Tanzania bado changa sana, hata hatujafikia teenage years

  • Ukweli ulio mchungu ni kwamba hakuna mtu yoyote yule - awe kiongozi, raia, hata kichaa - aliye tayari kukata tawi alilokalia.
  • Hata huko 'duniani' tunakokuangalia haiwezekani au J. Biden, B. Johnson, Sholz n.k aliye tayari kupitisha sera zitakazoathiri maslahi yake, familia yake au 'wadhamini' wake. Never!
  • Ni muundo tu wa kitaasisi kuwezesha sera na utekelezaje wake
 
Ndio pale pale nikasema inabidi sisi wananchi tukubali hatuna akili ndo maana viongozi wetu wako namna walivyo...maana hawa viongozi ni wananchi pia!
 
Mkuu, hakuna anayetaka kujitafuna, hilo ni kweli kabisa...lakini utawezaje kueleza pale nchi inachukua mikopo kwa ajili ya maendeleo, alafu watu wanapiga ma 10 percent mpaka hakuna kinachofanyika?

Wakati nchi inapata uhuru, kulikuwa na viwanda, mashamba, na taasisi kadhaa wa kadhaa za kuimarisha uchumi....pole pole wananchi tumeviua kwa kupiga ma percent kama yote.

Hiyo si ni sawa na kukata tawi ulilokalia mkuu?
 
Haya bana.... si ndio hao GEN Z wamelianzisha. Ukiskia vijana ndio taifa la kesho.

Miaka mingine 20 au 30 ijayo, kila atakayekuwa serikalini atakuwa mzalendo.

Kwa sasa bado utapya mlo ulioanzishwa na nyerere enzi za ujamaa. Tukumbuke viongozi wetu wa sasa wengi wao hawakuwahi kujua mafanikio. Maskini akipata lazma matako yalie.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…