Tangu Kikwete alipopata Urais, CCM wakafungua geti la viwango duni katika siasa

Tangu Kikwete alipopata Urais, CCM wakafungua geti la viwango duni katika siasa

Tatizo lenu Watanzania wengi, mnamfanya rais kama Mungu. Nyie wenyewe.

Halafu rais akikubali kuwa yeye ni Mungu akautumia u Mungu wake kuwapatiliza anavyotaka, kukataza mikutano ya siasa iliyokubalika kikatiba, mnalalamika huyu rais ana mkono wa chuma anajifanya yeye Mungu.

Wakati nyie wenyewe ndo mmeanza kumfanya rais kama Mungu.

Rais akikubali kuitwa Prezdaa ni sawa tu.

Kama hutaki, usimchague.

Inawezekana tulihitaji kumu humanize rais, alionekana kama jidubwana fulani li Juliasi Nyerere Kaizari limeshuka kutoka mbinguni wakati ni mtoto wa Msoga tu kuna watu wana story zake za Saigoni na kwa Macheni huwezi kuamini.

Huyo mwingine ni bidada wa Kizimkazi tu kajiongeza ongeza kaungaunga mambo na kwa bahati kawa rais. Unataka kumkataza asicheze taarab ya kwao kwa raha zake sababu ni rais?

Mbona hata Salim Ahmed Salim, world diplomat, Nyerere's favorite, alicheza taarab ya kwao?

Tena alisifiwa sana kwamba, Salim Ahmed Salim, licha ya kutembea dunia nzima na almanusura awe Katibu Mkuu wa Umoja wa mataifa kama si ubaradhuli wa vwto ya Wamarekani, lakini bado anapenda muziki wa taarab wa kwao Zanzibar.

Mwanasiasa anatakiwa kuwa sociable. Anatakiwa ku connect na watu. Kikwete alielewa somo hili ndiyo maana wakati nyie snobs mnamuona anaharibu, watu wa kawaida walimpenda wakamuona approachable. Samia watu wake wanaona huyu rais anacheza taarab kama sisi, hana makuu.

Nyie mnamuona huyu rais anaharibu standards kwa kucheza taarab, watu w amtaani wanamuona huyu ni mwenzetu anacheza kama sisi.

Si rais anayesikiliza movements na Sonatas za Mozart na Beethoven.

Watanzania kwa mara nyingine tena mnajua sana kukuza mambo trivial wakati mambo muhinu mnayaacha.

Mkuu waafrika tunapenda viongozi madikteta, ila wakitunyoosha tunalia na kulalamika. Hata Samia mwanzo walikuwa wanamwita dhaifu, sahivi anawanyoosha wanalalamika dikteta.
 
Hakuna anayemkataa rais kwa sababu ya Taarabu. Tunasema aache mchezo huo. Hakuchaguliwa kuonesha utamaduni wa kwao.

Yaani nitoke Ikulu nikashiriki sherehe ya ukeketaji wa wasichana kama ilivyo tamaduni ya kwetu?
Baadaye Mzalamo akashiriki kwenye sherehe ya mwali anaponema mbele ya TV?
Kuna tamaduni na matendo tusiyoyategemea kuwa ni maonesho ya tabia yako.

Hata Kanda Bongoman alipoteuliwa kuwa waziri wa utamaduni aliachana na muziki. Baadaye aliona hataweza akaachia kazi ya uwaziri na akaendelea na muziki wake. Huko ndo kujitambua na kutambua nafasi uliyonayo.

we jamaa bana, una mambo ya kishamba sana
 
Mkuu waafrika tunapenda viongozi madikteta, ila wakitunyoosha tunalia na kulalamika. Hata Samia mwanzo walikuwa wanamwita dhaifu, sahivi anawanyoosha wanalalamika dikteta.
Ukitaka kujua Waafrika wengi wanapenda udikteta, angalia wanavyoshangilia viongozi wa kijeshi kama Ibrahim Traore.
 
Ukitaka kujua Waafrika wengi wanapenda udikteta, angalia wanavyoshangilia viongozi wa kijeshi kama Ibrahim Traore.

