Tanzania bado changa sana, hata hatujafikia teenage years

FourTwoNet

JF-Expert Member
Joined
Aug 4, 2022
Posts
1,401
Reaction score
2,760
Habari wakuu,

Bila mengi, moja kwa moja naenda kwenye mada.

Ukiangalia kwa umakini, viongozi wetu wakubwa wanaoindesha serikali kwa wakati huu, wengi wao ni watu waliozaliwa miaka ya 1960's. Wapo mpaka wa 1950's huko....na wachache sana ni wa 1970's...hadi kufikia 1980's ni wa kubahatisha, hapo 1980's utasikia wanaitwa vijana.

Sasa basi, kama nchi ilipata uhuru 1961...ina maana intellect au mentality ya viongozi wa sasa rika la 1960's ni ya kipindi cha miaka hiyo, yani nchi bado ikiwa changa kuanzia mwaka mmoja hadi kumi, wale wa 1950's ni kabla hata nchi haijazaliwa, nikimaanisha effect ya kipindi hicho ndio inayoongoza nchi kwa sasa.

Sasa basi, average age ya marais wa Tanzania ni miaka 50 hapo, ina maanisha...wale waliozaliwa kipindi cha 2010's au kipindi hichi, mpaka wafikishe miaka 50 ndio uongozi wa nchi utakuwa "mature".

Kwa kuwa walizaliwa katika kipindi ambacho nchi ilikuwa na miaka 50, ambayo ni average age ya viongozi. Hapo nchi itakuwa ina miaka 100 huko, lakini uongozi wake utakuwa na maturity ya miaka 50.

Sipati picha mambo yatakavyokuwa mazuri wakati huo, ila kwa sasa, hatuna budi kupambana na utoto wetu.

Au mnasemaje wadau?
 
Mbona nchi kama Israel zilikuwa na maendeleo sana baada ya kutimiza miaka 60? Israel ilipata uhuru 1948 na baada ya miaka 60 yaani mwaka 2008, ilikuwa tayari ni nchi yenye maendeleo. Pamoja na kwamba wamepigana sana vita, nchi iko jangwani na hawana rasilimali tulizonazo.
 
Kila nchi inapozaliwa, ina changamoto zake. Israel ni kama mtoto anaezaliwa na mfalme....Tanzania yetu ni kama mtoto aliyezaliwa utumwani!!!
Hapo nimetumia analogy...ila natumai utanielewa.
 
Upo sahihi kabisa, kwa sababu bado sijasikia uwepo wa Raisi yoyote wa nchi za ulaya na marekani aliyeingia mkataba na nchi za kiafrica kuwaibia wazungu zaidi ya kusikia viongozi wa kiafrika wameungana na wazungu kuwaibia waafika. Bado tuko nyuma sana
 
Kila nchi inapozaliwa, ina changamoto zake. Israel ni kama mtoto anaezaliwa na mfalme....Tanzania yetu ni kama mtoto aliyezaliwa utumwani!!!
Hapo nimetumia analogy...ila natumai utanielewa.

Israel walimwaga damu kupata uhuru, walivyopata uhuru 1948 wakavamiwa na nchi majirani wakapigana vita, mwaka 1967 wakapigana tena vita na nchi majirani, mwaka 1973 wakapigana vita nyingine na mpaka leo wanapigana na Wapalestina. Sasa utasemaje Israel ni mtoto aliezaliwa na mfalme wakati historia yao imejaa vita? Na nchi yenyewe ina watu milioni 9 tuu na iko jangwani.
 
Mkuu, namna Israel iliundwa sio kama Tanzania ilivyoundwa...Israel hata hivyo hawakupigania uhuru, WALITANGAZA UHURU!! Atakayepinga inakula kwake... ingefaa uangalie kwa undani formation ya Israel....na formation ya Tanzania. Utaona utofauti.
 
