Tangu Kikwete alipopata Urais, CCM wakafungua geti la viwango duni katika siasa

Tangu Kikwete alipopata Urais, CCM wakafungua geti la viwango duni katika siasa

Naona raia wa Marekani huelewi.
Kwa kisingizio cha utamaduni wa kwenu:
-Hatutaki utoke Ikulu kuelekea kwenye taarabu
-hatutaki utoke ikulu ukacheze mdundiko mitaani
-hatutaki utoke ikulu ukacheze bugobogobo mitaani na kubaka wasichana kwamba ni chagulaga
-hatutaki utoke ikulu ukawinde ngiri kwa upinde na mishale,
- ..... ukachunge ng'ombe porini.
Mkuu,

Kama hutaki hata huhitaji kusubiri miaka mitano ya uchaguzi umuindoe rais.

Katiba yako inatoa nafasi kumuondoa rais kwa impeachment.

Anzisha tu impeachment process kwa sababu rais kacheza taarab, halafu waaambie Watanzania huyu rais hafai tumuondoe jwa sababu kacheza taarab.

Tuone utafika wapi.
 
Aliyeharibu hij nchi si Kikwete ni Magufuli. Wapinzani walianza kutekwa na kupotea kipindi gani ? Upendeleo wa watu wa aina fulani ulianza na Rais yupi ? (Magufuli na Kanda ya ziwa kama Mama na Visiwani ) . Teuzi za kupewa ndugu wa karibu katika baraza la mawaziri zilianza lini ? (MAGU NA Dotto Biteko{binamu} akaja mama na Mchengerwa {mkwe} na Wanu{binti} ameshachukua form ya kugombea ubunge Zanzibar.). Kikwete anajiharibia sasa hivi kwa kumkumbatia huyu mama lakini uongozi wake ulikuwa bomba sana. Wahandishi wa habari walikuwa na uhuru wa kufichua ufisadi nje nje. Magu ndiye Rais wa kwanza kupitisha miradi bila bunge kujadili. (Mf Miradi yote ya Chato uwanja wa ndege, chuo cha veta, hospitali na miradi wa NHC). Hii imewarahisishia marais wanaofuata maana wakitaka kuhamisha hela rahisi kwao. Namaliza kwa kusema as long as you are alive your legacy might change. Kikwete anaiharibu legacy yake sasa hivi.
Kikwete hakupaswa kuwa rais. Ni kosa la Mkapa kukubali mtu aliyetumia fedha kuingia ikulu. Mimi sina shida na taarabu au mambo mengine lakini urais siyo kwa kila mtu. Ni kweli alikuwa mvumilivu kwenye kukoselewa lakini hakuwa na upeo wa kuona mambo na pia udhaifu wake mkubwa ulikuwa kwenye watu aliowateua. Pengine mfumo wetu wa uongozi ungekuwa tofauti (rais asiwe na mamlaka kubwa kama ilivyo) angeweza kuwa kiongozi mzuri.
 
Mkuu,

Kama hutaki hata huhitaji kusubiri miaka mitano ya uchaguzi umuindoe rais.

Katiba yako inatoa nafasi kumuondoa rais kwa impeachment.

Anzisha tu impeachment process kwa sababu rais kacheza taarab, halafu waaambie Watanzania huyu rais hafai tumuondoe jwa sababu kacheza taarab.

Tuone utafika wapi.
Nadhani thrd inaeleza udhaifu wa tangu juu, kushuka chini. Impeachment ifanywe na nani? Sisi hapa Nchini tunashuhudia Mbunge akifanya sarakasi bungeni. Huyo ndo aanzishe impeachment kweli?
 
Kumbe mkuu Kiranga unatambua uwepo wa Mungu na unazitambua nguvu zake!!
Natambua uwepo wa muhusika wa hadithi iliyotungwa na watu anayeitwa Mungu.

Kutoa references za Romeo na Juliet si kuamini kwamba hao wahusika katika tamthiliya za Shakespeare walikuwepo au wapo kweli.
 
Kwa wahenga tunafahamu matatizo yaliyotokana na uongozi dhaifu wa JK.

Rais Kikwete alipoingia madarakani, alipendwa sana, na wengi wakawa na matumaini ya uongozi bora. Ilitokana na matamshi yake alipoishika wizara ya fedha juu ya Kigoma Malima aliyekuwa mtangulizi wake, na wakati huo alikuwa hapendwi kabisa!

