Tanroads! Barabara zenu Dar es Salaam ni mbovu kupindukia. Tuambieni sisi wananchi mna mipango gani na sisi?

Kuna barabara ziko chini ya tan road
Na tarura
Hawa tarura ndiyo ovyo kabisa

Ova
Tuanze na Tanroads, wakimaliza za kwao ndo twende Tarura. Itakuwa aibu barabara ya Tarura ijengwe iunganishwe kwenye barabara mbovu ya Tanroads.
 
Bora huko vijijini barabara zina changarawe, hizi za Dar ni za tope. Mvua ikinyesha ni mahandaki tupu.
 
Ukishasema barabara zenu tayari umemaanisha wana hiari kuziacha zilivyo wewe unatendewa hisani tu huna haki kuwaambia wakati ni kodi zako

Tanroads! Barabara zenu Dar es Salaam ni mbovu kupindukia. Tuambieni sisi wananchi mna mipango gani na sisi?​

 
Sijui Tanroads hawaioni hii barabara??
 
Dar......
Es....
Salaam...
 
Mumeambiwa iwekwe 💯 kwenye mafuta mjengwe Barabara za Dar hamtaki,komaeni hivyo hivyo na Jiji lenu la uswazi lenye msongamano.

Na hizi mvua mtaisoma namba.
Unajua mji unaoongoza kwa kuchangia pato kubwa la taifa?? Unajua uchumi wa nchi hii unategemea Dar? Kwa nini kuongeza hela kwenye mafuta wakati mkoa unachangia zaidi ya 60% ya mapato ya nchi? Ishu hapa ni kuujali huu mji ili uzidi kukusanya zaidi
 
DAR high way ndo nzuri kwingine kote ni ujinga ujinga mtupu..

1.Moro road
2.Mandela.+Samjoma
3.Ally Hasan mwinyi
4.Nyerere road
5.Kawawa. .

Barabara za mtaa MUNGU mwenyewe anajua
 
Mvua zimeharibu barabara nyingingi sana, hata Tabata Kimanga kuelekea kisukuru lami imevunjika kama biskuti..., magari yanaharibika, usafiri umekuwa mgumu
 
Njooo ukonga uone Palivyo. Banana - kitunda_ kivule_ msongola mama YANGU. KUTUNDA _ kibeberu_ magole. Maweeeeee.BANANA HADI PUGU ( BARABARA YA NGOMBE AU ZAMBIA) , MY GOD
Lakini angalau huko mna lami kilometa kadhaa na hata madaraja. Mna gari za kwenda Kariakoo au Posta na kufanya nauli zipungue. Ingawa haitoshelezi, inatakiwa barabara zote ziwekwe lami kama ilivyo Temeke kule Yombo, Buza nk

Sasa ukitoka Kibamba kwenda Kariakoo nauli sio chini ya elfu 5, maana bodaboda ni elfu 3 (kwenda na kurudi), mwendokasi ni Tshs. 2,900/=, jumla ni Tshs. 5,900/, sasa hapo ni bajeti ya kila siku. Madaladala hakuna sababu barabara ni mbovu watu hawaleti mabasi sababu yataharibika.
 
Mpigi Kupanda basi ni kwa foleni.

Kibamba Hondogo, Kibwegere, Kwa kisima huko hakuna daladala kabisa, ni mwendo wa bodaboda. Kipindi cha mvua hiki nao nauli wanapandisha.
Mbunge anauchapa usingizi na kula per diem. Diwani wa Kibamba tunaambiwa amehama kabisa kata anakaa Mbezi Beach, wananchi mtajijua wenyewe
 
DAR high way ndo nzuri kwingine kote ni ujinga ujinga mtupu..

1.Moro road
2.Mandela.+Samjoma
3.Ally Hasan mwinyi
4.Nyerere road
5.Kawawa. .

Barabara za mtaa MUNGU mwenyewe anajua
Ukiwa highway unaweza ukajisemea mji ndio huu,sasa chepuka kidogo tu mtaani utashangazwa.Pale kimara zilipo ofisi za TRA na CRDB lile eneo lina mashimo muda wote,ikinyesha mvua panageuka bwawa na hakuna hata anayeshtuka.
 
Tuliambiwa wapinzani wanachelewesha maendeleo
 
Acheni kutuona wehu, umeona watu wa mikoani wanalia na barabara na nyie watu wa Tanzania mnajifanya kujiliza.
 
Ni barabara ipi mmeshakwama kwa angalau hata siku 2?, maana huku kwetu Handeni-kilindi-Kiteto tunalala mpaka wiki nzima. Nyie si mna mpaka fly-overs? Kuna barabara inapita juu ya bahari ya Hindi? au Darisalama gani unazungumzi weye?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…