Tano kali za Nasibu (Diamond Platnumz)

Tano kali za Nasibu (Diamond Platnumz)

Pascal saulon

Member
Joined
Feb 4, 2023
Posts
26
Reaction score
23
TANO KALI ZA NASIBU .

Kabla matikiti hayajaanza kudondokeana yalistawishwa kwenye kitalu bora kabisa Cha bishoo bob junior pale sharobaro records.

Nasibu Abdul Juma hakuviiba na kuviuza Vito vya thamani vya mamaye bi.Sandra ili kwenda kuuza sura studio.Kwanza angeanzaje kuuza sura kama mdomo wake tu ulimparara ,kuna muda meno yalimsaliti na kuponyoka nje hata kama aliufunga ,waja wakambatiza domo.

Kifua chake kabla yakuanza kunyanyua vyuma kutafuta muonekano kilijazwa na upepo wa uchu wa kutoboa kupitia muziki.Alikwisha kuuona umaskini uliomwandama na kuivuta vumbi ya mafanikio iliyotimuliwa na watangulizi wake kama kina Mr.Nice mzee wa (TAKEU),TID na Dully Sykes bishoo wa kariakoo ambao walimiliki dolali ,wanawake waliowataka na hata umaarufu ...
Hii ikamtia chachu.

Usiku wa manane wakati wengine wakikoroma yeye alizikacha shuka zake na kukesha pale sharobaro records.Mkono wake wenye uchu ukayadondosha Mashairi ya dhahabu kwenye karatasi.Baadaye Mashairi yalipoingia Kwa mfumo wa sauti yakazichachafya nyoyo za wapenda burudani na kuvitutumua vinyweleo juu ya ngozi zao.Hakuna pahala sauti hii iliyobeba Mashairi makali mno ilishindwa kufika.

Hii ni kabla ya ujio wa fleva za kinaijeria na midundo ya Kwa madiba yenye lifespan/maisha mafupi kama yalivyo maisha ya n'zi .

Nasibu alianza Kwa kufoka foka (KURAP) lakini wafokewaji wenyewe Wala hawakuwa na habari naye ,mpaka alipobadilika na kuanza kubana pua and the rest was history.....

Nakusogezea mikwaju mitano ya nasibu.

01.NENDA KAMWAMBIE.

Kila mtu hugeuka kuwa mwandishi bora pale anapoumizwa na mwanamke au mwanaume aliyempenda Kwa dhati.

Pongezi ziende Kwa Sarah sadiki mwanamke aliyeurarua moyo wa Nasibu Tena Kwa madharau .
Alipozama pale sharobaro aliichora Ngoma hii ambayo ikawa funguo yake kwenye muziki wake .Pengine Sarah usingetuumizia Nasibu tusingelipata hili kopo na pengine tusingelimjua Nasibu huyu tumjuaye.GOD'S PLANS ARE THE BEST

Audio ilifanywa na bob junior na chupa likaongozwa na Adam Juma .

Hili sio kopo la kwanza Nasibu kutoa ila ni kopo la kwanza kumtambulisha Diamond na kulifuta jina la nasibu.Alikwisha kufanya Ngoma na kaka yake Romy Jones na Fatma kwenye kibao kinaitwa TOKA MWANZA

Moja ya shairi linalovutia .

"Wanaanzaga Kwa tafadhali
Wakishapewa wanapotea
Nenda mwambie ajihadhari
Na Dua njema namuombea.

So asidanganywe na Gari,
burudani na fedha Mimi
akanichukia ,akanishusha
thamani penzi ninalo mpenda
Kisa mvinyo na bia."

02.NITAREJEA

Hisia wazipatazo watu wawili wapendanao wakati wakutengana ili kuyatimiza majukumu ya lazima ndizo hisia utakazohisi usikilizapo kopo hili

"Vipi mizigo umeshaweka tayari ?
Nisije Chelewa nkaaachwa na gari
Basi jikaze usilie mpenzi, mi ntarudi
niombee Kwa mwenyezi.
Zile tabu na
njaa msimu mzima
Mavuno hakuna,huwa nakosa
raha pale nikikosa Cha kutafuna.
Roho yangu inauma ila nitafanya
Nini na pesa Sina .
Nakuonea na huruma bora niende
mjini kusaka chapa"

Kuna haya majibizano kati ya Hawa na Nasibu

Hawa :"Nakupenda kama ukifika salama utukumbuke na sisi ,usisahau kama mkeo na Wana umetuacha na dhiki."

Nasibu"Hilo usijali ila naomba chunga sana ,ogopa na marafiki wakikulaghai hata Kwa mbegu za mtama waambie sidanganyiki."

Pengine hili kopo ni kati ya makopo bora ya majibizano ya Muda wote kwenye gemu la bongo fleva.
Nilipo msikia Nasibu akisema haamini kama yeye ndiye mwandishi wa kopo hili nilimwelewa sana hebu kalisikilize hili kopo tena halafu njoo tutete

03.MBAGALA

Moja ya makopo makali kutoka Kwa nasibu.Mwanamke aliyempenda na kumthamini Kwa Kila namna anamtoa nishai kisa pesa na kuolewa na mchizi mwingine.

