Tangazo la kifo cha Benjamin Mkapa, Kurungenzi ya Mawasiliano Ikulu lawamani. Inahitaji kusaidiwa kumsaidia Rais - Jicho Letu Ndani ya Habari

Tangazo la kifo cha Benjamin Mkapa, Kurungenzi ya Mawasiliano Ikulu lawamani. Inahitaji kusaidiwa kumsaidia Rais - Jicho Letu Ndani ya Habari

Huwaga unakuwa na Point za kisomi sema tatizo wajumbe wengi wa CCM hawana elimu wao hawajui chambua code kabisa.

Nafasi nzuri ni Mzee baba akuteuwe ndo waeza julikana
Huyu nakuapia hata akiteuliwa akae yeye kuandaa mambo km hayo hataweza. Hapa yuko katika kujipendekeza lkn akishateuliwa akili zote zinapuputika. Rejea Mr Slowslow kabla na baada ya teuzi.
 
Mimi naona wangesubiri kukuche ndo watangaze maana hata aliyechukua hyo video ilikuwa na Giza Giza, Pasco umetoa ushauri mzuri.
 
Aliyefariki aliwahi kuwa rais wa Tanzania, kitendo cha serikali kutoeleza chanzo cha ugonjwa wake kinatoa mwanya wa kupokea taarifa zisizo rasmi za ugonjwa wake kwa hiyo tutegemee kila uzushi kuanzia sasa
 
Kwa sisi tuliofuatilia kwa Radio tangazo la Msiba wa Sokoine, tukaona tangazo la Msiba wa Mwalimu na Omar, tukaja tukamsikia JK akitangangaza msiba wa Kawawa, tunaungana na Mayala.

Juzi Tangazo limetoka kiwepesi na muda mbaya sana.
 
Paschal Mayalla sheria imevunjwa na mapungufu ya tangazo lile siyo flaws ndogondogo kama unavyosema hapo.

Rais katangaza kifo cha rais mstaafu kama vile anatangaza kifo cha msela wake tu kafia bar.

So sad
Siku inakuja mazishi yake mtangazaji yanaweza kufanana kama ya mbwa wa joshua nasari.
(fasihi imehusika)
 
Pascal Mayalla,

Hapo mtamlaumu bure huyo muandishi wa habari wa rais, nimjuavyo rais wetu huwa anafanya mambo mengi bila utulivu, wala kusubiri ushauri. Toka mwanzo awamu hii iingie madarakani, rais wetu ameonyesha ni mtu anayependa kufichaficha mambo, ndio maana anadhibiti vyombo vya habari. Kwa vyovyote vile yeye ndio atakuwa amegoma kutaja hospitali, na sababu ya kifo. Hata Mangula alitibiwa kwa usiri mkubwa.

Hizo ni tabia binafsi za rais, na huwezi kumpangia. Hivyo naamini kabisa, hiyo taarifa ameelekeza iandikweje kwa zaidi ya 90%, tena huenda hata alikuwa hasomi popote, bali kasema toka kichwani. Rejea anavyotoa taarifa nyingi kwa kukariri, anaweza kuwataja hata watu 10, na kutoa wasifu wao fulani fulani, ili kujenga taswira kuwa ubongo wake uko vizuri. Sasa mtu wa hivyo atahitaji kuandikiwa tangazo la kifo kwa huo mlolongo wenu? Na huyo Msigwa anaweza kumpangia cha kuongea, kama kina Kabudi na uprofesa wao wanaitwa wapumbavu? Tatizo liko kwa rais mwenyewe. Usimlaumi dobi, Kaniki ndio rangi yake.

NB: Bora leo hujatokea kwenye hicho kipindi maana ungefika ukiwa mwanaccm rasmi, baada ya kujificha muda mrefu.
 
Tatizo bwana yule mambo yake mengi hana haraka hata kama hana sababu za msingi za kuharakisha ukweli msiba wa Mkapa umetangazwa kana kwamba aliyekufa ni mjumbe wa Nyumba Kumi...yaani Mkapa aliyekua Rais wa Nchi amezidiwa hata na Ruge
 
Baada ya kukosa teuzi umeanza zile mada zako halisi sio zile za kusifu na kuabudu
Huyu ndio Pascal Mayalla ninayemfahamu. Na kwa chokochoko hizi ni kama vile anatamani kutaja chanzo cha kifo cha mzee katika ile thana ya JF tuna right ya kuwa wa kwanza kupata habari lakini anaogopa.... lakini JK anasema Mzee Mkapa alikuwa analalamika tumbo linamuuma. Labda Rais wetu Kipenzi chetu sisi wanyonge atatuambia sababu ya kifo siku ya mazishi.
 
Kila kitu anafanya siri...ama kweli ukizoea kua muongo huwezi kuanika jambo lolote lazima utaficha
Unaweza kudhani aliamshwa usingizini na kuanza kutoa taarifa bila maandalizi yoyote! Nilishangaa sana kuona taarifa haitaji jina la Hosp.

RIP Mzee Mkapa
 
Wanabodi,

Naangalia Kipindi cha Jicho Letu Ndani ya Habari, kipindi kinajadili Msiba wa Benjamin Mkapa.

Tangazo la Msiba lililotolewa na Rais Magufuli, Kurungenzi ya Mawasiliano Ikulu imelaumiwa kwa kutokumsaidia Rais kikamilifu kutoa tangazo hili, hali inayotafsiriwa kuwa katika baadhi ya matukio, Kurungenzi hiyo inahitaji kusaidiwa na manguli wazoefu ili waweze kumsaidia rais Magufuli katika baadhi ya matukio.

