Tanzania bado changa sana, hata hatujafikia teenage years

Miaka 50 ni mingi sana
Hapo ndio collective consciousness ya kila mtu itakuwa juu, hivyo hata ukifunga macho uchague kiongozi...atajikuta ni mtu anayeelewa uongozi ni nini!!! Kwa sasa, tukubali tu wengi wetu ni wajinga kwa hivyo ni rahisi sana kujikuta na ujinga madarakani!
 
Angalia fresh hiyo mandatory palestine ni nini...utanielewa. Kumbuka in war, the winner is the one who writes history according to his wishes. In short, wanaweka vitu viwe politically correct kwa manufaa yao wenyewe. Ila behind the scenes ndio kuna mchezo mzima...always the truth HIDES in PLAIN SIGHT!!!
 

Haya lakini bado huamini kuwa Wayahudi walipigania uhuru wao? Hawakuanza kama mtoto aliyezaliwa kifalme. Na hata hiyo Israel ya leo siyo ile waliyoanza nayo 1948. Wameijenga zaidi. Sisi tuna visingizio gani? Tuna nchi kubwa, ardhi nzuri, tuna amani, tuna rasilimali nyingi kulinganisha ka nchi kadogo kama Israel. Kwa nini tunakwama?
 
Naamini kwamba, walipigana. Lakini hapo kwenye context ndio panahitaji uchanganuzi vizuri kwamba ni nini walichokuwa wanapigania na pia, ni kina nani. Hao wayahudi tunaowazungumzia walioanzisha taifa la Israel ni aina ya wayahudi wanaoitwa "Ashkenazi"...uki google hapo utanipata vizuri. Sasa basi, wapo wayahudi ambao sio ashkenazi...na hao ndio waliovamiwa hapo palestina. Wayahudi wa palestina wamebatizwa jina la arabs. Yani, inachanganya kidogo lakini tuangalie kiundani.....kuna jews wa kidini na jews asilia. Yani unaweza kuta mtu ni myahudi asili yake, lakini kidini ni muislam au mkristo. Na unaweza kuta mtu wa kawaida aliye na dini ya kiyahudi. Sasa hawa wayahudi asilia wa ki palestina, walivamiwa na wabritish(wayahudi wa ki ashkenazi)...ndo maana inaweza kutwistiwa kwamba wayahudi walipigania uhuru na wakashinda...na ikawa politically correct. Ila ukweli ni kwamba, ni vita ya wenyewe kwa wenyewe. Huwezi amini nikikuambia royal family ya england ni descendants wa ashkenazi jews...hata windsor sio jina lao...ni jina la mahali walipojenga kasri.

Hawa ashkenazi, walichukiwa kwa sababu watu wa europe walijishtukia...hawa wayahudi wana mafanikio makubwa...yani ndio matajiri, wafalme n.k... Ndio maana wakaanza kuchukiwa tu...na walimalizwa wengi sana, ikabidi wafanye mkakati. Ndio wakaamua kurudi pale palestina na kutengeneza taifa lao. Kumbuka, ndio "mabepari" wakuu.

Sasa kujibu swali lako mkuu, tunapokwama ni kwamba, huku kwetu...kiongozi anataka kuwa kiongozi ili apate nafasi ya kujipatia maslahi. Yani, akiingia kwenye uongozi, hana cha ku poteza...kaingia ili atafute. Tofauti na wenzetu, ntatumia mfano wa ashkenazi...mtu tayari anakuwa na mali zake kubwa tu...kwa hiyo anataka kuchukua uongozi, ili aprotect interests za watu kama yeye na wale wanaoiletea faida biashara yake. Kwa iyo anaweza ata asichukue mshahara wake wa uongozi...anachotaka ni kulobby sheria ambazo zitafanya nchi ipanuke na hivyo biashara zake zifaidi. Yani kwamba uongozi sio permanent, bali biashara ndio permanent.

Ndio maana kule, mtu unatangaza kabisa biashara zako ni zipi, ulizipataje...pesa zako za kampeni umezipataje...mmechangianaje...wakishajiridhisha kwamba you have a lot to lose...ndio unaingia kwenye mchakato wa kutafuta uongozi. Kule hufai kujipa tender za serikali... yani hata hufai kuendesha biashara yako ukiwa madarakani...na ikijulikana umefanya direct business na kampuni zako mwenyewe unafungiwa hizo kampuni... kwa iyo unakuta anayetaka uongozi ni mtu anayependa hiyo kazi...yani ndo kitu roho yake inataka.

