TANU Tanga wakati wa kudai uhuru wa Tanganyika: Dua ya ushindi wa kura tatu Nnyanjani 1958

Mohamed Said

JF-Expert Member
Joined
Nov 2, 2008
Posts
21,967
Reaction score
32,074
TANU TANGA WAKATI WA KUDAI UHURU WA TANGANYIKA: DUA YA USHINDI WA KURA TATU MNYANJANI 1958

Chanzo cha yote yanayokuja hapo chini ni marehemu Mama Ummy bint Anzwan moja ya nguzo za CUF siasa za ushindani zilipoanza mwaka wa 1992.

Nimepitia faharasha (index) ya kitabu cha Abdul Sykes na nimekuta jina la Hemed Anzwan.

Ilikuwa mwaka wa 1958 na TANU inakabiliwa na Uchaguzi wa Kura Tatu uchaguzi ambao ulitishia kukisambaratisha chama.

Nyerere akaamua kwenda Tanga kutafuta msaada wa viongozi wa TANU Tanga - Hamisi Heri na Sheikh Rashid Sembe.

Baada ya kukamilisha mipango yote ya kupata ushindi katika mkutano utakaofanyika Tabora, uongozi wa TANU Tanga uliamua waende Mnyanjani wakafanye dua.

Kwenye kitabu cha Abdul Sykes nimeandika maneno haya:

‘’Nyerere na Amos Kissenge walichukuliwa hadi Mnyanjani na tawaswil ikasomwa.

Waliohudhuria kisomo hicho walikuwa Abdallah Rashid Sembe, Sheikh Dhikr bin Said, Mzee Zonga, Hemed Anzwan, Salehe Kibwana aliyekuwa mshairi maarufu, Akida Boramimi bin Dai na Mmaka Omari.

Aliyechaguliwa kusoma Quran Tukufu alikuwa mjomba wa Mwalimu Kihere, Sheikh Ali Kombora.’’

Nimekichukua kipande hicho na leo asubuhi nikamrushia mwalimu wangu Sharif Mohamed Yahya kutaka maelezo.

Mimi nilitaka kujua uhusiano wa Hemed Anzwan na Mama Ummy bint Anzwan ambae historia yake mama huyu nimeieleza hapa siku chache zilizopita.

Nilikusudia pima Shariff akanipa shubiri.
Nilitaka kadha nikapata kadha wa kadha.

Nakuwekeeni hapo chini maelezo ya hawa masheikh wanasiasa waliopigania uhuru wa Tanganyika ili muwafahamu.

Kwangu mimi hii historia imenishtua sana kani sikujua kamwe uzito wa hawa masheikh wazalendo.

Karibuni msome kwa furaha:

‘’Jina lake ndio hilo Anzuwani b. Mwinyimatano b. Anzuwani El-Kindy.

Mwanawe mkubwa Mwinyimatano (Mzee Nyenye) swahibu Mkuu wa Almarhum Sheikh Muhammad Ayoub Rahmatullahi alayhi.

Mbali ya kuwa ni shemegi yake. Maana Mke wa Sheikh ni Bi. Jaffa bint Muhammad b. Mwinyimatano.’’

Nikamuuliza kuhusu uhusiano wa Mama Ummy bint Anzuwani na Anzuwani b. Mwinyimatano.

‘’Hemed Anzuwani ni ami yake Anzuwani wa Mwinyimatano babake Ummy Anzuwani.’’
Sheikh Dhikri bin Said ni wa Mgome, (ukitoka Mgome ndio unaingia Mnyanjani).

Sheikh Dhikri akidarsisha Msikiti wa Wasegeju au wa Waboma Mnyanjani.

Katika wanafunzi wake ni Sheikh Suleiman b. Mbwana, muasisi wa Zahrau na Rais wa Kwanza wa TAMTA.

Mwanawe Sheikh Muhammad b. Sheikh Dhikri ni Khalifa wa Dandrawiyya.

