Tangu nipatwe na Matatizo kazini, mke wangu amebadilika tabia

Tangu nipatwe na Matatizo kazini, mke wangu amebadilika tabia

Habari za jioni wanajukwaa wa MMU, ikiwa mmetoka katika mihangaiko akili na mwili vimechoka nawaletea jambo jingine hili tupate kulijadili.

Mimi na mke wangu ni waajiliwa yeye ni mtumishi wa umma na mimi ni mtumishi wa sekta binafsi, ndoa yetu ina miaka mitatu sasa na tuna mtoto mmoja (asante sana MUNGU kwa hili).

Shida iliyonileta kwenu ni kuwa hapa karibuni nimepata matatizo ya kikazi sasa imenibidi niwe nashinda nyumbani kwa sababu mimi siyo mtu wa kukaa nje sana nahisi ndipo matatizo yalipoanzia. Tangu nipatwe na hii hali mke wangu amebadilika tabia sijui kama ni makusudi au lah.

Niwe muwazi kuwa mke wangu amenizidi mshahara lakini pamoja na hayo sijawahi kuona tabia hizi kwake hadi hapo nilipopatwa na hizo shida kazini.

Tabia zipo nyingi ila naleta tatu zilizonishitua;

~ Kwanza amekuwa hataki kushiriki nami tendo.

~ Pili sababu huwa nashinda na mtoto huwa napika kwa ajili yangu na mtoto ambapo ye akirudi anapika kwa ajili ya wote kwani anasema sijui kupika. Sasa hapo juzi kati alinambia itabidi nijifunze kupika kama nataka kuendelea kuwa naye.

~ Tatu ni kuwa tuna machine ya kufulia sasa imeharibika, nikamuomba kuwa nikipata hela tutafanya matengenezo akanijibu kama ni hivyo basi niwee namfulia nguo zikiwemo chupi zake daah.

Mimi nimefikiria uamuzi wa kuachana naye licha ya kuwa na mtoto naye, kwani sina mpango wa kumpiga na hiyo juzi ilibaki kidogo nipige arudi kwao Vunjo Mashariki na ulemavu wa uso alivyosema niwe namfulia.

Nauliza tu wanawake wa humu haya anayofanya mwenzenu ni halali kweli?
Samahani ,mkeo ni mpare?
 
Wanawake tunawapenda ila ni wakuwa nao makini sana. Ni vizuri kuoa mwanamke ukiwa huna kitu akukubalie kama ulivyo ili siku ukiwa nacho life still goes on. Ukiwa huna anaelewa
Ndo.maana namuelewa sn wife,
Kumuacha ntakua sijamtendea haki
Alinikuta zero, tumepambana sahv Niko hero
 
Ni ukweli kabisa ila sio kila mwanamke ana tabia ya kishenzi namna hio. Wako wanawake strong ambao hata ukitimuliwa kazi leo heshima yako iko pale pale.
Wenye hofu ya mungu na malezi bora
Hawa wapagani ujipange kisaikolojia[emoji4]
 
Duuh pole sana mkuu

Kama ni kweli ndoa yenu inavutia watu wengi basi hata yeye atakuwa nakigugumizi kiuvunja ndoa yenu labda mambo anayokufanyia saizi ni hasira tu za kukuona umekuwa mzigo

Tafuta mishe ila isiwe hatarishi sana kiasi cha kugharim afya au usalama wako Kwa kigezo Cha kuokoa ndoa, ikishindikana sana kubali tu aende we anza upya utainuka tena.

Sent using Jamii Forums mobile app
Maisha ni kupanda na kushuka,maisha ni kupata na kukosa.... Kuvumiliana ndo kipimo cha upendo......kama ameshindwa kumvumilia akiwa hana upendo uko wapi? Vipi angepata ajali na kuwa mlemavu wa kudumu kingetokea nini? Yani apambane kumfurahisha sio kwa manufaa ya familia!!!?
 
Option B uwe unaondoka hm kabla hajaamk, na urudi keshalala, sometimes unukie pafyum za kike
Akiomba hela za matumizi je au ununue mahitaji na wew unaondoka kuzuga tu???[emoji1787][emoji1787] Au awe anaendaa kuosha magari na kubeba mizigo mkuu
 
Akiomba hela za matumizi je au ununue mahitaji na wew unaondoka kuzuga tu???[emoji1787][emoji1787] Au awe anaendaa kuosha magari na kubeba mizigo mkuu
Hivi mtu ana ajira tena kamzidi mshaara mume anaomba matumizi ya nini? kaka wa watu atoke tu hata hajui anaelekea wapi mwishowe aonekane mzururaji!

Mtoa post kajikwaa tu kidogo naamini Mungu alitaka kumuonyesha kitu hapo, very soon atasonga.
 
Maisha ni kupanda na kushuka,maisha ni kupata na kukosa.... Kuvumiliana ndo kipimo cha upendo......kama ameshindwa kumvumilia akiwa hana upendo uko wapi? Vipi angepata ajali na kuwa mlemavu wa kudumu kingetokea nini? Yani apambane kumfurahisha sio kwa manufaa ya familia!!!?
Thats what happens when you love a wrong woman.
 
Hakuna mwanamke wa kukaa mahali ambapo hapana uhakika hata ukaoe mzaramo wa Samvula Chole eti dela la shughuli hana kisa anakuvumilia *****.
Na wewe ndo walewale tu..angekua kakaa bench miaka miwili sawa au angekua haajiriki sawa...muda mchache tu huo..tayari mabadiliko....???
 
Back
Top Bottom