Tangu tufahamiane naye, nimekuwa naota ndoto za ajabu ajabu

Ni kweli Kuna wanawake wana

Huyo shangazi ulikutana nae akakutamkia anakupenda ameamua akujie kivingine katika ulimwengu wa roho.upo katika process ya kurogwa....Kaa nae mbali Sali sana pia soma neno sana pia
Nikivunja mawasiliano, hawezi kuniijia tena kiroho?
 
Mzeee wangu chukua majani ya mti wa mbaazi na chumvi ya mawe weka ndani ya ndoo ya maji yakuoga hrf nuwia maneno utakayopenda Kisha oga usiku kuanzia saa nne muda tulivu,,, pia tumia chumvi ya mawe kudekia ndani mwako na asubuhi unapokwenda kwenye arakati kanyaga chini Kwa miguu miguu miwili ukiwa peku nuwia/ swali Kwa Imani yako! Akirudi Tena kwenye ndoto uje utoe ushuhuda
Ila kwenye ndoto sikuona sura yake, hapo naomba unifafanulie mkuu.
 
Nikivunja mawasiliano, hawezi kuniijia tena kiroho?
Mambo ya kiroho yanatibiwa kiroho zaidi na ya mwili yanatibiwa mwilini...hio ishu ishakua ya kiroho hapo ata useme umblock au uhame haitasaidia cha muhimu Sali sana ndo utaokoka na huyo jezebel
 
B
Ijumaa ya juzi niliamua nitoke kidogo angalau nikapate mbili tatu za baridi.

Nikiwa maeneo ya kujivinjari, huku napambana na mitungi yangu, mara akatokea lishangazi la makamo. Akaomba tukae naye pale mezani, kwa sababu nilikuwa mwenyewe nikamkubalia.

Akaagiza raundi, tukawa tunaendelea kunywa; ile namtazama puani,nikamuona ameweka kipini; na mimi watu wanamna hiyo huwa nawaogopa sana, kwa sababu wanamna hiyo huwa ni makonkodi kwenye mahusiano.

Baada ya kulewa, lishangazi likaanza kufunguka, ''unajua nakupenda sana, sitaki uwe mbali na mimi, nataka angalau nizae na wewe, kwa sababu nina mtoto mmoja ana miaka sita, anatakiwa apate mdogo wake''

Nikafikiria, nikamwambia tutaongea muda utakaporuhusu, kwa sasa tunywe pombe tu. Tukawa tumekubaliana Jumatatu jioni ndio tukutane kwa mazungumzo.

Baada ya kulewa sana, kila mmoja akarudi alikotoka; sasa jana jioni kwenye mida saa mbili nikaamua nipumzike; kutokana na uchovu nikapitiwa na usingizi mkali, nikawa naota ninatembea sebuleni, ghafla nikakutana na mwanamke ambaye sijui ameingilia wapi, ile namshika mkono nikawa naogopa. Ikawa hiyo ndoto inajirudia rudia; kushtuka naangalia saa, ni saa tano usiku.

Ikabidi niamke nianze kulikemea hilo pepo; kufika saa tisa ikabidi nirudi tena kulala; mara nikaota ndoto ya namna ile ile, ila hii ya sasa, walikuwa wanawake wawili wamekuja kitandani kwa kunishtukiza, wanalazimisha kutaka mapenzi; ile wananilazimisha, nikawakimbia nikajikuta nimedondoka kwenye ngazi, ile napambana nifungue mlango, nikawa nawasikia wengine wako jikoni.

Nimekuja kushtuka mchana huu, nipo hapa napata kongoro huku nikitafakari hizi ndoto, na kwa nini zitokee nyakati hizi.

Nimeanza kwa kufuta namba ya yule binti nikihisi labda kuna koneksheni, au labda itakuwa ni magonjwa ya akili.

Karibu kwa mawazo.​
Binti au lishangazi??
 
Ungekuwa wewe ungefanyaje, ungemfukuza?
Anaanzaje kuja kwangu sasa...mimi naongea kama Ke..nawajua ke wenzangu ukiona ke ana ujasiri wa kumfata me akiwa hamjui na kukaa nae ujue ana ujasiri wa kufanya lolote...
 
Wengi sasa hivi hawaoni aibu, wana ujasiri uliopitiliza, na mpaka anakuja kuna maamuzi anakuwa alishayafanya.
 
Ijumaa ya juzi niliamua nitoke kidogo angalau nikapate mbili tatu za baridi.

Nikiwa maeneo ya kujivinjari, huku napambana na mitungi yangu, mara akatokea lishangazi la makamo. Akaomba tukae naye pale mezani, kwa sababu nilikuwa mwenyewe nikamkubalia.

Akaagiza raundi, tukawa tunaendelea kunywa; ile namtazama puani,nikamuona ameweka kipini; na mimi watu wanamna hiyo huwa nawaogopa sana, kwa sababu wanamna hiyo huwa ni makonkodi kwenye mahusiano.

Baada ya kulewa, lishangazi likaanza kufunguka, ''unajua nakupenda sana, sitaki uwe mbali na mimi, nataka angalau nizae na wewe, kwa sababu nina mtoto mmoja ana miaka sita, anatakiwa apate mdogo wake''

Nikafikiria, nikamwambia tutaongea muda utakaporuhusu, kwa sasa tunywe pombe tu. Tukawa tumekubaliana Jumatatu jioni ndio tukutane kwa mazungumzo.

Baada ya kulewa sana, kila mmoja akarudi alikotoka; sasa jana jioni kwenye mida saa mbili nikaamua nipumzike; kutokana na uchovu nikapitiwa na usingizi mkali, nikawa naota ninatembea sebuleni, ghafla nikakutana na mwanamke ambaye sijui ameingilia wapi, ile namshika mkono nikawa naogopa. Ikawa hiyo ndoto inajirudia rudia; kushtuka naangalia saa, ni saa tano usiku.

Ikabidi niamke nianze kulikemea hilo pepo; kufika saa tisa ikabidi nirudi tena kulala; mara nikaota ndoto ya namna ile ile, ila hii ya sasa, walikuwa wanawake wawili wamekuja kitandani kwa kunishtukiza, wanalazimisha kutaka mapenzi; ile wananilazimisha, nikawakimbia nikajikuta nimedondoka kwenye ngazi, ile napambana nifungue mlango, nikawa nawasikia wengine wako jikoni.

Nimekuja kushtuka mchana huu, nipo hapa napata kongoro huku nikitafakari hizi ndoto, na kwa nini zitokee nyakati hizi.

Nimeanza kwa kufuta namba ya yule binti nikihisi labda kuna koneksheni, au labda itakuwa ni magonjwa ya akili.

Karibu kwa mawazo.​
Yaani ulikemea pepo kuanzia saa tano Hadi saa tisa usiku?Unafaa kuwa mtume na nabii.Fungua kanisa lako upate maokoto.
 
Back
Top Bottom