NAGAMAHONGA
JF-Expert Member
- Dec 11, 2012
- 12,322
- 10,920
Olasiti palilipuka mabomu,daudi mwangosi alipigwa akauawa mbele za watu,ulimboka aliokotwa mabwe pande,Na mengine mengi tu lipi tusiloliona.Na kama Magufuli aliharibu akina kibao na mdude wanauawa na nani?Aliyeharibu hii nchi si Kikwete ni Magufuli. Wapinzani walianza kutekwa na kupotea kipindi gani ? Upendeleo wa watu wa aina fulani ulianza na Rais yupi ? (Magufuli na Kanda ya ziwa kama Mama na Visiwani ) . Teuzi za kupewa ndugu wa karibu katika baraza la mawaziri zilianza lini ? (MAGU NA Dotto Biteko{binamu} akaja mama na Mchengerwa {mkwe} na Wanu{binti} ameshachukua form ya kugombea ubunge Zanzibar.). Kikwete anajiharibia sasa hivi kwa kumkumbatia huyu mama lakini uongozi wake ulikuwa bomba sana. Wahandishi wa habari walikuwa na uhuru wa kufichua ufisadi nje nje. Magu ndiye Rais wa kwanza kupitisha miradi bila bunge kujadili. (Mf Miradi yote ya Chato uwanja wa ndege, chuo cha veta, hospitali na miradi wa NHC). Hii imewarahisishia marais wanaofuata maana wakitaka kuhamisha hela rahisi kwao. Namaliza kwa kusema as long as you are alive your legacy might change. Kikwete anaiharibu legacy yake sasa hivi.
Na kama ni hamnazo kweli anafanyaje?Kipindi cha Kikwete kuna kiongozi wa upinzani alimuita Rais hamnazo na hadi itachapishwa magazetini na hakufanywa chochote. Jaribu leo halafu utoe mrejesho.
Tatizo lenu Watanzania wengi, mnamfanya
Watanzania kwa mara nyingine tena mnajua sana kukuza mambo
Kikwete ndiye nyoka mkuu katika taufa hili mungu amchukue tuu kwakweli nchi ibaki salamaKwa wahenga tunafahamu matatizo yaliyotokana na uongozi dhaifu wa JK.
Rais Kikwete alipoingia madarakani, alipendwa sana, na wengi wakawa na matumaini ya uongozi bora. Ilitokana na matamshi yake alipoishika wizara ya fedha juu ya Kigoma Malima aliyekuwa mtangulizi wake, na wakati huo alikuwa hapendwi kabisa!
Tatizo ikawa ni aina ya uongozi wa Kikwete. Ilitegemea urafiki, mahusiano yasiyo na mipaka na hata ngono ilionekana ni mtaji. Ni wakati ambapo nafasi za wakuu wa Wilaya ziligeuka ni nafasi za mafunzo, bila kujali umuhimu wa nafasi hiyo ktk jamii.
Wanachama wakaona kumbe U-rais ni nafasi ya kuchezea tu! Akapigiwa simu za kupewa heri ya 'Birth day*, naye akaitika akisikika nchi nzima. Akataniwa na kucheka, n.k. Baada ya hapo watu waliingia kwa makumi kuomba nafasi ya Urais.
Leo hii rais anaonekana akicheza taarabu, anaalikwa na wachekeshaji, anashikwa bega akiombewa kanisani. Kama ni hivyo, hata Ubunge imekuwa ni nafasi ya kila mtu. Mwaka huu wameomba kwa ubora wao wanaoujua, na wanagomba na kusema ni haki yao, ni wanachama. Mmoja hajui hata kazi ya Mbunge, kasema atakuwa chawa wa Serikali, na mwaziri.
Nafasi za uongozi zimepoteza hadhi yake. Ieleweke kwamba, Unapokuwa mwanachama wa chama cha siasa, haina maana kwamba unastahili kugombea uongozi wowote ktk chama au Taifa. Kila mtu ajipime nafasi anayoiweza. Ni aibu kama bunge litakuwa ni sehemu ya wachekeshaji, a.k.a wasanii. Nchi inayojigamba sasa ina vision 2050, yenye Ai ndani yake.
Kwani nikiwa Mtanzania siwezi kuona tabia fulani za Watanzania wengi na kuzisema?Mbona unaongea kama vile wewe sio mwenzetu Mtanzania ilhali tupo wote hapa tunajadili ya Tanzania ?
"Tatizo lenu Watanzania.... Watanzania mnajua kukuza..."
.
