanzania, kitendo cha serikali kutoeleza chanzo cha ugonjwa wake kinatoa mwanya wa kupokea taarifa zisizo rasmi za ugonjwa wake kwa hiyo tutegemee kila uzushi kuanzia sasa
 
Kwa sisi tuliofuatilia kwa Radio tangazo la Msiba wa Sokoine, tukaona tangazo la Msiba wa Mwalimu na Omar, tukaja tukamsikia JK akitangangaza msiba wa Kawawa, tunaungana na Mayala.

Juzi Tangazo limetoka kiwepesi na muda mbaya sana.
 
Paschal Mayalla sheria imevunjwa na mapungufu ya tangazo lile siyo flaws ndogondogo kama unavyosema hapo.

Rais katangaza kifo cha rais mstaafu kama vile anatangaza kifo cha msela wake tu kafia bar.

So sad
Siku inakuja mazishi yake mtangazaji yanaweza kufanana kama ya mbwa wa joshua nasari.
(fasihi imehusika)
 
Pascal Mayalla,

Hapo mtamlaumu bure huyo muandishi wa habari wa rais, nimjuavyo rais wetu huwa anafanya mambo mengi bila utulivu, wala kusubiri ushauri. Toka mwanzo awamu hii iingie madarakani, rais wetu ameonyesha ni mtu anayependa kufichaficha mambo, ndio maana anadhibiti vyombo vya habari. Kwa vyovyote vile yeye ndio atakuwa amegoma kutaja hospitali, na sababu ya kifo. Hata Mangula alitibiwa kwa usiri mkubwa.

Hizo ni tabia binafsi za rais, na huwezi kumpangia. Hivyo naamini kabisa, hiyo taarifa ameelekeza iandikweje kwa zaidi ya 90%, tena huenda hata alikuwa hasomi popote, bali kasema toka kichwani. Rejea anavyotoa taarifa nyingi kwa kukariri, anaweza kuwataja hata watu 10, na kutoa wasifu wao fulani fulani, ili kujenga taswira kuwa ubongo wake uko vizuri. Sasa mtu wa hivyo atahitaji kuandikiwa tangazo la kifo kwa huo mlolongo wenu? Na huyo Msigwa anaweza kumpangia cha kuongea, kama kina Kabudi na uprofesa wao wanaitwa wapumbavu? Tatizo liko kwa rais mwenyewe. Usimlaumi dobi, Kaniki ndio rangi yake.

NB: Bora leo hujatokea kwenye hicho kipindi maana ungefika ukiwa mwanaccm rasmi, baada ya kujificha muda mrefu.
 
Tatizo bwana yule mambo yake mengi hana haraka hata kama hana sababu za msingi za kuharakisha ukweli msiba wa Mkapa umetangazwa kana kwamba aliyekufa ni mjumbe wa Nyumba Kumi...yaani Mkapa aliyekua Rais wa Nchi amezidiwa hata na Ruge
 
Baada ya kukosa teuzi umeanza zile mada zako halisi sio zile za kusifu na kuabudu
Huyu ndio Pascal Mayalla ninayemfahamu. Na kwa chokochoko hizi ni kama vile anatamani kutaja chanzo cha kifo cha mzee katika ile thana ya JF tuna right ya kuwa wa kwanza kupata habari lakini anaogopa.... lakini JK anasema Mzee Mkapa alikuwa analalamika tumbo linamuuma. Labda Rais wetu Kipenzi chetu sisi wanyonge atatuambia sababu ya kifo siku ya mazishi.
 
Kila kitu anafanya siri...ama kweli ukizoea kua muongo huwezi kuanika jambo lolote lazima utaficha
Unaweza kudhani aliamshwa usingizini na kuanza kutoa taarifa bila maandalizi yoyote! Nilishangaa sana kuona taarifa haitaji jina la Hosp.

RIP Mzee Mkapa
 
Kwa mara ya kwanza mkuu umeongea point sana japo kuna elements za kujipendekeza pia.

Nilipoliona kwa youtube lile tangazo kama layman kwenye tasnia ya khabar kwa kweli nilikua najiskia kama aibu maana maneno yalikua kama hayajapangiliwa vile. Yaani kama anaongea tu kawaida kawaida.

Hiyo number 6 hapo juu mmmmh. Labda mkiambiwa sababu mtaanza kuzua taharuki sijui lkn. Ila unafikiri Mungu hajui hata kama sisi tunafichwa?! Mi kwa maoni yangu kutokana na mitazamo ya sirikali yetu ktk baadhi ya mambo naona wako sahihi kivyao vyao lkn. Sisi tukaaage mwili na tuzike tu. Mengine, Wallah Aa'lam wadigo wenyewe wanakuambia.
 
Ukiona jinsi Mkapa na sumaye walivotangaza musiba wa Nyerere Tena kavaa official na wimbo wa taifa ukapigwa ilionyesha u serious wa tukio Mimi kuona mheshimiwa anatangaza ya Mkapa I thought was a joke kwa kweli,hyo kurugenzi wajiangalie
 
Bujibuji,

Hata huo nao ni ugonjwa mkuu, na unauwa pia.

Sote hatuwezi kufa kwa sababu au kutokana na ugonjwa mmoja japo pia wengi wengine tutaondoka kwa sababu au magonjwa yanayofanana. Yote ni mola peke yake.

Ugonjwa wa kumwua mtu hauchaguliwi kama wanavyochaguliwa watia nia wa Kawe.
 
Mkuu P nadhani walilinda hiyo habari isisambae mana siku hizi wajuzi tupo wengi just imagine ingetangazwa na kigogo2014 na auongezee kwa kusema jiwe amemuuwa Bwm. huu ni ulinzi
Yani kigogo ndo wamuogope hivo sidhani!!
 
Mnamuonea tu mh. Rais, naye ni binadamu kama wengine,ana moyo wa nyama,ukute baada ya kupata taarifa za msiba,alilia weee...uchungu ulivyopoa ndio akatangaza msiba kwa umma,utawaza contet saa ngapi?body language yake tu inaonyesha mwili hauna ushirikiano kwa mshituko.kuna wappuuzi wanasema alikuwa anamgegeda jane. Hii nchi hii!!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…