Kabisa mkuu, wanashangaza sana, tena unaweza kuta mtu anapamabania NRNE lakini upande wa pili anamshabikia Traore
 
Sitaweka mtazamo wangu kuhusu JK na mama kuhusu udhaifu au streath zao kwenye uongozi wao lakini kama nimemwelewa vizuri kaka Kiranga ni kwamba, huwezi kuuondoa utamaduni au makuzi ya mtu tu kwasababu eti sasa amekua rais. Ni kweli taarabu ni muziki wa ukanda wa mwambao and mitaani hasa miaka ya 90 kurudi nyuma, kulikua na msemo, "umewahi kuona Mjaluo akiimba taarabu"? Why that? Ni music wa ukanda wa pwani na visitation, same as Sengeri. Naendelea kueleza nilivo muelewa mkuu Kiranga katika maandishi yake. Naongeza hili, rais JPM ni "Msukuma" wa kuzaliwa na kukulia, Wasukuma ni wacheza ngoma maarufu sana Tanzania, marehemu "baba" yake tu nae alikua mcheza ngoma maarufu enzi zake na hata jina Magufuli ni nickname yake, sio jina lake. This is according to binti yake Jessica, Je hatukuwahi kumwona Magufuli akipiga ngoma mara baada ya kuziona? Video zake zipo nyingi tu akifanya hivo, mojawapo akiwa airport wakipokea moja ya ndege alizo agiza, JPM baada ya kuona ngoma (ulikua music wa kisasa ) video inamuonesha akiomba ampishe yule mpiga TUMBA na akaenda na kuanza kupiga; now what's the difference between mama kucheza taarabu ambao ni music wa kwao aliokulia tokea utoto na usichana wake? Same as Magufuli nae, ni utamaduni wa Wasukuma baada ya mavuno ya mazao yao, ni ngoma. I'm not sure kama nimemuelewa vibaya bwana Kiranga

mkuu watu wengi wa Kanda ya Ziwa na Kaskazini wana makasiriko sana na Muziki wa Taarab, sijui nini kinachowasumbua.
 
Watanzania wengi kama hawa wanaolalamika hapa hawajui kutenganisha jinsi ya kumkosoa kiongozi kwa masuala ya kitaifa, kifalsafa na kisera on one hand na chuki binafsi dhidi ya mtu na utamaduni wake on another.

Hili jambo linawasumbua watu wengi tu Tanzania bado. Hawawezi ku articulate critique iliyojikita katika mambo relevant, wanaishia kumsema rais kucheza taarab as if rais kucheza taarab ni kosa.

Ndiyo maana wanashindwa kumsema Samia kwa mabaya mengi sana anayofanya, wanaishia kumsema kwa sababu anacheza taarab, kitu ambacho ni trivial na haki yake.
RAIS SIO ROBOTI,NI BINADAMU ANA HISIA KAMA WATU WENGINE.MWACHENI ASAKATE RUMBA.
 

Attachments

  • watch_trump_dances_to_ymca_at_his_campaign_rallies_nbc_news_now_h264_61824.mp4
    4 MB
Watanzania wengi kama hawa wanaolalamika hapa hawajui kutenganisha jinsi ya kumkosoa kiongozi kwa masuala ya kitaifa, kifalsafa na kisera on one hand na chuki binafsi dhidi ya mtu na utamaduni wake on another.

Hili jambo linawasumbua watu wengi tu Tanzania bado. Hawawezi ku articulate critique iliyojikita katika mambo relevant, wanaishia kumsema rais kucheza taarab as if rais kucheza taarab ni kosa.

Ndiyo maana wanashindwa kumsema Samia kwa mabaya mengi sana anayofanya, wanaishia kumsema kwa sababu anacheza taarab, kitu ambacho ni trivial na haki yake.

Hilo ndio moja ya tatizo letu kubwa sana wabongo, badala ku focus na kukosoa au kohoji matatizo tunafanya personal attack
 
Ukitaka kujua Waafrika wengi wanapenda udikteta, angalia wanavyoshangilia viongozi wa kijeshi kama Ibrahim Traore.
Waafrika, waafrika! Ninyi wazungu mukoje?
Katika dunia hii nchi au tifa gani halikushangilia udikteta. Au nchi gani imeendelea bila udikteta. Taja mojawapo tuone uelewa wako.
 
