Tangu Soka lianze hadi leo hii, Kuna Mchezaji yeyote aliyefikia kiwango cha Maradona au Messi?

Tangu Soka lianze hadi leo hii, Kuna Mchezaji yeyote aliyefikia kiwango cha Maradona au Messi?

WADAU WENZANGU HESHIMA KWENU!

1-LEONEL ANDRES MESSI-LA PULGA
View attachment 399998 View attachment 399999 View attachment 400000 View attachment 400001 View attachment 400003

2-DIEGO ARMANDO MARADONA-GOLDEN BOY

View attachment 400004 View attachment 400010 View attachment 400011 View attachment 400009 View attachment 400008 View attachment 400005

Tangu soka lianze hapa ulimwenguni. Ni mchezaji yupi aliyefikia kiwango cha wafalme hawa wa soka hapa duniani Al maarufu LEONEL ANDRES MESSI-LA PULGA & DIEGO ARMANDO MARADONA-GOLDEN BOY

Nataka tu niwakumbushe wadau wenzangu! Najuwa kuna wengine watakuja hapa na misemo tofauti tofauti na mada isemavyo flani anamagoli mengi la hasha! hapa hatuzungumzii wingi wa magoli bali tunazungumzia viwango bora vya mchezaji!

MESSI na Maradona wanajulikana ni wachezaji wa kipekee mno kuwahi kutokea katika ulimwengu huu wa soka, wamepitia wakati mgumu sana,

Tofauti na kipindi cha akina PELE Wamecheza katika kipindi ambacho watu hawakuwa wakijua sana mpira tofauti na sasa, na hata sheria zilikuwa laini Mno tofauti na sasa Sheria zimekuwa ngumu kitu kidogo filimbi, hebu fikiria kuwa kipindi hicho OFF-SIDE zilikuwepo za kumwaga , hata ukimpa mtu ki-pepsi ilikuwa ni poa tu, ukimpiga mtu push ya nguvu jambo la kawaida REFA hakufikirii kama sasa.....

Vile vile ufungaji ulikuwa ni mrahisi mno, magoli yalikuwa sio magumu kama ambavyo tumewashuhudia katika kipindi chao.


Pia ningeomba tuwe wakweli bila kuwa na ubaguzi wa aina yeyote ule.. eti kwa sababu huyu White tusimpe haki yake, eti kwa sababu huyu ni Black tusimpe haki yake..... No! hiyo haipo... na kama mtu huyo atachagua mchezaji kwa kigezo cha rangi ama utaifa wake basi huyo atakuwa si mshabiki haswaa wa soka. Kila mchezaji tumpe haki yake awe mweusi ama mweupe na vilevile taifa alikotoka.

Ahsanteni;

Maradona hakuwahi kubeba UEFA champions League wala hako ka Nesi kenu hakana World Cup wala Copa America...
taja watu wenye mafanikio katika Soka.
 
Hivi kuna kipimo gani cha kujua kiwango cha ubora WA uchezaji toka soka liaze, ambacho kitatusaidia kuelewa jambo hili, pasipo kuwa na ushabiki. Tena tuzingatie nyakati, kumlinganisha Pele na Messi walioishi nyakati tofauti sidhani kama ni sawa. Hao kila mmoja ni bora kwa nyakati zake na mashabiki wake. Hata Leo wengine hawamkubali Messi, wanamkubali Ronaldo. Ushabiki na nyakati vizingatiwe kupima ubora WA mchezaji

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kichwa chako kitakuwa kigumu kuelewa....nimekusaidia lkn naona bado unarudi pale pale! Pole sana
Black panther ,mbona hoja ya compact iko wazi sana?watu wanakuwa bora kwa vigezo maalum kwanza ulitakiwa utoke vigezo gani vilivyokufanya uwa weke hao juu na kuwataka wadau waweke wanaoweza kuwa beat hao.
Na ukifuatilia comments kuna member humu kaweka list tofauti ambapo messi na maradona hawapo.
Kwa kuweka vigezo itapunguza kelele humu labda.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mleta uzi kafafanua vizuri mno! Tatizo letu waaflika tunaangalia rangi ya mtu na utaifa wake, hii kitu mbaya sana inatuponza...

sasa wewe kwa akili yako tu ya kuzaliwa unaamini Gaucho kamzidi Maradona,mfalme wa soka,hata pele katupiliwa mbali?

