Tanzania haina Mapato ya kubeba ongezeko la Mishahara yote kwa asilimia 23.3%

Una akili timamu kweli? Average ya makusanyo kwa mwezi ni zaidi ya Til.1.8 ,mtoa mada kasema ni til.1.5 unaona yuko sawa?

Pili je Uchumi umesimama au unashuka au uko stagnant?

Muwe mnafikiria kabla ya kuropoka.
Inawezekana ukatoa hoja kinzani na mwenzako bila hata kumtusi.....hapa ni jukwaani na kila mtu anatoa maoni kulingana na mtazamo wake...lakini wakati mwingine unaweza kwenda kombo kimitazamo na mwenzako akakurekebisha......
 
Umekariri makaratasi bila hata kujua chanzo cha hiyo inflation..

Turkey kwa mfano inflation ilikuwa 55% na Rais kaongeza minimum wage kwa 50% ..

Ni hatari sana kwa Taifa kuwa na wanaojiita wanauchumi waliokariri vitabu bila kuwa na uwezo wa kuchanganua..

Nikuulize je inflation ya Tanzania imesababishwa na nini? Je husikii kwamba pesa haipatikani mtaani? Unajua sababu?
 
Kulikuwa na maneno humu wakati wa hayati JPM kwamba jamaa wa TRA wanapika data za kodi. Awamu hii michezo hiyo imekwisha?. maana sisikii tena hizo lawama.
 
Inawezekana ukatoa hoja kinzani na mwenzako bila hata kumtusi.....hapa ni jukwaani na kila mtu anatoa maoni kulingana na mtazamo wake...lakini wakati mwingine unaweza kwenda kombo kimitazamo na mwenzako akakurekebisha......
Wakati mwingine kuna watu wanapotosha makusudi ilhali ukweli wanaufahamu..
 
Yeye alizibiti mfumuko wa vitu muhimu, baada ya miezi miwili huduma muhimu zitakuwa juu, mfano Hospital galama Zita panda, bill ya maji, umeme, Kodi ya Nyumba.
Unapiga ramli au? Serikali ipandishe gharama za Huduma za jamii kivipi ikiwa imeshusha gharama za Huduma hizo?
 
Hata miradi ya sasa hakutakuwa na pesa ya kuiendeleza. Yote itakufa.

Tutachukua mikopo kulipia hili tangazo.
Ramli haziwezi kukusaidia,cha kukusaidia tuu ni kwamba Samia ni akili kubwa na Serikali ina pesa..

Tafuta wizara yeyote ya Jiwe ambayo imewahi fikia utekelezaji wa bajeti kama hivi 👇

 
Kanuni ya kukokotoa ni kupunguza asilimia kadiri unavyota kwenye minimum wage kwenda salary ya Juu.
 
Hujui kitu
 
Wewe umejaa usaha kichwani..

Kwa hiyo bajeti ya serikali inasema uongo sio?

Lini Samia aliwaambia wafanyabiashara wasilipe Kodi? Unapotosha kwa maslahi ya nani?

Wapi ambapo Serikali imekwambia imeshusha Mafuta kwa sh.29? June mosi imefika?

Kama Serikali inasema uongo,hii efficiency inatoka wapi? 👇



 
SGR haijamalizika, Stigler bwawa sijui Nyerere Hydropower haijamalizika, na miradi aliyoiacha mwendazake haijamalizika, unataka ianzishwe mingine? Tumalize hiyo kwanza
Sio tuu haijamalizika aliacha hiyo miradi ikiwa inatekelezwa kwa kusua sua kwa sababu hakuna pesa..

Sasa hivi miradi inatekelezwa kwa Kasi na miradi mipya mingi inaenda kuanzishwa kuanzia mwaka huu, miongoni mwazo ni hii hapa kwenye sekta ya maji👇



 
Watanzania NI watu waajabu sana yaani kupata haki zao wanaanza kumpongeza mtu ,Baba yako kununua unga unampongezeee tunasafari ndefu
 
Tuonyeshe mapato yalivyopungua
 
Kwanini mmetoa ruzuku kwa wakulima ambao ndio wengi 70% ya Watanzania.

Mshaurini vizuri SSH kwenye vikao vyenu. Kukuza uchumi kwa kasi punguzeni kodi, ukiritimba, milolongo, biashara zitashamiri.
Haya yote Rais anayajua tena haishii kusikiliza wasomi tuu bali anasikiliza watu wa biashara TccIa..

Muwe mnapenda kufuatilia bajeti za wizara,mtapata mrejesho wa utekelezaji wa bajeti na mipango mipya..
Mathalani bajeti ya Kilimo ijayo serikali itafuta tozo lukuki kwenye sekta za maziwa nk..

Kana kwamba haitoshi Watu wako makini 👇

 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…