Waafrika, waafrika! Ninyi wazungu mukoje?
Katika dunia hii nchi au tifa gani halikushangilia udikteta. Au nchi gani imeendelea bila udikteta. Taja mojawapo tuone uelewa wako.
Kwanza kabisa sihitaji kuwa mzungu ili kusema Waafrika wengi wako hivi.

That is a logical no nsequitur fallacy.

I am pretty sure the Finns, Swedes and Norwegians are not asking their soldiers to take over their governments.
 
Kwa wahenga tunafahamu matatizo yaliyotokana na uongozi dhaifu wa JK.

Rais Kikwete alipoingia madarakani, alipendwa sana, na wengi wakawa na matumaini ya uongozi bora. Ilitokana na matamshi yake alipoishika wizara ya fedha juu ya Kigoma Malima aliyekuwa mtangulizi wake, na wakati huo alikuwa hapendwi kabisa!

Tatizo ikawa ni aina ya uongozi wa Kikwete. Ilitegemea urafiki, mahusiano yasiyo na mipaka na hata ngono ilionekana ni mtaji. Ni wakati ambapo nafasi za wakuu wa Wilaya ziligeuka ni nafasi za mafunzo, bila kujali umuhimu wa nafasi hiyo ktk jamii.

Wanachama wakaona kumbe U-rais ni nafasi ya kuchezea tu! Akapigiwa simu za kupewa heri ya 'Birth day*, naye akaitika akisikika nchi nzima. Akataniwa na kucheka, n.k. Baada ya hapo watu waliingia kwa makumi kuomba nafasi ya Urais.

Leo hii rais anaonekana akicheza taarabu, anaalikwa na wachekeshaji, anashikwa bega akiombewa kanisani. Kama ni hivyo, hata Ubunge imekuwa ni nafasi ya kila mtu. Mwaka huu wameomba kwa ubora wao wanaoujua, na wanagomba na kusema ni haki yao, ni wanachama. Mmoja hajui hata kazi ya Mbunge, kasema atakuwa chawa wa Serikali, na mwaziri.

Nafasi za uongozi zimepoteza hadhi yake. Ieleweke kwamba, Unapokuwa mwanachama wa chama cha siasa, haina maana kwamba unastahili kugombea uongozi wowote ktk chama au Taifa. Kila mtu ajipime nafasi anayoiweza. Ni aibu kama bunge litakuwa ni sehemu ya wachekeshaji, a.k.a wasanii. Nchi inayojigamba sasa ina vision 2050, yenye Ai ndani yake.
Umejaa chuki tu kwa JK. Viwango duni katika siasa? Labda ulipata akili kipindi hicho. Hao unaowaita wachekeshaji walikuwepo mabunge ya awamu zote. Sema wewe ulikuwa kwenye kende za dingi yako.
 
Kwanza kabisa sihitaji kuwa mzungu ili kusema Waafrika wengi wako hivi.

That is a logical no nsequitur fallacy.

I am pretty sure the Finns, Swedes and Norwegians are not asking their soldiers to take over their governments.
Jifunze historia ya kila nchi. Nchi gani haikupitia unachoita ni udikteta kabla ya kusema demokrasia?? Soma King Harald Fairhair, soma kuhusu King Sverre Sigurdsson?
Hii siyo dunia ya kujidai utaendelea kwa demokrasia.

Nchi au taifa gani? Au wote tuimbe demnokrasia! demokrasia! Tusitake kumiliki uelewa mitandaoni.
 
Umejaa chuki tu kwa JK. Viwango duni katika siasa? Labda ulipata akili kipindi hicho. Hao unaowaita wachekeshaji walikuwepo mabunge ya awamu zote. Sema wewe ulikuwa kwenye kende za dingi yako.
Mutatukana watu bure tu! Wengi nchi hii tunajua alikuwa kiwango duni! Dhaifu. Nini alifanya kwa miaka 10?
 