Manguli wa Mwanza, Dotto Bulendu, Edwin Soko na Moses Mathews, wamesema kwa vile hii ni shocking news, kulipaswa kuwepo kwa muda kidogo wa kumuandaa rais Magufuli kutoa tangazo hilo kulitangazia kuanzia, timing, dress code na content za tangazo lenyewe.

Timing
Kwa vile msiba umetokea usiku, kutoa tangazo saa 6:30 usiku was not the right timing kwa Watanzania, news ya msiba ingekuwa held, halafu Wahariri wakaitwa Ikulu usiku ule, halafu Tangazo litolewe live saa 12:00 asubuhi, rais akiwa na VP na PM.

TCRA kutoa taarifa vyombo vyote vya habari vya kielectroniki kujiunga na TBC ili hiyo live itangazwe Tanzania nzima.

Dress Code
Kuna mavazi ya kawaida mtu anaweza kuvaa katika tukio lolote, lakini kuna dress code ya msiba. Wanasema rais Magufuli alipaswa kushauriwa kutoa tangazo hilo akiwa amevaa a proper dress code ya tangazo hilo.

Contents za Tangazo
Tangazo la msiba wa kiongozi wa kitaifa linaongozwa na sheria ya Vifo vya viongozi, sheria imeweka contents za kisheria ambazo lazima liwe na vitu 6
  1. Jina la Kiongozi ni nani
  2. Kifo kimetokea lini
  3. Kifo kimetokea wapi nchini, mkoani, safarini, nje ya nchi
  4. Mahali mahsusi, kimetokea nyumba, hospitalini, safarini,
  5. Kama ni hospitalini, hospitali gani
  6. Sababu za kifo, kimesababishwa na nini, maradhi, ajali, usingizini, etc
Tangazo la rais Magufuli kutangaza kifo cha Mkapa, lilikosa, baadhi ya taarifa muhimu za kisheria, hivyo kuleta sintofahamu kwa jamii.

Hajawahi kusikika kuwa Benjamin Mkapa anasumbuliwa na maradhi yoyote, hivyo taarifa kuwa amefariki hospitali ni shocking, hospitali gani na ameumwa nini, ni maswali ambayo taarifa ya rais ilikosa.

My Take
Kwa vile taarifa ya msiba ni shocking news, flaws ndogo ndogo katika tangazo la msiba huo, zinavumilika. Ni kweli kulikuwa hakuna uharaka wa kukimbilia kutangaza usiku mkubwa, ili kutoa nafasi kwa rais kutangaza in a proper way na kufanya mashauriano na watu wawili watatu ili kutoa tangazo kamilifu kisheria, kikanuni na kiutaratibu.

Namalizia kwa kutoa pole kwa Rais wa JMT, Dr. John Pombe Magufuli, Familia ya Mkapa na Watanzania kwa ujumla, kwa msiba huu mkubwa wa rais Mstaafu, Benjamin Mkapa.

Paskali

Wasaidizi wa Rais, Please Msaidieni Rais Wetu Kwenye Public . Msimuachie Kila Kitu Peke Yake!
Kwa mara ya kwanza mkuu umeongea point sana japo kuna elements za kujipendekeza pia.

Nilipoliona kwa youtube lile tangazo kama layman kwenye tasnia ya khabar kwa kweli nilikua najiskia kama aibu maana maneno yalikua kama hayajapangiliwa vile. Yaani kama anaongea tu kawaida kawaida.

Hiyo number 6 hapo juu mmmmh. Labda mkiambiwa sababu mtaanza kuzua taharuki sijui lkn. Ila unafikiri Mungu hajui hata kama sisi tunafichwa?! Mi kwa maoni yangu kutokana na mitazamo ya sirikali yetu ktk baadhi ya mambo naona wako sahihi kivyao vyao lkn. Sisi tukaaage mwili na tuzike tu. Mengine, Wallah Aa'lam wadigo wenyewe wanakuambia.
 
Saa ile ilikuwa mbaya sana, Rais kweli hakuandaliwa, nahisi huko aliko naye leo ana BP,

Sikusikia hata wimbo wa Taifa, hata ule wa Tanzania Tanzania nakupenda kwa moyo wote.

Hata kama alifia nyumbani au kituo cha afya wangesema, waseme pia aliugua nini,

Mbona maziko yamekimbizwa sana.

Sent using Jamii Forums mobile app
Ukiona jinsi Mkapa na sumaye walivotangaza musiba wa Nyerere Tena kavaa official na wimbo wa taifa ukapigwa ilionyesha u serious wa tukio Mimi kuona mheshimiwa anatangaza ya Mkapa I thought was a joke kwa kweli,hyo kurugenzi wajiangalie
 
Bujibuji,

Hata huo nao ni ugonjwa mkuu, na unauwa pia.

Sote hatuwezi kufa kwa sababu au kutokana na ugonjwa mmoja japo pia wengi wengine tutaondoka kwa sababu au magonjwa yanayofanana. Yote ni mola peke yake.

Ugonjwa wa kumwua mtu hauchaguliwi kama wanavyochaguliwa watia nia wa Kawe.
 
Mkuu P nadhani walilinda hiyo habari isisambae mana siku hizi wajuzi tupo wengi just imagine ingetangazwa na kigogo2014 na auongezee kwa kusema jiwe amemuuwa Bwm. huu ni ulinzi
Yani kigogo ndo wamuogope hivo sidhani!!
 
Mnamuonea tu mh. Rais, naye ni binadamu kama wengine,ana moyo wa nyama,ukute baada ya kupata taarifa za msiba,alilia weee...uchungu ulivyopoa ndio akatangaza msiba kwa umma,utawaza contet saa ngapi?body language yake tu inaonyesha mwili hauna ushirikiano kwa mshituko.kuna wappuuzi wanasema alikuwa anamgegeda jane. Hii nchi hii!!
 
Back
Top Bottom