Kwa akili yako tu ya kuzaliwa unaamini Gaucho kamzidi Messi,mfalme wa soka?

Kwa akili yako tu ya kuzaliwa unaamini Gaucho kamzidi Zidane?

Watanzania tunaongea mno without facts...kwakuwa bob marley kaongea na wewe ukaamini sindio?

Why Maradona and Messi wameshika no 1 ktk best Players in the world alaf Gaucho yupo wa 31 na still siku zinavyozidi kuloloma anaendelea kudrop? Usipende kuhadithiwa hakikisha mwenyewe......

Mkuu MDEGEREKO katoa ushauri smart yakuwa msipende kuhadithiwa nendeni youtube mkajionee wenyewe mtapata jibu.....
Nimeamia upande wako sasa ,am hooting for M and M!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Wachezaji wa leo messi na ronaldo wanakimbilia kufunga magoli tu na kuvunja rekodi, zaman kuwa mchezaji bora hivi vitu walikua hawaangaliii ndio maana unaweza kukuta beki kawa mchezaji bora, messi na Ronaldo ukitaka kuwashindanisha unaangalia magori na record lakin ukitaja kuangalia ufundi wa mpira yaani unaenda kuangalia mpira sio magori tu na pasi bali utam wa mpira GAUCHO ndo mhezaji aliekua amekamilika kila kitu

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Nmemfatilia pele vilivyo.. naamin kabisa pele alikuwa mchawi wa soka he is the best, alikuwa na kipaji cha soka sijui angezaliwa kwenye dunia ya sasa ingekuwaje, alikuwa na speed, power, anatumia miguu yote, skills za hali ya juu.. mfupu lakin anaenda hewan..

Then messi, kwangu messi amemzid maradon vitu vdogo, dribbling na wepes messi anadribble mpira vzur zaid ya shuja maradona na pia maradona alikuwa mzito kidogo.. n hii ni baada ya kuwachek na kuwafatlia vzur..

Ronaldo de lima na wenzie wanafata..

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Gaucho ndo mtu pekee anaeweza kuucommand mpira anavyotaka yeye, tangu uanze mchezo wa soka had leo hakuna kiumbe alieweza kusogelea uwezo wa gaucho hata robo, yule ni mteule kwa ajil ya burudan ya soka. Kitu pekee ambacho messi kamzid gaucho ni idadi ya magoli

Sent from koromije using bashite
 
He he he hee mti wenye matunda siku zote hupigwa mawe,,,,,,,, hao hao wataalamu mkuu wanamtambua Mhuni Diego ndie baba lao after Leonel Mec. Uyo muzee analindwa kutokana na umri wake na kujipendekeza kwa mizungu. Ukitaka mzungu akupende mnyenyekee 2 kama anavyofanya pele.atakupa adi nyumba na kupewa umaarufu.




FIFA Player of the Century was a one-off award created by FIFA to decide the greatestfootball player of the 20th century, announced at the annual FIFA World gala, held in Rome on 11 December 2000.[1] Diego Maradona andPele were joint winners of the award.[2][3]Maradona won the award based on the Internet poll, while Pelé won the award based on votes from FIFA officials, journalists and coaches.[2][3]

Since 1991, FIFA have had awards for FIFA World Player of the Year and they decided to bring in the new millennium by conducting a public vote to decide the FIFA Player of the Century. This was to be decided by votes on their official website, their official magazine and a grand jury. Maradona won the Internet-based poll by wide margins, garnering 53.6% of the votes against 18.53% for Pelé.[4]
Sasa mkuu ulishasikia wataalam wanaojua soka ndio walimtawaza pele kuwa mchezaji wa karne ila KURA ZA INTERNET ndio akashinda maradona sasa je hapo kwa vigezo vyako nani ni bora??? Aliyechaguliwa na washabiki au na wataalam??

