Tanzania bado nchi masikini sana, kwa miaka 8 watanzania wameagiza magari 561,875

Nani kakwambia watanzania ni masikini?
Umasikini uo kwa mtu binafsi.
 
Hayo yanayouzwa humu humu yanayoka wapi?
 
Wewe ni zero brain.
Nchi inaundwa na watu na kama idadi kubwa ya watu wanaounda hiyo nchi ni masikini hiyo nchi itakuaje tajiri?
Okay big brain.
Na wanaotembelea ma V8 binafsi na serikali na hai waliiagiza magari laki sita unawaweka wapi.
 
Hivi hili suala la.kodi za magari kuwa sawa au zaidi na bei ya kununulia gari hakuna wakulisemea??

#MaendeleoHayanaChama

Hakuna. Nchi hii ni ya ajabu sana. Unataka maendeleo lakini vitu vya kuchochea maendeleo huvipi vipaumbele, unavipiga vita, unavikwamisha kwa makusudi kabisa.

Kuweka kodi kubwa kwenye magari, mafuta, mbolea, tozo, kwenye miamala, luku jitihada za serikali kupunguza Kasi ya maendeleo ya watu ili kuwafanya wabaki maskini.

Serikali yetu inaonekana inapambana Sana kupunguza Kasi ya maendeleo Kwa Mtanzania kupitia sera, Kodi, tozo, vipaumbele visivyo rafiki wala kumsaidia Mtanzania zaidi ya kumkamua na kumrudisha nyuma kimaendeleo
 
Sana tutapokezana za humu humu ndani maana waagizaji watakuwa wachache.
Fikiria Fuso ya mwaka 1988 kuiingiza nchini ujipange na pesa si chini ya million 75+. Je ya mwaka 2012 utailipia pesa ngapi.[emoji28]

Ukiangalia daladala nyingi, gari nyingi Tanzania zimechoka balaa. Ajali nyingi zinasababishwa na gari zilizochoka.
 
Kwa ulimwengu wa SAsa ant dumping ni useless principal.sababu antidumping uja kumezwa na scrapping principal yaani kitu au gari likifika mwisho linaenda screpa kukatwa chuma chakavu then linarudi kiwandani kama raw materials ya kuzalisha tena gari.
Yangebaki huko wanakozalisha
 
Umesahau kwamba mpaka miaka ya karibuni piki piki na magari yalikua yana share number. Means kama ingekua kama sasa kwamba gari zisimame zenyewe inawezekana namba E ingesogea mpaka miaka 4 mbele, so piga hesabu upya.
 
Wahuni hawapunguzi kodi kila kukicha wanaona gari ni anasa na pia wale madarali wa Toyota wanawapiga kwa kuwauzia bei ya kilimo kwanza ambayo Nchi zingine hawaagizi kwa bei yetu wao wanaona sawa maana wapo wanaokula 10% kwa Serikali kupigwa..Nimeona pale Kasumulu mpaka wa Malawi gari za kumwaga na matoleo ya sasa hivi kwa sababu ya kodi yao ni rafiki gari ndogo halizidi Tsh 2m wakati hilo gari Tanzania ni 12m kodi yake...
 
Kununua gari ndo dalili ya ukwasi wa mtu binafsi?
Shule umetoka lini?
Umeshawahi kufanya kitu kinaitwa wealth ranking huko kwenye vijiji au mitaa yetu?? Ukitaka kujua economic status ya jamii fulani unaipimaje kama siyo kutumia vigezo vya mtu kumiliki vitu??
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…