Botswana,Malaysia, Singapore, zina miaka mingapi,unmri wao sio kama wa Tanzania?
Ni kweli, nchi hizi ni rika moja na Tanzania...ila viongozi wao hawakuwa na mentality kama hizi zetu...za miaka hiyo. Yani nachosema ni, kwa malaysia, singapore...tayari walikuwa na exposure. Kuhusiana na Botswana, ni mfano wa yule mtoto anayekuwa mature kuliko wengine...yani ana umri mdogo, lakini maamuzi yake yanakuwa ya mtoto mkubwa. Na ukichunguza vizuri, utakuta viongozi wa Botswana wengi wamekuwa na exposure....hauwasikii kwa majina makubwa...unaweza usiwajue...ni kazi yao ndio inaongea.
By exposure namaanisha...kujionea na kuexperience na kuelewa umuhimu wa maendeleo ya ujumla.
 
@FourTwoNet

Mkapa, Kikwete walikuwa mawaziri wa mambo ya nje. Lazima walipata exposure wakiwa kwenye Ile nafasi, lakini hawakufanya vitu vingi vya maana Kwa Taifa lao ukilinganisha na viongozi wa South Korea, Singapore, Malaysia.

Uthubutu, seriousness, maono, utekelezaji, misimamo, kujifunza Kwa waliofanikiwa, nia ya dhati, uzalendo, jinsi ya kucheza na wababe wa dunia, international diplomacy.

Tunakwama hapo ukilinganisha na wenzetu.
 
FourTwoNet

Mkapa, Kikwete walikuwa mawaziri wa mambo ya nje. Lazima walipata exposure wakiwa kwenye Ile nafasi, lakini hawakufanya vitu vingi vya maana Kwa Taifa lao ukilinganisha na viongozi wa South Korea, Singapore, Malaysia.

Labda uthubutu, seriousness, maono, utekelezaji, misimamo, jinsi ya kucheza na wababe wa dunia, international diplomacy wanakwama hapo ukilinganisha na wenzao.
Yes, ila....kidole kimoja hakivunji chawa. Unaweza kuwa na exposure lakini kama wengi waliokuzunguka hawaelewi dunia inaelekea wapi? Utaonekana mmoja wao, sana sana utajikuta unafanya wanayofanya...maanake hakuna checks and balance. Haswa kwenye urais.
 
FourTwoNet,

Ukiwa na maono, unajua unataka nini, unajua utatimiza vipi maono yako, njia gani utatumia nchi changa inaweza kuwa nafasi nzuri sana ya kutengeneza nchi, uchumi wa nchi viongozi madhubuti vijana nk.

Unafikiri viongozi wa Kwanza wa Indonesia, Singapore, South Korea, UAE, walikuwa na check and balance, au walizungukwa na watu makini?
 
Mkuu, namna Israel iliundwa sio kama Tanzania ilivyoundwa...Israel hata hivyo hawakupigania uhuru, WALITANGAZA UHURU!! Atakayepinga inakula kwake... ingefaa uangalie kwa undani formation ya Israel....na formation ya Tanzania. Utaona utofauti.

Hawakupigania uhuru vipi wakati kulikuwa na "war of independence"? Unafikiri Uingereza iliondoka kwa hiari kama walivyoondoka Tanganyika? Walichapwa na Wayahudi mpaka wakaondoka.

FourTwoNet,

Ukiwa na maono, unajua unataka nini, unajua utatimiza vipi maono yako, njia gani utatumia nchi changa inaweza kuwa nafasi nzuri sana ya kutengeneza nchi, uchumi wa nchi viongozi madhubuti vijana nk.