Yaani by 2000 kizazi chote cha waliochesa mpira na pelel plus washabiki waliomshuhudia live walishakuwa wamekufa ila kufkia 2000 maradona alikuwa na miaka 6 tu tangu astaafu soka la kimataifa!!!! Sasa hapo nani ambaye alikuwa bado kwenye limelight ya mpira???

We ulitegemea poll iliyofanyika ulaya kwa kutoa 70% ya kura wamchague mchezaji ambaye hawakuwahi muona akicheza alafu wamuache maradona waliomuona live akicheza!!!!mkuu i assure u hata ssa wakimshindanisha muhamed ali na mauweather kwa kura tu atashinda mayweather
 
Hahahahahaa embu kapitie mechi za hungary miaka ya 50 umuone njemba inaitwa ferenc puskas ndio urudi hapa kumsifia messi
Sina haja ya kumaliza bundle langu what I know is lapulga is d baddest player I ever seen......


Hao wengine I'd just a history

Sent From My Nokia Ya Tochi
 
😛😛Mkuu Watapata wapi facts...ukweli utabaki pale pale,wanajua yupi mkali wa soka ila hawataki kusema tu, maradona na messi kitu ingine hakuna wakuwakamata wafalme hawa
Messi atastafu timu ya Taifa Bila kunyanyua kwapa Kombe la dunia
 
Sina haja ya kumaliza bundle langu what I know is lapulga is d baddest player I ever seen......


Hao wengine I'd just a history

Sent From My Nokia Ya Tochi
Duh kaz kwelikweli watanzania yaani unafanya conclusion hata puskas humfaham na hata huelewi kwanni fifa wamededicate tuzo za goal of the year kwa jina lake ????? Ushamsikia Telmo zara???? Kocsis je??? Kwa ufupi messi hamkuti hata zico afu mnataka kuconclude tu kisa umeangalia mpira enzi za messi??? Ni vzuri uka dedicate muda wako kuangali channel kma espn classics uone biography za hizo njemba nlizozitaja ndio uje na conclusion ila kma huwafaham then unajidanganya tu kuwa messi ndio best eva
 
Duh kaz kwelikweli watanzania yaani unafanya conclusion hata puskas humfaham na hata huelewi kwanni fifa wamededicate tuzo za goal of the year kwa jina lake ????? Ushamsikia Telmo zara???? Kocsis je??? Kwa ufupi messi hamkuti hata zico afu mnataka kuconclude tu kisa umeangalia mpira enzi za messi??? Ni vzuri uka dedicate muda wako kuangali channel kma espn classics uone biography za hizo njemba nlizozitaja ndio uje na conclusion ila kma huwafaham then unajidanganya tu kuwa messi ndio best eva
1502116389308.png
1502116413817.png


Lionel Messi Akiwa na Miaka 30 tayari ameshafikisha magoli zaidi ya 500

Huyo Puskas Mpaka anastaafu alikuwa na Magoli takribani 500 .... Sasa nadhani utakuwa unaelewa who is the best, usidanganyike na tuzo kuitwa majina yao,



Nakusihi tena Lionel Messi ni mchezaji balaa saaaaaana tena mshukuru mungu umebahatika kumshuhudia kiumbe huyu ....


Hivi huyo Puskasi record zake pale real Madrid zikoje mbele ya Cr7


NB: MIAKA HIYO KULIKUWA HAKUNA OFFSIDE

Sent From My Nokia Ya Tochi
 
Back
Top Bottom