Tatizo ikawa ni aina ya uongozi wa Kikwete. Ilitegemea urafiki, mahusiano yasiyo na mipaka na hata ngono ilionekana ni mtaji. Ni wakati ambapo nafasi za wakuu wa Wilaya ziligeuka ni nafasi za mafunzo, bila kujali umuhimu wa nafasi hiyo ktk jamii.

Wanachama wakaona kumbe U-rais ni nafasi ya kuchezea tu! Akapigiwa simu za kupewa heri ya 'Birth day*, naye akaitika akisikika nchi nzima. Akataniwa na kucheka, n.k. Baada ya hapo watu waliingia kwa makumi kuomba nafasi ya Urais.

Leo hii rais anaonekana akicheza taarabu, anaalikwa na wachekeshaji, anashikwa bega akiombewa kanisani. Kama ni hivyo, hata Ubunge imekuwa ni nafasi ya kila mtu. Mwaka huu wameomba kwa ubora wao wanaoujua, na wanagomba na kusema ni haki yao, ni wanachama. Mmoja hajui hata kazi ya Mbunge, kasema atakuwa chawa wa Serikali, na mwaziri.

Nafasi za uongozi zimepoteza hadhi yake. Ieleweke kwamba, Unapokuwa mwanachama wa chama cha siasa, haina maana kwamba unastahili kugombea uongozi wowote ktk chama au Taifa. Kila mtu ajipime nafasi anayoiweza. Ni aibu kama bunge litakuwa ni sehemu ya wachekeshaji, a.k.a wasanii. Nchi inayojigamba sasa ina vision 2050, yenye Ai ndani yake.
 
Bado unampongeza Kikwete!

Hapana! Awe ni rais au chifu wa tawla zetu za kineyeji, bado kuna viwango vya matendo na maneno anayostahili kuzungumza kwa kiwango cha nafasi yake. Baadhi ya watu kumfurahia akicheza taarabu au 'kujichanganya' siyo kibali cha kwamba wapiga kura wanataka hilo. Tukidekeza hilo, tutamuona mitaani akiwapongeza changudoa.

Tunapomchangua rais kuna vigezo vya wazi tunavitumia. Kuna vigezo haviotajwi na havionekani, lakini hatutegemei kuona rais akivifanya. Hatuwezi kuandika au kutangaza kwamba rais asiwe mlevi, asiwe changudoa, asiwe mwizi, nk. Lakini hatutegemei mchujo wa kumpata rais uruhusu mwenye sifa hizo awe rais.

Tukianza kupongezana kwa sifa zake za nyumbani eti anafaa, anajichanganya, n.k., iko siku tutamkuta kalaa bar akibebwa na wapiga kura.
Mwinyi aliachana na mgogoro wa mgomo na madaktari wa Muhimbili, akaenda Uwanja wa Taifa kuangalia mziki wa Kanda Bongoman. Hiyo ndo unapongeza? Itakuwa ni nchi ya hovyo tu inayoweza kupongeza mtu wa aina hiyo.
Sitaweka mtazamo wangu kuhusu JK na mama kuhusu udhaifu au streath zao kwenye uongozi wao lakini kama nimemwelewa vizuri kaka Kiranga ni kwamba, huwezi kuuondoa utamaduni au makuzi ya mtu tu kwasababu eti sasa amekua rais. Ni kweli taarabu ni muziki wa ukanda wa mwambao and mitaani hasa miaka ya 90 kurudi nyuma, kulikua na msemo, "umewahi kuona Mjaluo akiimba taarabu"? Why that? Ni music wa ukanda wa pwani na visitation, same as Sengeri. Naendelea kueleza nilivo muelewa mkuu Kiranga katika maandishi yake. Naongeza hili, rais JPM ni "Msukuma" wa kuzaliwa na kukulia, Wasukuma ni wacheza ngoma maarufu sana Tanzania, marehemu "baba" yake tu nae alikua mcheza ngoma maarufu enzi zake na hata jina Magufuli ni nickname yake, sio jina lake. This is according to binti yake Jessica, Je hatukuwahi kumwona Magufuli akipiga ngoma mara baada ya kuziona? Video zake zipo nyingi tu akifanya hivo, mojawapo akiwa airport wakipokea moja ya ndege alizo agiza, JPM baada ya kuona ngoma (ulikua music wa kisasa ) video inamuonesha akiomba ampishe yule mpiga TUMBA na akaenda na kuanza kupiga; now what's the difference between mama kucheza taarabu ambao ni music wa kwao aliokulia tokea utoto na usichana wake? Same as Magufuli nae, ni utamaduni wa Wasukuma baada ya mavuno ya mazao yao, ni ngoma. I'm not sure kama nimemuelewa vibaya bwana Kiranga
 
Naam. Exactly.

