Tanroads! Barabara zenu Dar es Salaam ni mbovu kupindukia. Tuambieni sisi wananchi mna mipango gani na sisi?

Tanroads! Barabara zenu Dar es Salaam ni mbovu kupindukia. Tuambieni sisi wananchi mna mipango gani na sisi?

Hali ni mbaya sana tena sana. Sehemu ya dakika 5 sasa hivi tunatembea nusu saa. Shida kubwa ikiwa hasa jimbo la kibamba. Mpaka daladala wameondoa mabadi yao kwa sababu ya ubovu wa barabara. Mfano mzuri ni hii barabara ya Mbezi High School kwenda Mpigi magoe. Hii siyo barabara ni handaki kabisa.

Hivi hawa TARULA wanashindwa kweli kuweka Lami kipande kidogo namna hiyo? Yaani wanaweza kupiga 1.7T = Bilioni 1700 ambazo ni sawa na 1700km.
 
Jimbo ka kibamba limetelekezwa kabisa.siyo barabara tu hadi maji ya kunywa hamna kabisa.watu kwa sasa wanatumia ya mvua,na masika ikiisha wanahamia visima vya watu binafsi kwa shi 5000kwa unit moja.mbunge wa huko kila siku anamsifu rais eti picha yake iwekwe kwenye pesa?haya ndiyo walikutuma wananchi wako wewe mbunge?
 
Mimi nikajuaga Daresalama nzima ni lami hadi vibarazani, kumbe kuna sehemu ni kama huku vijijini ambapo tangu kuumbwa kwa nchi hatujawahi kujua lami ni nini
Dar kuna maeneo ukifika huamini kabisa km upo Dar yaan panashindwa hata na mikoa mingine, mvua ikinyesha ndio balaa kudadek
 
Jimbo ka kibamba limetelekezwa kabisa.siyo barabara tu hadi maji ya kunywa hamna kabisa.watu kwa sasa wanatumia ya mvua,na masika ikiisha wanahamia visima vya watu binafsi kwa shi 5000kwa unit moja.mbunge wa huko kila siku anamsifu rais eti picha yake iwekwe kwenye pesa?haya ndiyo walikutuma wananchi wako wewe mbunge?
Sasa mbunge mnashindwa kumpa makavu yake anzeni na Mwenyekiti na Diwani wenu wa mtaa mnaoishi mpeni makavu, mnamchekea chekea kuna eneo lilikua linaleta ukorofi taarifa ikapelekwa kwa Mwenyekiti Mwenyekiti kapeleka kwa Diwani na Diwani hio ni njia yake anapita na Gari lake daily akaongea na Halmashauri ikaenda kwa wenyewe bungeni ikaombwa Million 100 pajengwe daraja, ninavyakwambia Daraja imara limejengwa Ila barabara ilibidi ipigwe lami haijapigwa lami mpaka leo Ila shida ilikua Daraja sio lami
 
Dar kuna maeneo ukifika huamini kabisa km upo Dar yaan panashindwa hata na mikoa mingine, mvua ikinyesha ndio balaa kudadek
Bora hata huko mpaka mvua, vijijini kiangazi vumbi na rasta, masika mashimo
 
Dar ni JIJI sio KIJIJI jaribu kutofautisha hapo
Najaribu kulinganisha tabu za huko vs za vijijini

Nb: huduma kama barabara nzuri, maji, umeme zinahitajika kwote tuu iwe mjini au vijijini

Utofauti utakuja kwenye baadhi ya mambo, mfano vijijini hatuwezi kudai fly over, ila barabara nzuri wote tunahitaji
 
Kumbe huko haijawa mbaya zaidi? Ebu pita hii ya mbezi high ndo utajua barabara mbaya zaidi zinavyofanana. Hii ni hatari mnooo.
Hii ni ya Tanroad... Ebu waiwekee lami mpaka bunju. Wananchi wamechoka
 
Najaribu kulinganisha tabu za huko vs za vijijini

Nb: huduma kama barabara nzuri, maji, umeme zinahitajika kwote tuu iwe mjini au vijijini

Utofauti utakuja kwenye baadhi ya mambo, mfano vijijini hatuwezi kudai fly over, ila barabara nzuri wote tunahitaji
Yes mkuu hapa umesema ukweli
 
Hii ni ya Tanroad... Ebu waiwekee lami mpaka bunju. Wananchi wamechoka
Wanakula mishahara, posho na marupurupu mengi ya Serikali Ila kazi zao sasa, barabara ya Maji Chumvi iliyojengwa kwa ZEGE tupu ni barabara moja imara sana kajenga Nani Tarura au TanRoads ?
 
Lakini angalau huko mna lami kilometa kadhaa na hata madaraja. Mna gari za kwenda Kariakoo au Posta na kufanya nauli zipungue. Ingawa haitoshelezi, inatakiwa barabara zote ziwekwe lami kama ilivyo Temeke kule Yombo, Buza nk

Sasa ukitoka Kibamba kwenda Kariakoo nauli sio chini ya elfu 5, maana bodaboda ni elfu 3 (kwenda na kurudi), mwendokasi ni Tshs. 2,900/=, jumla ni Tshs. 5,900/, sasa hapo ni bajeti ya kila siku. Madaladala hakuna sababu barabara ni mbovu watu hawaleti mabasi sababu yataharibika.

Wilaya ya Temeke wako vizuri mnoo kwenye barabara na huduma nyengine mfano unataka kuweka umeme yani hakuna longolongo.

Ilala ni Wilaya ya hovyo sana kwa miundombinu hapa Dar na huduma nyengine.
 
Wilaya ya Temeke wako vizuri mnoo kwenye barabara na huduma nyengine mfano unataka kuweka umeme yani hakuna longolongo.

Ilala ni Wilaya ya hovyo sana kwa miundombinu hapa Dar na huduma nyengine.
Mheshemiwa Naibu Speka Mzee Zungu anapita hapa anasoma comments Ilala inamhusu,
 
Naunga mkono hoja.. Inatakiwa wabadilike katika kujenga barabara zenye ubora. Inashangaza kuona barabara zinajaa maji na kusababisha foleni mvua inaponyesha hata kidogo tu! Yaani mitaro ya maji inayojengwa pembezoni mwa barabara ndio inayoleta shida yote hyo na zile chemba za maji.

Hapo ni kariakoo, nilipita juzi, yaani hali ni mbaya sana kwakweli. Wabadilike
 
Attachments

  • IMG20230420113622.jpg
    IMG20230420113622.jpg
    1.6 MB · Views: 6
Back
Top Bottom