Jifunze historia ya kila nchi. Nchi gani haikupitia unachoita ni udikteta kabla ya kusema demokrasia?? Soma King Harald Fairhair, soma kuhusu King Sverre Sigurdsson?
Hii siyo dunia ya kujidai utaendelea kwa demokrasia.

Nchi au taifa gani? Au wote tuimbe demnokrasia! demokrasia! Tusitake kumiliki uelewa mitandaoni.
Sijaongelea historia, naongelea leo.

Kama hujui kusoma kwa ufahamu, hilo ni tatizo lako, si langu.

Yani wewe unataka kuhalalisha Waafrika wanywe maji yenye mavi na kufa kwa kipindupindu leo kwa sababu watu ambao wameendelea huko Ulaya leo wanakunywa maji safi na salama walikunywa maji yenye mavi miaka 200 iliyopita?

Kwa kisingizio cha historia?
 
RAIS SIO ROBOTI,NI BINADAMU ANA HISIA KAMA WATU WENGINE.MWACHENI ASAKATE RUMBA.
Kwa hiyo Trump akicheza mbele ya gari ni sawa na Samia kutoka ikulu kwenda ukumbi wa taarabu na kuanza kunengua? fallacy!
 
Sojaongelea historia, naongelea leo.

Kama hujui kusoma kwa ufahamu, hilo ni tatizo lako, si langu.

Yani wewe unataka kuhalalisha Waafrika wanywe maji yenye mavi na kufa kwa kipindupindu leo kwa sababu watu ambao wameendelea leo wanakunywa maji safi na salama walikunywa maji yenye mavi miaka 200 iliyopita?

Kwa kisingizio cha historia?
Ni sawa boss! Lakini kumbuka leo yetu, wao ni miaka 100 niliyopita. tusijidai wakati bado tunafundisha watu kutumia choo cha shimo. tuache mifano ya US iko hivi, Norway iko hivi!
 
Ni sawa boss! Lakini kumbuka leo yetu, wao ni miaka 100 niliyopita. tusijidai wakati bado tunafundisha watu kutumia choo cha shimo. tuache mifano ya US iko hivi, Norway iko hivi!
Kwanza kabisa bandiko langu la awali limetaja Waafrika tu.

Wewe ndiye uliyeleta inferiority complex ya kutaja wazungu.

Kama vile Waafrika wenyewe kwa wenyewe hatuwezi kukosoana.

Yani umeshindwa kumfikiria Muafrika anayekosoa Muafrika mwenzake mpaka ukanihoji ninavyowasema Waafrika kwani mimi ni Mzungu.

Yani haikuuwahi kutokea akilini mwako Muafrika akawakosoa Waafrika wenzake.

Akili yako ilivyokuwa fupi.
 
Tukio la Kikwete kupigiwa simu na kupewa Happy Birthday na watangazaji wa Clouds FM nalikumbuka. Yawezekana ni uelewa wetu au culture yetu, lakini halikustahili na aliyepigiwa alistahili kutokubali jambo hilo. Najua siyo rahisi kwa rais kupigiwa kama hajaulizwa na kukubali.

Nasema hivyo kwa sababu waliopiga wenyewe, walionesha wazi kwamba wako kwenye utani na rais. Rais (president) akaitwa 'Presdaa' (shame!). Ilikuwa ni kutoheshimu nafasi ya urais kwa mazungumzo na watu walioonesha uhuni wa mitaani. Tukumbuke Taifa zima linasikia. Je ni culture yetu? Au ni vizuri kufanya kama Amerika? 'Happy Birthday Mr President -Marlyn Monroe.

Hilo la taarabu nalo tusilitetee. Nini sababu ya kutuonesha rais anacheza Taarabu? Yaani naye anajua kutikisa kiuno? Hii ni Taarabu ya 2000s; Kanga moko, n.k. Mtu asiniambie eti naye ni binadamu bhla-bhla! Huyu ni rais ana majukumu muhimu aliyoomba kwa kupenda kwake, tunampa privileges zote kwa ahadi ya kutumikia majukumu. Kama anatamani kucheza Taarabu kama akina Hadija Kopa, aondoke tusiingie gharama za ulinzi kwa furaha zake.
Crap
 
Back
Top Bottom