Hili ni jambo linalofanyika dunia nzima.

Kiongozi anatakiwa ku connect na watu. Kiongozi si dubwana fulani la mbao lililoshushwa kutoka mbinguni kutumalizia matatizo yetu kama Deus ex Machina.

Viongozi wanatakiwa kudumisha tamaduni za kwao, ikiwamo ya ngoma na muziki.

Nilikuwa nasoma habari kuhusu Salim Ahmed Salim, mwanadiplomasia nguli wa kimataifa anayejulikana dunia nzima. Walikuwa wanamsifia kwa kusema kuwa Dr. Salim Ahmed Salim, pamoja na usomi wake wote, pamoja na kutembea dunia nzima, muziki wake anaoupenda kabisa ni muziki wa kwao wa taarab.

Sasa hiyo ilikuwa ni sifa nzuri kwake, kwamba Salim ni mtu anayethamini utamaduni wa kwao licha ya kuwa mtu aliyezunguka na kuishi sehemu nyingi duniani.

Sasa kwa nini Magufuli akipiga ngoma za kwao, au Samia akicheza taarab tuone tatizo?

Hivi kweli rais kucheza taarab ndiyo tatizo letu?

Yani katika matatizo yoote tunayoweza kuyataja kuwa haya ni matatizo ya uongozi wetu (ambayo kiukweli kabisa yapo mengi sana, hilo sikatai) lakini je, rais kucheza taarab nalo ni tatizo?

Hili ni tatizo au tunashindwa kutenganisha matatizo na chuki binafsi kwa baadhi ya tamaduni za Watanzania?
 
Tatizo lenu Watanzania wengi, mnamfanya rais kama Mungu. Nyie wenyewe.

Halafu rais akikubali kuwa yeye ni Mungu akautumia u Mungu wake kuwapatiliza anavyotaka, kukataza mikutano ya siasa iliyokubalika kikatiba, mnalalamika huyu rais ana mkono wa chuma anajifanya yeye Mungu.

Wakati nyie wenyewe ndo mmeanza kumfanya rais kama Mungu.

Rais akikubali kuitwa Prezdaa ni sawa tu.

Kama hutaki, usimchague.

Inawezekana tulihitaji kumu humanize rais, alionekana kama jidubwana fulani li Juliasi Nyerere Kaizari limeshuka kutoka mbinguni wakati ni mtoto wa Msoga tu kuna watu wana story zake za Saigoni na kwa Macheni huwezi kuamini.

Huyo mwingine ni bidada wa Kizimkazi tu kajiongeza ongeza kaungaunga mambo na kwa bahati kawa rais. Unataka kumkataza asicheze taarab ya kwao kwa raha zake sababu ni rais?

Mbona hata Salim Ahmed Salim, world diplomat, Nyerere's favorite, alicheza taarab ya kwao?

Tena alisifiwa sana kwamba, Salim Ahmed Salim, licha ya kutembea dunia nzima na almanusura awe Katibu Mkuu wa Umoja wa mataifa kama si ubaradhuli wa vwto ya Wamarekani, lakini bado anapenda muziki wa taarab wa kwao Zanzibar.

Mwanasiasa anatakiwa kuwa sociable. Anatakiwa ku connect na watu. Kikwete alielewa somo hili ndiyo maana wakati nyie snobs mnamuona anaharibu, watu wa kawaida walimpenda wakamuona approachable. Samia watu wake wanaona huyu rais anacheza taarab kama sisi, hana makuu.

Nyie mnamuona huyu rais anaharibu standards kwa kucheza taarab, watu w amtaani wanamuona huyu ni mwenzetu anacheza kama sisi.

Si rais anayesikiliza movements na Sonatas za Mozart na Beethoven.

