Tangazo la kifo cha Benjamin Mkapa, Kurungenzi ya Mawasiliano Ikulu lawamani. Inahitaji kusaidiwa kumsaidia Rais - Jicho Letu Ndani ya Habari

Tangazo alitoa ndani ya dk 1 na sekunde 15 kamaliza hakuna info zozote unajua muda ule nilipoona ile video nikashangaa sana nikajiuliza mbona kama aliyekufa ni Mjumbe wa Nyumba kumi yaani...halafu pia hakukua na uharaka wa kutangaza vile katika usiku ule.
Kwa sisi tuliofuatilia kwa Radio tangazo la Msiba wa Sokoine, tukaona tangazo la Msiba wa Mwalimu na Omar, tukaja tukamsikia JK akitangangaza msiba wa Kawawa, tunaungana na Mayala.
Juzi Tangazo limetoka kiwepesi na muda mbaya sana.
 
Tumbo limeungana na kifua, kwa ukubwa wa mwili ule ni rahisi kabisa ukakabwa koo ukahisi maumivu tumboni.
 
Saa 12 asubuhi?...[emoji23][emoji23][emoji23] wazee wenzangu wa jamii forums usiku wa manane isingekuwa taarifa mpya tena..ingeshakuwa story.
 
Pascal Mayalla,
Upo sahihi 100%, ila inakuwaje kama yeye mwenyewe aliamuru alitoe hilo tangazo muda huo huo baada ya kupewa taarifa?
Kuna watu wanasemaga mzee hasikilizi ushauri muda mwingine.

Haya ngoja tuwaachie wajuzi wanaoangalia on both sides of the coin
 
Yeye alitaka Tangazo liwafikie wa Tanzania wanyonge usiku ule ule, milundikano mingine ya kisheria inakwamisha mambo.
P
 
Tangazo la msiba wa aliyekuwa kiongozi mkuu wa nchi hukaa kwenye record hata kwa miaka mingi.

Hii ina maana namna ile alivyotangaza, alivyovaa na yale aliyoyasema, yatatazamwa na kuikiwa na vizazi vingi vijavyo. Hivyo inahitajika maandalizi na utulivu wa hali ya juu.

Mlioshuhudia kifo cha Princess Diana wa Uingereza, nadhani mliona. Diana alikuwa na watoto wake wawili teenagers. Katika hali ua kawaida wangeweza hata kutoa machozi hadharani kutokana na kifo cha ghafla cha Mama yao. Lakini kwa taratibu za kifalme, mfalme, malkia au wanafamilia wa ufalme hawaruhusiwi kulia hadharani. Na katika tukio zima hakuna aliyeonekana kutoa machozi hadharani. Ile haikutokea tu bali kulikuwa na maandalizi.

Sisi hatulazimiki kuiga ya watu wengine lakini tunalazimika kuwa na miongozo ya kila kitu.

Rais Magufuli katika hili, ni miongoni mwa wafiwa wakuu, kama kiongozi wa nchi na pia kwa mahusiano yao ya karibu. Alistahili kutulizwa, kulukezwa na hata kuvumiliwa. Kumwacha afanye kama alivyoongozwa na dhamira yake, haikuwa sahihi.

Kuna wakati watu wanakosa kutimiza wajibu wao halafu kujitetea kwao inakuwa ni rahisi tu - Rais hasikilizi ushauri.

Sent using Jamii Forums mobile app
 

Hilo swali la mwisho ndio mzizi wa yote haya.
 
Naunga mkono hoja. Hata mheshimiwa alitakiwa aandikiwe hotuba yenyewe maana kuna wakati alikuwa anarudia rudia contents ... na wimbo wa taifa ulitakiwa upigwe...kwa kweli limetolewa simple simple sana.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…