Tangu nipatwe na Matatizo kazini, mke wangu amebadilika tabia

Duh! Pole mkuu. Maisha kwa sasa yapoje upande wako
 
Pole sana. Toka nje katafute pesa mangi, hakuna heshima yeyote utakayopata kwake kama huna pesa especially kama amekuzidi kipato. Baada ya hizo dharau itafuata usaliti ulio waziwazi. Changamka man.
Mleta maada kasema hata Kama anashinda home lakini mkwanja unaiingia Kama kawa,sema labda Mke wake anataka Jamaa awe na kipato Cha Kama Cha boss wake kisa tu labda anahongwa na huyo boss wake vijicenti ndiyo maana anamzarau Mume wake!!!
 
Piga udayworker,kabebe mizigo,kachanganye zege,kachimbe mitaro,kaombe ukondakta nk..
Kwani mleta maada kasema hana pesa!? Mbona pesa anayo hadi anahudumia familia! Sema wife anataka kuona akitoka asubuhi kwenda kazini na kurudi Jioni, yaani anataka Mume wake awe na ajira, ndiyo Mwanamke alivyo kariri Maisha ya 8 to 5 job!

Wakati Dunia Sasa imebadilika,watu wengine wanaingiza pesa hata wakiwa wamelala kitandani au Yuko sebuleni anaangalia tv huku mishe za pesa zinaingia kupitia simu yake!
 
Yupi Bora, Mwanaume anae shinda Nyumbani huku anaiingiza pesa,au Mwanaume anae damkaa asubuhi na kwenda kuzurula bila plani na kurudi home bila kitu na kesho akiamka anaomba tena nauli kwa wife na kwenda kuzurula tena bila mipango!!??
Hujanielewa point yangu mkuu, kazi anaweza asiwe nayo daily kwa sisi wapambanaji sio kila siku ukitoka unapata(vice versa is true), unaweza usitoke kila siku ina uafadhali kuliko kutokutoka kabisa. Kuna watu mwezi unaisha hajatoka kabisa, mishe unazifuata/unazitafuta, hazikutafuti ndio maana ni vyema kutoka.
 
Duh! Pole mkuu. Maisha kwa sasa yapoje upande wako
Nilipitia kipindi kigumu ndani pale kulikuwa na nondo iliyojitokeza kila siku nikilala nilihisi ndio sahihi ya maamuzi (kujiuwa ) nilikonda sana kwa mawazo mtu ulimpa kila kitu mwisho wa siku anakusaliti kisa uje drop kimaisha.

Nashkuru Mama alinipokea japo mama ilimuuma sana cz nilimuuminisha ni mke wa maisha. Kwa sasa naanza upya maisha from 25m to 0 balance.

Nilimpenda sana wife wangu mpaka sasa
 
Narudia kauli yangu, MKE wangu mtarajiwa atafanyiwa VETTING yakibabe sana.. Ili ndoa ikija kuwa NDOANO nisilaumu mtu wala kujilaumu bali nitasema "MUNGU NDIO KAPANGA HILI"
 
Ajira uliyopoteza ulidumunayo kwa muda gani..?
Halafu mbali na hiyo ajira ulikua na mishe gani nyingine iliyokuwa inakuweka town..?
Na bank or mobile account unabalance ya bei gani..?
 
Huyo mke wako hawana tofauti na wale wa love connect ambao kigezo chao kikuu umeajiriwa au umejiajiri. Na hawa wapo wengi sana.
1. Alikujibu kuwa uanze kujifunza kupika km unataka kuwa naye

2. Uanze kumfulia nguo ikiwemo chupi
Ningekuwa mimi ningemfukuza siku hiyo hiyo. Hii ni dharau iliyopitiliza alitakiwa awe mfariji wako kwa sasa
 
Kuna vitabia vya kivivu kaviona kwako vinamboa.hata kama huna kazi amka saa 12 kapambane sio unalala mpaka saa tano ukiamka unashindia kwenye TV.All in all wanawake wengi wanadharau sana unapokosa kipato.
Siwezi kuishi kumfurahisha mwanamke. Uzunguke ili ubembeleze ndoa na kumfurahisha mwanamke?

Ndoa inajengwa na upendo na kuvumiliana kwa kila hali. Ningekuwa mimi ndoa ingevunjika siku hiyo hiyo.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…