Watanzania kwa mara nyingine tena mnajua sana kukuza mambo trivial wakati mambo muhinu mnayaacha.
Haaaa, kweli kabisa, hallucination, kutaifisha Nyumba zile zinamfanya Kikwete awe bingwa kwa wengine. Hata zile shule na hospitali, tulienda bure. Kisirani hakiishi, I really support you, lakini huwezi kusupprt evil kwa kulipiza kisasi
 
1995 EL alifanya kosa kubwa kumwachia Urais huyu jamaa - alipoukwaa akamtosa mazima. Boyz II Men ikafa mazima.
 
Haaaa, kweli kabisa, hallucination, kutaifisha Nyumba zile zinamfanya Kikwete awe bingwa kwa wengine. Hata zile shule na hospitali, tulienda bure. Kisirani hakiishi, I really support you, lakini huwezi kusupprt evil kwa kulipiza kisasi
Watanzania wengi kama hawa wanaolalamika hapa hawajui kutenganisha jinsi ya kumkosoa kiongozi kwa masuala ya kitaifa, kifalsafa na kisera on one hand na chuki binafsi dhidi ya mtu na utamaduni wake on another.

Hili jambo linawasumbua watu wengi tu Tanzania bado. Hawawezi ku articulate critique iliyojikita katika mambo relevant, wanaishia kumsema rais kucheza taarab as if rais kucheza taarab ni kosa.

Ndiyo maana wanashindwa kumsema Samia kwa mabaya mengi sana anayofanya, wanaishia kumsema kwa sababu anacheza taarab, kitu ambacho ni trivial na haki yake.
 
Jk was the best president of modern Tanzania ever got .........huwezi kumlinganisha na JPM au BM
The best president in Tanzania after Nyerere wa Benjamin Mkapa. Waliofuata wote waliongoza nchi kwa matakwa yao binafsi sio kwa mujibu wa Katiba.
 
Ulimboka hakuwa upinzani alitekwa ili mgomo wa madaktari uishe, watu watibiwe. It's justifiable.
Hakuna kutekwa kuliko justifiable.

Kama mtu kafanya makosa apelekwe mahakamani na kuhukumiwa kwa sheria.

Hii habari ya kutekwa kuliko justifiable ndiyo mwanzo wa mtu yeyote kukubambikia wewr mambo na kujenga habari ya kutekwa kuliko justifiable.
 
In the right situation hata kuua kunakuwa justifiable. Kuna situation usipouwa utauwawa. Ulimboka asinge wekwa sawa wafu wengi wangekufa.
 
In the right situation hata kuua kunakuwa justifiable. Kuna situation usipouwa utauwawa. Ulimboka asinge wekwa sawa wafu wengi wangekufa.
Kuua kunakuwa justifiable mahakamani baada ya hukumu ya kimahakama na mchakato wote wa kimahakama kukamilika.

Hii nchi inatakiwa kuendeshwa kwa sheria, si kwa matakwa ya watu fulani tu.
 
Kuua kunakuwa justifiable mahakamani baada ya hukumu ya kimahakama na mchakato wote wa kimahakama kukamilika.

Hii nchi inatakiwa kuendeshwa kwa sheria, si kwa matakwa ya watu fulani tu.
Ndiyo kwa mgomo wa madaktari ilikuwa sahihi Ulimboka kutekwa n mimi nilisupport wala sikumuona huruma.
 
Ndiyo kwa mgomo wa madaktari ilikuwa sahihi Ulimboka kutekwa n mimi nilisupport wala sikumuona huruma.
Wewe uli support lakini wewe si muhimu.

Wala mimi si muhimu.

Wewe wala mimi si muhimu katika hili kwa sababu hatujakubaliana kuendesha nchi kwa matakwa yako wewe wala yangu mini.

Tumekubaliana kuendesha nchi kwa utawala wa sheria.

Kanuni za utawala wa sheria haziku support utekaji.
 
Wewe uli support lakini wewe si muhimu.

Wala mimi si muhimu.

Wewe wala mini si muhinu katika hili kwa sababu hatujakubaliana kuendesha nchi kwa matakwa yako wewe wala yangu mini.

Tumekubaliana kuendesha nchi kwa utawala wa sheria.

Kanuni za utawala wa sheria haziku support utekaji.
Nimekubali maana nikiendelea kukupinga nitaanza kuonekana kama JPM na wewe utaanza kuonekana kama Tundu Lissu.
 
Back
Top Bottom