Kikwete ndiye raisi bora kabisa kwa wafanyabiashara chafu,madawa ya kulevya na wezi wa mali za umma ndicho nijuachoJk was the best president of modern Tanzania ever got .........huwezi kumlinganisha na JPM au BM
StupidAliyeharibu hii nchi si Kikwete ni Magufuli. Wapinzani walianza kutekwa na kupotea kipindi gani ? Upendeleo wa watu wa aina fulani ulianza na Rais yupi ? (Magufuli na Kanda ya ziwa kama Mama na Visiwani ) . Teuzi za kupewa ndugu wa karibu katika baraza la mawaziri zilianza lini ? (MAGU NA Dotto Biteko{binamu} akaja mama na Mchengerwa {mkwe} na Wanu{binti} ameshachukua form ya kugombea ubunge Zanzibar.). Kikwete anajiharibia sasa hivi kwa kumkumbatia huyu mama lakini uongozi wake ulikuwa bomba sana. Wahandishi wa habari walikuwa na uhuru wa kufichua ufisadi nje nje. Magu ndiye Rais wa kwanza kupitisha miradi bila bunge kujadili. (Mf Miradi yote ya Chato uwanja wa ndege, chuo cha veta, hospitali na miradi wa NHC). Hii imewarahisishia marais wanaofuata maana wakitaka kuhamisha hela rahisi kwao. Namaliza kwa kusema as long as you are alive your legacy might change. Kikwete anaiharibu legacy yake sasa hivi.
"Tatizo Watanzania mnapenda ..."Kwani nikiwa Mtanzania siwezi kuona tabia fulani za Watanzania wengi na kuzisema?
Unapata wapi habari ya kuona mtu akisema tabia za Watanzania wengi ni lazima yeye asiwe Mtanzania?
Unaelewa hiyo ni non sequitur logical fallacy?
Lakini nchi ilikua inaenda vizuri, deni a nje lilipungua, Amani ilikuepo na pesa ilipatikana, hapo ubaya uko wapi mkuu.Kikwete ndiye raisi bora kabisa kwa wafanyabiashara chafu,madawa ya kulevya na wezi wa mali za umma ndicho nijuacho
Chuki humchoma aliyeihifadhiKikwete ndiye raisi bora kabisa kwa wafanyabiashara chafu,madawa ya kulevya na wezi wa mali za umma ndicho nijuacho
Lakini nchi ilikua inaenda vizuri, deni a nje lilipungua, Amani ilikuepo na pesa ilipatikana, hapo ubaya uko wapi mkuu.Kikwete ndiye raisi bora kabisa kwa wafanyabiashara chafu,madawa ya kulevya na wezi wa mali za umma ndicho nijuacho
Nimeandika facts kama haijaridhika Leta facts zako kupinga kilichoandikwa nimeweka na ushahidi kwenye kila point.Stupid
Ben Saanane Yu wapi ? Kiasi kupigwa risasi ilitokea lini. Rais anafuata reference. Vifo vya kina Kibao na Mdude vimetokea kwa sababu predecessor alianzisha utekaji na uuwaji. Kwa hiyo huyu Mama anaendeleza.Olasiti palilipuka mabomu,daudi mwangosi alipigwa akauawa mbele za watu,ulimboka aliokotwa mabwe pande,Na mengine mengi tu lipi tusiloliona.Na kama Magufuli aliharibu akina kibao na mdude wanauawa na nani?
Kwanza kabisa sijasema mimi ni Mtanzania."Tatizo Watanzania mnapenda ..."
Halafu we mwenyewe unasema ni Mtanzania.
Wasemaji na waandishi wa kistaarabu na kitaalam huwa hawajitoi kwenye utambulisho wa jamii wanayolenga kuikosoa.
Kujiwka mbali na asili ya utambulisho wako katika kuikosoa ni aina ya ulimbukeni.
Jk was the best president of modern Tanzania ever got .........huwezi kumlinganisha na JPM au BM
Ascha udini wako kwani alichaguliwa na waislamu tu.correction: he was the best muslim president ever labda hapo unaweza kuwa na point na inajadilika kama raisi kikwete alikuwa zaidi ya raisi mwinyi tunaweza kujadili au kama uraisi wa kikwete unazidi wa raisi samia leo hii β¦
Hakika kabisa mambo mabaya yalianzia awamu ya Nne na kisha kuzoeleka !Olasiti palilipuka mabomu,daudi mwangosi alipigwa akauawa mbele za watu,ulimboka aliokotwa mabwe pande,Na mengine mengi tu lipi tusiloliona.Na kama Magufuli aliharibu akina kibao na mdude wanauawa na nani?
Kwasababu wanasahau wanadhani Kila mtu husahauHakika kabisa mambo mabaya yalianzia awamu ya Nne na kisha kuzoeleka !
Hata Mzee Warioba na wazee wengine pia walidhalilishwa awamu ya Kikwete π³
Msema kweli ni mpenzi wa Mungu ππ€·πΏββοΈ !