Mjukuu wake Sheikh Muhammad b. Sheikh Muhammad Dhikri ndiye Karibu Mkuu wa TAMTA sasa, ni mpwawe Sheikh Muhammad b. Ayoub.

Mzee Akida Boramimi ni wa Mgome tajiri kwa viwango vya siku hizo akiwa na tanuri la mbata.

Mwalimu wa Mwalimu Kihere ni wa Ndumi jamaa yake Mzee Mwindau ndugu yake Shaaban Robert, Vibambani Machui.

Sheikh Abdallah Rashid Sembe ni wa Manzabay.
Waliobaki ni wa Mnyanjani.’’

Ikiwa watu kama hawa ndiyo waliokuwa wanachama na viongozi wa TANU vipi mtu angeweza kupambana na TANU au Julius Nyerere akashinda?

Alhamdulilah hakika shukurani zote zinamstahikia Allah.
Ilikuwa historia hii imepotea na Allah kwa rehema zake kairejesha tunaisoma hii leo.

Historia hii itafunza kizazi cha leo kuwa watangulizi wetu walikuwa watu wema wenye kupenda haki na amani.

Waislam hawakupata kumbagua yeyote na historia hii ndiyo shahidi.
Imekuwaje historia hii haisomeshwi watu wakajua tulikotoka?

Screenshot_20220217-043824_Facebook.jpg
 
tawasil za hawa wazee zilikua nzito sana.nimepita Tamta hapo karibu na mikanjuni
 
Julaibibi,
Leo kuna masheikh wa kukodiwa.

Unaweza ukawapata ukawatia kwenye basi hadi Dodoma siku ya pili ukasma kwenye gazeti kuwa masheikh wamekwenda nyumbani kwa fulani kumuomba agombee urais.

Sisemi kama hawa ni masheikh hasa lakini walipokuwapo masheikh haya hayakuwapo.
 
Sh. Mohammed Said,
Huyo wa chini kushoto mwenye kilemba cheupe ni Shekhe Ali bin Hemed bin Abdulla. Aliwahi kuwa Kadhi Mkuu wa Tanga na ni Ami yake marehemu Hemed bin Jumaa aliyekuwa Shekhe Mkuu enzi za Mkapa.
 
Julaibibi,
Leo kuna masheikh wa kukodiwa.

Unaweza ukawapata ukawatia kwenye basi hadi Dodoma siku ya pili ukasma kwenye gazeti kuwa masheikh wamekwenda nyumbani kwa fulani kumuomba agombee urais.

Sisemi kama hawa ni masheikh hasa lakini walipokuwapo masheikh haya hayakuwapo.
hapa leo nimekuelewa vizuri mzee wangu
 
TANU TANGA WAKATI WA KUDAI UHURU WA TANGANYIKA: DUA YA USHINDI WA KURA TATU MNYANJANI 1958

Chanzo cha yote yanayokuja hapo chini ni marehemu Mama Ummy bint Anzwan moja ya nguzo za CUF siasa za ushindani zilipoanza mwaka wa 1992.

Nimepitia faharasha (index) ya kitabu cha Abdul Sykes na nimekuta jina la Hemed Anzwan.

Ilikuwa mwaka wa 1958 na TANU inakabiliwa na Uchaguzi wa Kura Tatu uchaguzi ambao ulitishia kukisambaratisha chama.

Nyerere akaamua kwenda Tanga kutafuta msaada wa viongozi wa TANU Tanga - Hamisi Heri na Sheikh Rashid Sembe.

Baada ya kukamilisha mipango yote ya kupata ushindi katika mkutano utakaofanyika Tabora, uongozi wa TANU Tanga uliamua waende Mnyanjani wakafanye dua.

Kwenye kitabu cha Abdul Sykes nimeandika maneno haya:

‘’Nyerere na Amos Kissenge walichukuliwa hadi Mnyanjani na tawaswil ikasomwa.

