Ahsante mkuu, walete....
Hizi ni zile tamaduni za kale ninazojaribu kuziangazia mwanga. Watawala wa sasa wanapaswa kuelewa kuwa siku hizi, maslahi zao na za wale wanaotawaliwa...zinategemeana. La sivyo, bila balance kunakuwa na chaos. Wenzetu huko ukiwaangalia, wamelielewa hili kutokana na trial and error. Sisi tuna bahati ya kujifunza kwao.
Ndio pale pale nikasema inabidi sisi wananchi tukubali hatuna akili ndo maana viongozi wetu wako namna walivyo...maana hawa viongozi ni wananchi pia!Mimi naona hapo ni kujifariji akili tunazo na tumezitumia 80% kwa vitendo tunafanya kwa 5%
Ukiwa na akili safi mwaka 1 wa mabadiliko inatosha.
Nchi yetu inavitu vingi vya hovyo AMBAVYO havihitaji kusubiri hiyo so called teenage years.
NI MIAKA 61 YA UHURU SASA HUU NI UMRI WA MZEE TEENAGE YEARS TUMESHAPITA SASA HIVI TUPO KAMA MANG'OMBE YANAYOSWAGA KUONYESHWA MUELEKEO.
Mkuu, hakuna anayetaka kujitafuna, hilo ni kweli kabisa...lakini utawezaje kueleza pale nchi inachukua mikopo kwa ajili ya maendeleo, alafu watu wanapiga ma 10 percent mpaka hakuna kinachofanyika?
- Ukweli ulio mchungu ni kwamba hakuna mtu yoyote yule - awe kiongozi, raia, hata kichaa - aliye tayari kukata tawi alilokalia.
- Hata huko 'duniani' tunakokuangalia haiwezekani au J. Biden, B. Johnson, Sholz n.k aliye tayari kupitisha sera zitakazoathiri maslahi yake, familia yake au 'wadhamini' wake. Never!
- Ni muundo tu wa kitaasisi kuwezesha sera na utekelezaje wake