dr namugari
JF-Expert Member
- Nov 19, 2022
- 10,466
- 18,206
Mwanamke kabila gani Hilo nichukue taadhariChief jiandae visa vya makusudi apo anatafuta sababu za kutemana .
Hii same story imenitokea juzi tu KWA wife niliempenda na kumuamini .
Badala uchumi kuyumba alitengeneza mazingira ya niwe nakasirika mda wote (namshukuru mungu sikuwahi kumgusa ata singi )
Atatengeneza mazingira ya uwe unamnyenyekea Ili ukasirike .
Vitimbwi vyote atakuletea mwisho wa siku mume utakuwa na hasira zako na tendo la ndoa utalikinai (Izo ni plan baadaye sana ndio utakuja kugundua zilikuwa za makusudi )
Jiandae na vikao maana ataenda kulalamika humtimizi haja zake tendo na huduma za ndani .
Ukweli nilipigana vitimbwi na dharau mwisho wa siku anajitangazia kwao nimemuacha na mbaya zaidi alishapakaza mbaya kwao akaja home kimya kimya akabeba vitu .
Usiku narudi home nakuta godoro tu niliumia sana sikutaka purukushani kupiga piga simu najua sababu mti wa pesa umekauka yote haya yametokea.
Ila yote na yote Jipange Ili usije ukakonda KWA mawazo. Good luck budy
Sent from my Infinix X650 using JamiiForums mobile app