Kule matajiri ni wakubwa kuliko viongozi wa serikali, kwa iyo mtu anayetaka hela, anaona kuliko niingie siasa, si heri nifanye biashara ntapata ela zaidi!!!

Samahani kwa kuandika rasimu kama ya warioba. 🤣🤣🤣

Na hilo naomba ukalitazame mkuu.
 
Hata baada ya miaka 1000 kama hao ng'ombe wa CCM bado watakuwepo, tegemea umaskini, magonjwa, upumbavu na majanga zaidi
Chama hakina shida mkuu, watu ndio wabaya. Hata ukabadilisha jina la chama uache watu hao hao....ni sawa na kuliita giza mchana...na mchana giza. Lakini siku ni ile ile.
 

Waingereza waliopigwa na Wayahudi ni wazungu wa kawaida tuu kama Waingereza waliotawala Tanganyika. Kwa mfano High Commisioner wa mwisho aliitwa Alan Cunningham, huyo siyo Ashkenazi na wala hana uyahudi wa aina yoyote. Majeshi ya Cunningham yalipigana na Wayahudi sana tu mpaka akashindwa na Waingereza wakafunga virago na kuondoka.


Ila umeongea ukweli kuwa sisi viongozi wetu ni wasaka fursa. Tunajikwamisha wenyewe tuu. Miaka 60 inatosha kabisa kuleta maendeleo kwenye nchi yenye rasilimali kama Tanzania.
 
Mfano wa royal family niliokutolea hapo...unamaanisha, by the decree of the queen, lakini majeshi ni ya wazungu wa kawaida. Na ukitaka kujua they didnt really lose the war..israel ina exist mpaka leo.

Ni kama yule mtu anayechezesha puppets kwa kutumia strings. We haumuoni, unaona tu the puppets.

Angalia marekani na britain wanaipaga israel annual GRANTS(sio mikopo) za shingapi. Yani kila mwaka. Yani angalia tu annual grants za Israel zote zinatoka wapi. Alafu jiulize KWA NINI? Utanipata mkuu.

Nashkuru umenielewa hapo kwenye ishu ya viongozi.
 

Unajua lakini kati ya Wayahudi waliokuwa mstari wa mbele kupigana na majeshi ya Waingereza walikuwa ni hao hao Ashkenazi? Mfano mzuri ni Menachem Begin ambaye alikuja kuwa Waziri mkuu wa Israel mwaka 1977. Na hiyo misaada kutoka Marekani na Britain haikuanza Wayahudi walipopata uhuru, ilikuja baadaye miaka ya 1970s. Sababu za misaada ya nchi za magharibi kwa Israel ni vita baridi (cold war). Israel ilifungamana na nchi za magharibi halafu nchi za kiarabu kama Misri, Syria zilifungamana na Urusi.
 
Hoja yako ya uchanga haina mashiko, ina "ila" na "lakini" nyingi sana.
 
  • Mtu mmoja au wachache sana hawatoshi kuleta mageuzi ya haraka kwa mentality za uswahili.
  • Mleta mada yawezekana kwa kiasi fulani akawa sahihi: kuwa walijifunza maisha kipindi haijulikani ni ujamaa au ubepari.
  • Mtizamo wangu: Kukiwa na taasisi imara, shirikishi na huru misingi na mafanikio ya taifa hudumu. Mh. Mkapa alijitahidi hujenga taasisi, mpaka hivi sasa sioni matumaini ya taasisi hizo kuwa imara, shirikishi na huru
 
Perfect facts!!! Sasa hapo ni on face value...lakini kwa undani zaidi, for example, ashkenazi wa ujerumani anajikuta akipambana na ashkenazi wa britain...yani kwa kifupi...europe's political wars zilikuwa zinareflect kwenye nchi kama palestina...na hata uku kwetu. Yani fahali wawili wakipigana, unajua kinachoumia. Zionist ambayo "walipigania" uhuru...mwanzilishi wao ni ashkenazi kutoka austria, na austria na ujerumani, kitu kimoja, na kipindi hicho ujerumani na its allies ilikuwa in a political war with allies(other european countries)....ukiangalia vita hivi vilikuwa vinacoincide na world wars...
So you can follow the money, alafu utajua who was really fighting who!
 
