Tangu Rais Samia Suluhu aingie madarakani, anatumia usafiri wa ndege tu, gharama zikoje hapa

Tangu Rais Samia Suluhu aingie madarakani, anatumia usafiri wa ndege tu, gharama zikoje hapa

Unazungumzia ile misafara ya barabarani yenye magari 200+ na mahelicopter juu (ambayo yote yanakula mafuta) na wapambe kibao (ambao wote wanalamba posho), achilia mbali kujisimamisha simamisha na kugawa vibunda na kununua majogoo kwa mahela kibao....!?

Halafu baada ya long trip kila chombo cha moto kingelazimu service...

Sasa hapo kipi nafuu kati ya kurusha chombo moja ambacho hakina mbwembwe nyingi au kujaza msururu wa mavieite na kutunyima smooth access watumiaji wa kawaida wa barabara na kusubirishana masaa hadi manne kisa mamisafara

Mzee itakuwa unakosa chaneli ya kutafuna kupitia misafara au chuki binafsi za kimkakati...
 
Wivu tu huna hoja yeyote ya msingi.

Hivi kati ya Samia na Magufuli nani anatumia hela kidogo kwenye safari zake? Msafara wa Magufuli magari 30+ na ulinzi wa hali ya juu jumlisha posho unaweza kulinganisha na msafara wa Samia akitumia ndege moja.

Plus gharama ya kuchelewesha wananchi kwenye shughuli zao za kila siku. Hivi unajua gharama ya watu kukaa foleni kusubiri kiongozi apite?
 
Jf kumbe ina vilaza kiasi hiki..Ndege ya Rais ilinunuliwa kwa ajili gani?

Ulitaka SSH apande bus la Mgamba ashukie nyegezi au?.
Mleta mada kataka kujua gharama zikoje, wewe unahamisha mjadala. Wewe ni wale shuleni mlienda kusomea ujinga.
 
Cheaper kuliko magari Mia moja, na watu Mia tatu na kusimamisha miji

Look at the cost holistically, sio kitopolo-topolo

Umejibu swali lake vibaya, kijuaji na kumbe ni mtupu tu. Hiyo unayoita “holistically” ina-kuwa tu katika mji husika na kwa mfano Mwanza leo. Huwezi kusema Shinyanga au Musoma hawaendelei na shughuli zao!! Gharama za kutumia ndege pia ni zaidi ya barabara tu kwa sababu wale waliopaswa kuwa katika msafara bado watakwenda kwa ndege au barabara LAKINI na magari yao. Kwenda kwa ndege hakupunguzi idadi ya magari yanayohusika na msafara wa Rais. Kuna kitu kinaitwa “last mile”. Hiyo haitafanywa kwa ndege!!

Tuzoee hili - ziara za taasisi hii zina gharama kubwa. Ni sehemu ya kazi.
 
Jf

Itakumbukwa katika awamu ya serkali ya tano kila kitu kilifanyika kwa minajili ya kubana matumizi ya serkali

awamu ya sita chini ya Samia Suluhu imekuwa ya kitofauti kabisa na awamu ya tano hususani katika suala la matumizi ya rais
Mheshimiwa Rais Samia tangu kuapishwa kwakwe amupiga route kadhaa ndani na nje ya nchi
Usafiri unaotumika muda wote ni ndege pekee

Hivi gharama zake hapa ziko vipi ukilinganisha na ule usafiri wa barabara ambao ni rahisi kubana matumizi
Awamu ya tano ilikuwa na hesabu zisizo na maana yaani 1+1-1 = Na Sifa zisizo na tija. Rais anasimamisha gari toka Dodoma hadi Dar watu wote hawafanyi kazi wanajipanga Barabarani, Uchumi unasimama, Huku anamsafara wa gari 70.
Mwisho wa siku anasema anabana matumizi
 
Si ni Bora kuliko azunguke kwa Gari kila akipita jam barabaran,hana muda wa kupoteza hovyo
She is very smart
 
Kwanini munajisahaulisha haraka mwendazake msafara wake ulikuwa na helkopta juu inamfuata kila aendapo bure bure ndio mbali msafara wa magari ya kifahari msururu mrefu gari ata hazihesabiki, Zile ndege pale airport hazina route yoyote hasara tupu kwanini mama asitembee nazo kuzitoa toa mavumbi?
 
Back
Top Bottom