"Busara na upole na hekima nilorithi kutoka Kwa mama yangu mama vyote hukuvijali.
Ukaona silingani kabisa kuwa na wewe.
Kwa kuti na mkole ukakata kabisa na shina la penzi langu nana eti kisa mali Mali ukaona kabisa uniache Mimi na uolewe

Ile siku shehe namuona anachoma ubani .
Unavishwa Pete unakuwa make wa Fulani niliumia sanaaa."

Ni hisia gani utazipata unaposikia yule uliye panga kuzaa naye watoto mkapanga hadi na majina tayari amepata mtoto na mtu ambaye siye wewe na amefanana naye sana

"Nasikia Sasa una mtoto anaitwa Mamu ,
Vile akinuna mpaka atabasamu ,
Umefananaye sana aah sana "

04.NTAMPATA WAPI

Kopo lilitoka 2015 .Nasibu anamuongelea mwanamke aliyempenda sana kiasi Cha kushindwa kumsahau .Anajiuliza atampata wapi mwanamke kama yule alonyakuliwa kisa pesa

"Sura yake mtaratibu
Mwenye macho ya aibu
Kumsahau najaribu
Ila namkumbuka sana.
Umbo lake mahabibu
Kwenye maradhi alonitibu
Siri yangu mkarimu
Bado namkumbuka sana

Anaye nifanya silali, juakali ,nitafute tukale .
Lakini hata hakujali ,tali ,
akatekwa na wale."

Sio kisa pesa tu Nasibu analalamikia pengine nyota yake nd'o imponzayo.

"Nyota,nyota ndo tatizo langu
Nyota mpaka nalia pekeangu
Nyota ,nyota ndo shida yangu
Nyota wamenizidi wenzangu"

05 . NUMBER ONE

Hii n'do kopo linalonifungia orodha yangu .Sijaiweka Kwa sababu ya ukali wake lahasha hili ndio lilikuwa tobo la bwana Nasibu kutoboa kimataifa itakuwa dhambi nisipoitia kwenye orodha .
Mashairi mepesi kama utosi wakichanga Cha siku tatu ila yenye kuvutia na kuchezeka ndio yaliyoipeleka hii ngoma majuu.

Kichupa kilifanywa huko Capetown
South Africa chini ya kampuni ya OGOPA VIDEOS na kuwa msanii wa kwanza kulaunch video bila kiingilio pale SERENA.

Baada ya hili kopo kutambaa .Mkali wa Nigeria Davido kipindi hicho anatamba na SKELEWU akatia sauti kwenye remix and the rest was history...
Hii ndo nyimbo ya Nasibu ilomtambulisha kimataifa na nd'o nyimbo iliyochukuwa tuzo nyingi za kimataifa hapa Bongo ,tuzo 17 .

All in all old is good .Kitambo bwana Nasibu alikuwa anaumiza sana kichwa kamsikilize pia kwenye Lala salama ,Binadamu wabaya ,mawazo ,ukimuona na I miss you halafu uje tutete.

Mwandishi Pascal saulon 0699109802

1717612700238.jpg
 
kwani TV na redio yake ina kazi gani mpaka utuwekee hapa JF
 
DIAMOND PLATNUMZ NI MMOJA KATI YA WASANII KUTOKEA AFRIKA YA MASHARIKI KUFANYA VYEMA KIMATAIFA, NI MFANO WA KUIGWA KATIKA JAMII, DIAMOND PLATNUMZ NI MSANII MWENYE JUHUDI, USIKIVU, UTULIVU, AMEFANYA MAMBO MAKUBWA SANA KATIKA TASNIA YA MUZIKI.

UWEPO WA WASANII WA SASA HARMONIZE, LAVA LAVA, MBOSO, RAY VANNY, D VOICE, ZUCHU, YOTE HAYA NI MATUNDA NA MATOKEO CHANYA YA UCHAPA KAZI WA RAIS WA WASAFI.

ENDELEA KUPEPERUSHA BENDERA YETU NASSIB ABDUL ISSACK JUMA.
 
Diamond platinumz The true Legend...

Jamaa ana uandishi flanii hizi amazing nadhani ni Kwa sababu alianza kurapu kabla ya kubana pua...

Na hii inawabeba Sana wasanii waliopita Wasafi records.. wanajua kuandika Sana...

Mikwaju Mitano Nayoipenda zaidi toka Kwa Diamond Platinumz ni hii...

1. Mbagala
"Ile siku shekhe namwona anachoma ubani, unavishwa Pete unakua mke wa flani... Niliumia Sana sanaaaa ahaahha"...

Hapo yakikukuta ndo utaelewa mwamba alimaanisha nn

2. Sikomi
Kama kuna Ngoma imepangiliwa vizuri zaidi kutoka Kwa Simba basi Sikomi ni namba moja.... Kuanzia beat, mashariki, vina, content, vocal na video ni balaa tupu.

3. Ukimwona...
Huenda ndo wimbo wa Simba unaweza kukupa feeling zaidi za mahaba

4. Hunisumbui
Hakuna wimbo wa diamond naupenda kama huu

5. Kesho
Ile beat itachuja siku muziki ukitolewa duniani
 
Aga mi nashangaaga, licha ya Diamond kuimba nyimbo kali za mapenzi. lakini, tukitazama uhalisia wa maisha yake ya Mapenzi tunapata hitimisho jamaa hajakomaa kabisa. We Nasibu tega sikio nikufunze, mapenzi ni kujitoa pasipo kutegemea malipo, mapenzi ni kupoteza uthibiti wa maisha yako na kudondokea penzini.
 
Back
Top Bottom