Hoja yako ya uchanga haina mashiko, ina "ila" na "lakini" nyingi sana.
Ni sawa kabisa kama hiyo ndiyo opinion yako. Ofcourse huu ni mjadala. Ningependa kuomba ukiweza unifafanulie labda imekosa mashiko kama yapi mkuu.
 
Kabisa mkuu! Na Muheshimiwa Mkapa, anaweza akaonekana hakufanya cha maana ata kama alijaribu, lakini alizungukwa na wengi ambao hawakuelewa mtizamo huo. Mwishowe akaonekana na yeye pia mmoja wao...
Lakini miaka ya mbeleni, natumai collective conciousness ya watanzania itakuwa better kuliko sasa, hivyo kuwa na urahisi wa kupata viongozi bora. Maanake viongozi wa taifa, ni kioo cha wananchi....kumaanisha sio viongozi wana shida, bali ni wananchi(viongozi included)....yani wananchi wengi tuko hivyo, kwa iyo hata ukibadilisha kiongozi, atakayekuja atafanya yale yale au ata zaidi kwa sababu ndivyo wananchi walivyo.

Ni kama kuwa na mifugo maelfu iliyokondeana, na michache sana iliyonawiri...alafu ukaambiwa ufunge macho uchague mnyama mmoja kwa mara mia....kuna probability kubwa unaweza kujikuta wote mia uliochagua wamekondeana.
 
Una uhakika umetueleza ulichokusudia?Mimi sijakiona.
 
Una uhakika umetueleza ulichokusudia?Mimi sijakiona.
Kabisa mkuu, labda haukuwa unataka kukiona....

Kwa kifupi, wananchi wengi miaka ya mbeleni wataelewa ni jukumu lao kujijenga...na hivyo kuijenga nchi. Kumaanisha viongozi wa kipindi hicho, watakuwa reflection ya wananchi walivyo!!!
 
Kabisa mkuu, labda haukuwa unataka kukiona....

Kwa kifupi, wananchi wengi miaka ya mbeleni wataelewa ni jukumu lao kujijenga...na hivyo kuijenga nchi. Kumaanisha viongozi wa kipindi hicho, watakuwa reflection ya wananchi walivyo!!!
Kujieleza kwa vijana imekuwa shida.Usiandike hoja kwa kigogo na kiha hautoeleweka.Hebu rudia kunieleza muheshimiwa,sijaelewa.
 
Kujieleza kwa vijana imekuwa shida.Usiandike hoja kwa kigogo na kiha hautoeleweka.Hebu rudia kunieleza muheshimiwa,sijaelewa.
Mkuu, shkamoo kwanza!! Kwa kweli, nimejaribu kadri ya uwezo wangu kufafanua swala hili... darasani sio kila mtu anafaulu hesabu, kuna wale upeo wao uko vizuri kwenye jiografia. Kwa kufikia hapo,

Ningeomba hilo pia, ukalitizame!
 
  • Na zaidi ya yote, kila jamii (taifa) ina miiko na namna ya kutatua shida zake. Je tangu awali tulihamasishwa kutumia rasilimali zetu kutatua changamoto zetu?
  • Maandishi kadhaa yanaonyesha tangu zama hizo, hata kabla ya Dola ya Kirumi, tawala nyingi zilipinga maboresho kwa kuhofia 'usalama na maslahi' ya watawala. Je hapa kwetu hali ikoje?
 
Ahsante mkuu, walete....
Hizi ni zile tamaduni za kale ninazojaribu kuziangazia mwanga. Watawala wa sasa wanapaswa kuelewa kuwa siku hizi, maslahi zao na za wale wanaotawaliwa...zinategemeana. La sivyo, bila balance kunakuwa na chaos. Wenzetu huko ukiwaangalia, wamelielewa hili kutokana na trial and error. Sisi tuna bahati ya kujifunza kwao.
 
Mimi naona hapo ni kujifariji akili tunazo na tumezitumia 80% kwa vitendo tunafanya kwa 5%
Ukiwa na akili safi mwaka 1 wa mabadiliko inatosha.
Nchi yetu inavitu vingi vya hovyo AMBAVYO havihitaji kusubiri hiyo so called teenage years.
NI MIAKA 61 YA UHURU SASA HUU NI UMRI WA MZEE TEENAGE YEARS TUMESHAPITA SASA HIVI TUPO KAMA MANG'OMBE YANAYOSWAGA KUONYESHWA MUELEKEO.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…