Tangazo la kifo cha Benjamin Mkapa, Kurungenzi ya Mawasiliano Ikulu lawamani. Inahitaji kusaidiwa kumsaidia Rais - Jicho Letu Ndani ya Habari

Kwa hiyo mlitaka JF ndio watoe hiyo taarifa, then Serikali itoe asubuhi baada ya kuweka nadharia za JF?
 
Labda kwa sababu tumezoea ‘breaking news’ za JF sijui raisi ateuewa akina nani.

Raisi ni mtu mkubwa sana kwenye nchi anapotokea yeye mwenyewe usiku mnene kutangaza breaking news ya kitu chochote iwe tumevamiwa, kuna kiongozi kafa or whatever ‘symbolic’ inaashiria umuhimu wa tukio kwa taifa na habari yenyewe trustworthy 100%.

Unataka watu watangaze habari za kifo na press conference sijui na kuvaa nguo sahihi; mambo mengine only in Tanzania, wapi kwengine wanafanya ivyo.

Tangazo la kifo cha Mandela au Nkuranziza likikuwa na press conference?
 
Una tafsiri vipi kitendo cha raisi kuongea na taifa saa sita ya usiku? Is it normal au ni kutokana na uzito wa habari yenyewe pamoja na wasaidizi wote kwanini waliona atokee mwenyewe.

Watu wa Ikulu walijua wanafanya nini ‘symbolically’ kutaka yeye aongee, sio kwamba walikurupuka.
 
Pascal Mayalla,

Kwa mitandao ya sasa, mida ya saa kumi na mbili asubuhi hiyo isingekua taarifa tena kwa umma maana nchi nzima saa saba au nane ingekua imeshajua! Labda hii ingekua tamko tu la rais ila sio taarifa!

Kuna mida codes tupa kule.
Kwa hiyo serikali inashindana na mitandao ya kijamii nani awahi kukomenti sio...

Tatizo Ni kwamba licha ya uharaka wote huo bado taarifa haikutimia, yule ni kiongozi wa nchi inahitajika uwazi na umakini kuhusu kifo chake.

Mwalimu alifia hospital ya Mtakatifu Thomas pale Uingereza, tuliokuwa tunakua wakati huo mpaka leo hilo jina halitutoki.

Sasa Mheshimiwa amefia wapi kwa ugonjwa gani haijulikani kabisa.
 
Rais mstaafu Mkapa alizidiwa ghafla usiku akiwa kihospitali cha hapo Makumbusho ambako hakuna hata ventilator. Kiukweli alibanwa na mapafu ila timing ikawa mbovu. Mzaha mzaha wa serikali ya Magufuli kuhusu mambo muhimu ya afya za watanzania yanawagarimu wengi.

Halafu Rais wa nchi kutangaza msiba huku umelegea kama umetoka kula ile kitu ya Mshana Jr au mrangi haileti picha ya kuwa Amir jeshi mkuu tena umewahi kuvaa gwanda kabisa. Kutangaza huku unalegeza mwili ili watanzania waone kuwa umeumizwa sana ni ulimbukeni. In short lile tangazo nililiangalia mwanzoni tu nikaachana nalo maana Rais alikuwa very weak! Kuwa vile hakukufanyi kuonekana eti umeumizwa sana na ni udhaifu mkubwa kwa Amir jeshi mkuu.
 
Ni kuhusu Lissu mkuu, mpaka leo wengine hamjajua tu au hamtaki tu kukubali.

Tulishauri aombwe radhi yaishe lakini wapi, matokeo yake ndiyo mambo kama haya....
 
Leo poti umeweka nukta tupu.
 
Taarifa isingeweza kuvuja family ikisimamiwa isitoe tàrifa,hamna wa kuvujiaha taarifa kubwa kiasi hico


 
Dah! Wakati mwingine unaweza ku-complicate mambo bila sababu za msingi, sasa issue za nguo sijui uwe umevaa hivi au muda angesubiri hadi asubuhi, awaite watu fulani wawepo, nk nk nk, yote haya yangefanyika yangeleta utofauti gani ambao kwa sasa unaonekana umetoweka au umepungua?

Au labda tuendelee kusubiri huko mbeleni litaleta madhara ambayo kwa sasa hayajajitokeza, which I doubt.
Ni mtazamo wangu tu.
 
Pasi nimeshakutabiria mara nyingi tu kuwa nafasi ile ya Gerson ni yako baada ya November,ila Mami usinisahau katika ufalme wako.
 
With due respect, I beg to differ.
Tufike mahali, tuishi maisha halisi, badala ya maisha ya maigizo.
Mzazi wako anapoaga dunia, wazo la kuangalia aina ya mavazi haliakisi uhalisia wa maisha yetu.
Rais Magufuli, katika kutoa taarifa ya kifo cha Rais wetu mstaafu Benjamin Mkapa, alionyesha utu wake katika uhalisia wake.
Kama alikataa kuwasikiliza 'Washauri' wake kuhusu "dress code" nk, ninamuunga mkono.
Dress code na taratibu nyingine ni "uigizaji" na tofauti na 'waigizaji wanavyojiita kioo cha jamii', uhalisia ni kinyume chake.
Watanzania hawapendi uigizaji bandia.
Ukweli huu umejionyesha kwenye chaguzi za maoni za CCM ambapo hao "wanaojiita kioo cha jamii" wamekataliwa kuwa sehemu ya uongozi wa jamii yetu katika majimbo waliyoenda kuomba ridhaa.
Paskali Mayala, Baruani Muhuza, Steve Nyerere, Mpoki, Pilipili na wengineo wamethibitishiwa kuwa kamwe wao siyo kioo cha jamii.
Kioo cha jamii ni wale wanaojitahidi kuishi maisha ya uhalisia.
Siyo maisha ya maigizo.
Rais Magufuli ameonyesha uhalisia wa machungu anayopata binadamu aliyeondokewa na mzazi wake.
Kwa umri aliofikia wa miaka takriban 82, Mzee Mkapa ni mzazi wa sehemu kubwa ya jamii ya nchi yetu, iliyo na umri chini ya miaka 60.
 
Labda tumesikiliza clip tofauti mbona alisema mzee Mkapa kafia hospitali ya Dar Es Salaam automatic picha inayokujia ni Muhimbili.

Tatizo ni hawa waandishi wetu mtu anaanza fani mpaka anakaribia kumaliza udhani kama keshawai kukutana na jina Bronislow Malinowski au ata amewahi kushika kitabu chochote cha ‘social anthroplogy’ katika maisha yake kujiongeza kwenye kutafsiri matukio.

Ndio tatizo liliopo hapa hao wachambuzi ni kutokana na tafsiri zao; hila watu wa Ikulu jinsi walivyoitoa habari walizingatia symbolic significance ya raisi kuzungumza. Na big deal kiongozi wa nchi anapotekea usiku mnene. Hawa kukurupuka Ikulu walijua wanachofanya.
 

Mkuu Pascal unanikumbusha tukiwa wadogo tukienda winda porini na ukaona mbwa anaacha kuwa makini na alichokifuata basi unamstua kwa sauti ya " Hey..Shika shika"
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…