Unafikiri viongozi wa Kwanza wa Indonesia, Singapore, South Korea, UAE, walikuwa na check and balance, au walizungukwa na watu makini?
Kabisa mkuu, ilikuwa ni jopo la wazalendo...kwa kifupi watu wenye hisa katika maendeleo ya nchi. Ujamaa bwana...ulifanya kila aliyepata nafasi baada ya ujamaa kufutika, ajaribu kujilimbikizia kadri ya uwezo wake. Ndo maana South Korea haiko kama North Korea... izo nchi zingine ulizotaja...ni nchi za falme...na falme hizo zilielewa maendeleo yakiwepo...wananchi hawatapindua falme...maana mpaka kufikia hapo falme hizo tayari zilishaelewa utajiri...sio kama zilikurupuka kutokea umaskini na kutaka kufyonza kila senti.
Kwa kifupi... political interest za falme hizo, mojawapo ilikuwa ni kustabalize uchumi...ili zisipinduliwe. Huku hakuna mtu anajali iyo kitu...sana sana utaambiwa hamia burundi.
 
Hawakupigania uhuru vipi wakati kulikuwa na "war of independence"? Unafikiri Uingereza iliondoka kwa hiari kama walivyoondoka Tanganyika? Walichapwa na Wayahudi mpaka wakaondoka.

Ndugu yangu...jina lako lenyewe jibu tosha kwa nilichoelezea kwenye kumpa jibu jamaa yangu hapo juu. Haya....
Kasome kitu inaitwa "Balfour Declaration"....si una google hapo? Ndo utaelewa wanachofanyiwa wapalestina....hakuna mtu aliyemfukuza british...ni british kavamia hapo. Na unaambiwa, ilikuwa wamechagua sehemu ya Uganda, ila tafiti zao za kijasusi wakaona sio feasible.
Kwa kifupi, hiyo link uliyonitumia, ni kiini macho...the real reason for the war sio independence...ni ku establish a state. Na wanao establish hiyo state ni british.
Join the dots na nilichokuambia usome.
 
Ndugu yangu...jina lako lenyewe jibu tosha kwa nilichoelezea kwenye kumpa jibu jamaa yangu hapo juu. Haya....
Kasome kitu inaitwa "Balfour Declaration"....si una google hapo? Ndo utaelewa wanachofanyiwa wapalestina....hakuna mtu aliyemfukuza british...ni british kavamia hapo. Na unaambiwa, ilikuwa wamechagua sehemu ya Uganda, ila tafiti zao za kijasusi wakaona sio feasible.
Balfour Declaration ilitolewa mwaka 1917 wakati wa vita ya dunia ya kwanza ili Wayahudi waiunge mkono Uingereza kwenye hiyo vita. Lakini baadaye Waingereza walibadili mawazo na ndiyo maana Wayahudi waliwapiga mpaka wakaondoka.
 
Mkuu, Pale Palestina(see the wordplay there?) hapakuwa na myahudi(kwa maana ya jews hao walioanzisha Israel). Yani hawa wayahudi, hawakuwa na sehemu maalum, walikuwa wametapakaa eastern europe nzima...na hata western europe...na walikuwa wameshikilia nafasi kubwa kubwa za uongozi europe nzima nikimaanisha falme, mabenki. Yani mpaka sasa...katika ulimwengu wa siasa.
Israel unayoiona sasa hivi, ni nchi ambayo ilimegwa forcefully kutoka kwenye kipande cha Palestina. Yani Jerusalem, Galilee, Gaza, Nazareth...huko kote...ni ndani ya Palestina. Sasa kutokana kwamba watu waliwapiga vita hawa wayahudi, yani walichukiwa na wazungu wenzao kama ilivyo racism...sema wao wanaiita anti-semitism(unaona the careful wordplay hapo....kwa nini yao iwe na neno anti...na racism iwe ni neno kama neno!!) ndio maana wayahudi wenzao kama kina balfour na kina Rothschild wakachukua sehemu ya palestina na kutangaza wayahudi wanaweza kwenda hapo baada ya kutawanyishwa!!!!
Kwa iyo, wakamyang'anya mpalestina ardhi yake....ndo maana wanapigana mpaka kesho. Yani vita ni dhidi ya hawa "wayahudi" na wapalestina.... hapo hakuna british!!!
 
Waingereza walihusika na walipigwa na Wayahudi. Mfano huu hapa

Back
Top Bottom