Waliohudhuria kisomo hicho walikuwa Abdallah Rashid Sembe, Sheikh Dhikr bin Said, Mzee Zonga, Hemed Anzwan, Salehe Kibwana aliyekuwa mshairi maarufu, Akida Boramimi bin Dai na Mmaka Omari.

Aliyechaguliwa kusoma Quran Tukufu alikuwa mjomba wa Mwalimu Kihere, Sheikh Ali Kombora.’’

Nimekichukua kipande hicho na leo asubuhi nikamrushia mwalimu wangu Sharif Mohamed Yahya kutaka maelezo.

Mimi nilitaka kujua uhusiano wa Hemed Anzwan na Mama Ummy bint Anzwan ambae historia yake mama huyu nimeieleza hapa siku chache zilizopita.

Nilikusudia pima Shariff akanipa shubiri.
Nilitaka kadha nikapata kadha wa kadha.

Nakuwekeeni hapo chini maelezo ya hawa masheikh wanasiasa waliopigania uhuru wa Tanganyika ili muwafahamu.

Kwangu mimi hii historia imenishtua sana kani sikujua kamwe uzito wa hawa masheikh wazalendo.

Karibuni msome kwa furaha:

‘’Jina lake ndio hilo Anzuwani b. Mwinyimatano b. Anzuwani El-Kindy.

Mwanawe mkubwa Mwinyimatano (Mzee Nyenye) swahibu Mkuu wa Almarhum Sheikh Muhammad Ayoub Rahmatullahi alayhi.

Mbali ya kuwa ni shemegi yake. Maana Mke wa Sheikh ni Bi. Jaffa bint Muhammad b. Mwinyimatano.’’

Nikamuuliza kuhusu uhusiano wa Mama Ummy bint Anzuwani na Anzuwani b. Mwinyimatano.

‘’Hemed Anzuwani ni ami yake Anzuwani wa Mwinyimatano babake Ummy Anzuwani.’’
Sheikh Dhikri bin Said ni wa Mgome, (ukitoka Mgome ndio unaingia Mnyanjani).

Sheikh Dhikri akidarsisha Msikiti wa Wasegeju au wa Waboma Mnyanjani.

Katika wanafunzi wake ni Sheikh Suleiman b. Mbwana, muasisi wa Zahrau na Rais wa Kwanza wa TAMTA.

Mwanawe Sheikh Muhammad b. Sheikh Dhikri ni Khalifa wa Dandrawiyya.

Mjukuu wake Sheikh Muhammad b. Sheikh Muhammad Dhikri ndiye Karibu Mkuu wa TAMTA sasa, ni mpwawe Sheikh Muhammad b. Ayoub.

Mzee Akida Boramimi ni wa Mgome tajiri kwa viwango vya siku hizo akiwa na tanuri la mbata.

Mwalimu wa Mwalimu Kihere ni wa Ndumi jamaa yake Mzee Mwindau ndugu yake Shaaban Robert, Vibambani Machui.

Sheikh Abdallah Rashid Sembe ni wa Manzabay.
Waliobaki ni wa Mnyanjani.’’

Ikiwa watu kama hawa ndiyo waliokuwa wanachama na viongozi wa TANU vipi mtu angeweza kupambana na TANU au Julius Nyerere akashinda?

Alhamdulilah hakika shukurani zote zinamstahikia Allah.
Ilikuwa historia hii imepotea na Allah kwa rehema zake kairejesha tunaisoma hii leo.

Historia hii itafunza kizazi cha leo kuwa watangulizi wetu walikuwa watu wema wenye kupenda haki na amani.

Waislam hawakupata kumbagua yeyote na historia hii ndiyo shahidi.
Imekuwaje historia hii haisomeshwi watu wakajua tulikotoka?

View attachment 2121622
Mashalla
 
Katika familia hii,nafikiri yupo mtoto ambaye ni wa kike,ameshika ukuu wa wilaya ya Mheza,baadaye akateuliwa kuwa na cheo Mkoa wa Pwani,kama sijakosea

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom