SoC02 Tanzania bila ajali inawezekana

SoC02 Tanzania bila ajali inawezekana

Stories of Change - 2022 Competition

munemod

JF-Expert Member
Joined
Jan 17, 2017
Posts
224
Reaction score
590
Habari wanajamvi.

Nimekaa na kutafakari ongezeko la àjali za baràbarani ambalo limeikumba nchi yetu. Ajali ambazo zinagharimu maisha ya watu, uharibifu wa Mali na miundombinu, huku zikiacha idadi kubwa ya walemavu, yatima, wajane na wategemezi. Ajali zinazorudisha nyuma maendeleo ya familia na taifa kwa ujumla.
Baada ya kufikiri niakaona nije na bandíko hili ambalo litaleta tafakari ndani ya fikra zetu.. Andiko ambalo litatukumbusha namna gani kosa/makosa yetu au wengine yanaweza gharimu maisha, furaha na maendeleo ya wengine. Nitasimulia visa vichache nilivyoshuhudia na namna vilivyobadili fikra zangu juu ya ajali za barabarani.


Ajali iliyobadili maisha yangu.
Baada ya kupungua kwa hofu ya corona nilisafiri toka dar kwenda songea. Kwa hakika gari nililopanda lilikuwa linaendeshwa kwa mwendo kasi sana. Niwe mkweli, sio Mimi wala abiria yeyote aliyekemea mwendo huu. Kwangu Mimi wakati huo huyu dereva nilimuona kama shujaa, tena fundi ambae angetufikisha songea mapema sana. Baada ya giza kuingia tukiwa tumevuka namtumbo tunaifukuzia songea Mara tukashtushwa na kelele za abiria walioko mbele, kuja kutahamaki gari likaganga gari ndogo iliyoingia barabarani ghafla. Gari yetu ikaanza kuyumba. Hakika hakuna kipindi kigumu maishani kama wakati wa ajali.

Tukawa tumechanganyikiwa, gari iko spidi, inayumba, hatujui kama itasimama au itapinduka na kama itapinduka itapinduka upande gani na Mara ngapi. Baada ya muda gari ikaingia mtaroni na kubinuka, abiria na vitu tukarushwa. Nilifunga mkanda, nikawa naning'inia kawa mtoto anapopimwa uzito kliniki. Tukaja okolewa, majeruhi wakakimbizwa hospitali. Mimi kwa wakati huo nilikuwa nimechanganyikiwa nikajibu niko sawa, baada ya kuandikisha taarifa kwa askari, tukapewa gari ya serikali itufikishe songea. Mizigo na vingene havikuweza tolewa mpaka gari lilipoinuliwa siku iliyofuata.

Baada ya kuamka, nikagundua ule mkanda umeniumiza sana tumboni, na mguu wangu umeumia. Nimeangaika sana kutibiwa na mpaka sasa japo no zaidi ya miaka miwili ila bado athari hazijaisha.

Uzembe wa huyu dereva kuingia barabarani bila taadhali ulitugharimu, pia kama gari yetu ingekuwa katika mwendo wa kawaida tungeepuka janga hili kwani dereva angeweza simama. Ukimwa wetu abiria juu ya mwendo umetugharimu.

SOMO: Usiwe sababu ya maumivu kwa wengine. Endesha kwa uangalifu, chukua tahadhari unapotaka kuingia barabarani kuu. Huyu mama anaweza kuwa na amani aliko lakini waathirika hatuwezi sahau maumivu na mateso aliyotupa maishani.


Msiba wa bodaboda.
Hiki ni kisa kingine. Kilitokea kibada baada ya bodaboda kugongwa na gari ndogo. Dereva wa gari alikuwa amelewa kwa taarifa nilizosikia msibani. Nilikuwa kati ya waliohudhulia mazishi ya huyu baba kwa kuwa alikuwa anaishi jirani na ninapoishi.

Hakika nilikuwa huzuni kubwa kuwatazama wanae wadogo ambao hawakuwa wanaelewa hata kilichoko mbele yao, maana licha ya watu kujaa na huzuni wao walikuwa bize na michezo. Starehe ya mtu mmoja, zimeacha wajane wawili na watoto yatima.

