Tangazo la Kondomu au Pedi likirushwa nikiwa karibu na binti yangu huwa napata tabu sana

Tangazo la Kondomu au Pedi likirushwa nikiwa karibu na binti yangu huwa napata tabu sana

babe mimi kuna Bongo movie tulikua tunatizama na maza,jamaa anamsifia demu wake mambo ya kitandani
hata wazungu tu wana maadili ndio mana wana viewers Guidelines.
Bongo movie sio za kuangalia kabisaa ukiwa na mtu mnayeheshimiana nae. Hawana maadili kabisa
 
Bongo movie sio za kuangalia kabisaa ukiwa na mtu mnayeheshimiana nae. Hawana maadili kabisa

ninafikilia hata nikafute kale ka channel, decoder za zamani zilikuwa na option ya kufuta channel
 
Wewe unasema hayo ya kwenye TV na REDIO, mimi juzi nilikuwa napita mahali nikakuta Dogo mmoja wa kama miaka 8 au 10 hivi anacheza na Ndama, nikavutiwa ikabidi nimtanie "niuzie huyo Ng'ombe basi" akaniambia "lete laki moja" alafu akaongeza "au nikuuzie yule" huku ananionyesha Ng'ombe mwingine mweusi aliyekuwa mita kadhaa kutoka pale, nilipochoka ni pale aliposema "ni dume linapanda".
 
Hutaamini lkn ni kweli. Kuna jamaa yangu tukiwa ShopRite enzi hizo mlimani city, alipigiwa simu na binti yake wa kumzaa aliye form tuu kwamba asisahau kumletea taulo za kike. Na lijamaa akapeleka kweli.
Enzi hizo nchi ikiwa na maadili mmama akienda dukani alikua anasema. Naomba biscuti ya Dada. Siku hiziiiii......h
 
We mjita wa wapi wa kuongea matusi na wanao eti elimu ya afya? Acheni kuiga mila zisizo wasaidia! Wewe wazazi wako walikufundisha hiyo elimu? Ili iweje? Ndiyo naana hii ngozi inadharauliwa. Usenge muige! Ushoga muige! Ndoa za nanihii moja muige! Nyie kwnu ni kambale watupu?
 
Unafungua redio unakutana na tangazo la dr mtwenya [emoji1787][emoji1787][emoji1787]
 
Jamani, ni kweli tuko kwenye utandawazi lakini haya matangazo yamezidi ukali utasikia Kondomu ina vidoti inanukia inaongeza utamu au yule binti yuko chooni analia damu zimemtoka ghafla hana Pedi mambo hayo yanatia ukakasi au ni ushamba wangu tu ndo unanisumbua.
POLE SANA. Uwe kama mim tu,UNAANGALIA CHANNELS ZENYE MATANGAZO YA HIVYO NA REMOTE MKONONI yaan tangazo likiwekwa tu chap ushabadilisha.
 
wanakwama sana aise hapa nafikilia kum convince maza abadili king’amuzi aweke Dstv. maana mambo ya sinema zetu ni aibu ule sio uigizaji ni uasherati
Mnunulie DStv sinema zetu zenyewe quality ndogo, hizo movie ni za kuangaliwa na akili ndogo
 
Elimu ya afya haipaswi kuonewa aibu, ni vyema watoto Wakaona na ikibidi waulize na maswali.
Ni sawa ila elimu hii inapaswa kutolewa na mama kwa watoto wa kike na baba kwa watoto wakiume. Sidhani kama baba unaweza kaa na bint yako mzungumzie condom na mambo ya hedhi. Tunachokisema apa tangazo linatoka wakati upo na watoto wako wa jinsia zote na wengine ni wadogo zaid wanatudia kila aina ya Neno wanaloskia kwenye TV.
 
mimi juzi nilikuwa nyumbani kwa maza akawa anatazama channel ya sinema zetu,ghafla wakaanza kuongea matusi na mambo ya kitandani nikanyanyuka nikaondoka,leo pia nimekuta imewekwa channel ya sinema zetu wanasifiana kukatika mauno kitandani nikabadili channel
Kuna tamthilia inaitwa panguso duh!! Wanaume wanaitana majina ya kike, kuna siku niko na familia kuna sehemu jamaa anazungumzia mwanamme kushughulikiwa huku akirekodiwa, sitaki kuangalia tena.
 
Kuna tamthilia inaitwa panguso duh!! Wanaume wanaitana majina ya kike, kuna siku niko na familia kuna sehemu jamaa anazungumzia mwanamme kushughulikiwa huku akirekodiwa, sitaki kuangalia tena.

ni wapuuzi sana Mkuu,kama una watoto wadogo haifai uwape access ya Tv kwa sasa,kuna channel fulani tena nilikua naangalia movie mida ya saa saba au saa nane usiku ghafla nikastukia wanaume wanapigana denda.
 
Daaah umenikumbusha Siku moja,nilikuwa nacheki taarfa ya habari kwa jirani tajiri wa kijijini huko, likapitishwa tangazo la pedi.
Seblen yupo mkewe,binti yake wa kidato cha nne na kijana mmoja.
Mzee ni mtu wa makamo.

Lilipopita tangazo Mzee akauliza.
"HIVI HII ITAKUA MIKATEE EEEH?"
😂😂😂
Nilibanwa na cheko,
Huwa sisahau mpk wakati huu.
Watu walioko seblen akiwemo mkewe wakakausha tu hawakujibu neno.
 
Back
Top Bottom