Tanzania 0-3 DR Congo | 2022 FIFA WC Qualifiers | Benjamin Mkapa Stadium

Hivi hatuwezi kuwapa uraia akina Bangala, Inonga and co.? Kama tulivyofanya kwa Kibu.
Sio suala la kuamua tu kuwapa, hadi nao wauhitaji. Kwani wamekwambia wanataka kuwa Watanzania?
 
Shughuri imeisha, turudi kwenye ligi yetu ya Nbc.

Ligi yetu sasa hivi wanatamba Wacongo, sasa National team yao tunaiwezaje? Tuwe wakweli jameni.
Hilo nalo nenooo.....🤣

Halafu wakongo wanaocheza ligi yetu hawapo katika KIKOSI CHA KWANZA....

Tujipange tutafika 🙏
 
Wiki nzima kabla ya mechi ya Stars na DRC kulikuwa na pilikapilika za ofisi ya Waziri Mkuu kuhangaika na ahadi kedekede kwa Stars ikiwa watashinda game hii , INAFAHAMIKA MADHARA ya ahadi kama hizi kuelekea kwenye mechi muhimu kama hii , Matokeo yake ni tensheni ya kufa na kupona huku wachezaji wakiwaza ahadi walizopewa tu .

Iko haja sasa kwa TFF kudhibiti wanasiasa uchwara wanaotafuta umaarufu kupitia timu ya Taifa huku wakifahamika kwamba kwenye enzi zao hawakuwahi kupiga danadana hata mbili , wanaua morali ya wachezaji .
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…