SOMO:usiendeshe ukiwa umelewa. Kwani kilevi kinakufanya usiwe na maamuzi ambayo ungeyafanya ukiwa na akili za kawaida. Starehe zako zinaweza gharimu maisha yako au ya wengine, pamoja na furaha na maendeleo ya wengine. Wafikirie wanao na wategemezi wako namna wataishi ukiwa gerezani, wafikirie yatima na wajane watakaoachwa hapa duniani wataishije.


Kisa cha kulala njombe
hii iliyokea wakati naenda songea miaka mingi iliyopita. Mwanzo wa safari hadi mwisho sitaki kuukumbuka kwani ni kwa neema tu za Muumba tulifika salama. Tulipofika makambako tulikamatwa baada ya kukaguliwa gari ilionekana ni mbovu, hasa upande wa taa. Tukaamliwa kulala njombe, gari lisitembee usiku. Ukatokea mzozo abiria , dereva hatutaki kulala njombe. Yule kamanda akashikiria msimamo wake kuwa kulala njombe ni amri sio ombi. Mwenye haraka apande usafiri mwingine lakini lile gari halina taa sio salama kusafiri usiku. Tukalala njombe kwa shingo upande.
LEO, ningependa kumpongeza afande huyu. Aliwajibika na alituepusha na kuwaepusha wengi na janga ambalo lingeweza tokea. Japo tulimuona mbaya lakini hakika alitenda jambo jema. Ajali sio lelemama jamani. Ajali inatisha.

Hitimisho.

1.
Abiria tusifumbie macho uvunjwaji wa sheria barabarani. Mwendokasi sio ushujaa. Tuache kusifia madereva waendeshao ovyo na kuvunja sheria. Tekemee mwendokasi.
2. Wananchi, unapotembea kwa mguu au baiskeli fuata sheria za usalama.tembea upande wako. Usiingie wala kuvuka barabara bila tahadhari. Kosa lako linaweza gharimu wengine au wewe mwenyewe
3. Madereva, unapobeba abiria tambua umechukua dhamana ya kubeba roho za wengine. Fuata sheria, zingatia usalama. Usiendeshe umelewa, kosa lako ni mauti kwa wenzako. Kuwa makini na chukua tahadhari ili ikitokea dharura ya mtu/kitu au gari kuingia barabarani ghafla uweze kuepusha ajali.

4. Askari, walipoitwa askari wa usalama hawakukosea. Msiwe askari wa mapato barabarani. Kipaumbele chenu kiwepo katika kusimamia usalama zaidi kuliko mapato. Waelimisheni madereva na wananchi juu ya sheria. Watu hasa watoto wa shule wanaelewa kuwa wanatakiwa kuvuka katika pundamilia ila je wanaelewa kuwa sio kila wakati ni haki yao kuvuka? Kuna wakati taa zinaruhusu magari ila abiria hulazimisha kuvuka kwa kuwa pana pundamilia.

Simamieni sheria, epukeni rushwa. Uzembe wenu unaweza ligharimu taifa.
5. Serikali, wananchi wanalipa kodi. Ni haki yao kupata huduma. Miundombinu salama ni haki yao. Ni aibu kukaa ofisini ukila hela ya walipakodi huku wao wakifa katika ajali zilizosababishwa na ubovu wa barabara.

Tubadilike, kila mmoja akitimiza wajibu wake tunaweza tokomeza ajali Tanzania. Mimi kama mwananchi nakemea madereva wavunjao sheria. #sitokaakimya #tanzaniabilaajali #tanzaniasalama #nitatimizawajibu #ziroajali
 
Upvote 0
Wanajamvi, kama kuna makosa ya kisarufi mtanisamehe, binadamu hukosea. Kubwa tubebe maudhui ya thread
 
Naweza nisionekane sana katika mjadala kutokana na kukosa internet nilipo ila nitajitahidi kila niwezapo. Tuungane pamoja kutokomeza ajali. Twende na hashtag #ziroajali. Tupeane visa ili tujielimishe
 
Pia ningependa kuchukua nafasi hii kuomba kura zenu wapendwa
🙏🙏
 
Back
Top Bottom