Tanzania haina Mapato ya kubeba ongezeko la Mishahara yote kwa asilimia 23.3%

Tanzania haina Mapato ya kubeba ongezeko la Mishahara yote kwa asilimia 23.3%

Mkuu yule aliyepita ambaye nafikiri ndio mnamuona alikuwa sahihi alishawahi kuwajali hao wakulima unakwasema hapa?

Lakini pia, unataka kuniambia kwa njia yoyote ile serikali inakosa/itakosa nyongeza ya Billion 130 kwa mwezi ya hii nyongeza ya mshahara? Kama bwana yule aliweza kilipa trillions ndani ya mwaka kwa ajili ya ndege tena Cash kwanini nyongeza ya mshahara kwa wafanyakazi inakuwa nongwa?

Au hii ni vita tu kwakuwa yule hakuongeza na mnaona kama legacy yake inachafuliwa??
Ndio aliwapuuza kabisaa,ni katika kipindi chake ambako sio tuu alikuwa hatengi pesa za kutosha kwenye wizara ya kilimo bali hata kiduchu zilizotengwa zilifika chini ya 40%..

Ni katika kipindi hicho Mazao mengi yaliporomoka bei na yakaacha kuuzika kwa sababu aliharibu mnyororo wa biashara..

Sasa ndio mama anahangaika kufufua..
 
Sasa hivi serikali inalipa wafanyakazi wake 500bn kwa mwezi.

Tu assume serikali iwaongezee kila mfanyakazi wake 50% ya mshahara wake.

Hii ina maana wage bili itakuwa 750bn kwa mwezi.

Je serikali haiwezi kupata hiyo 250bn kwa mwezi?
Kwa nini u'assume kwamba mfanyakazi ataongezewa 50% ya mshahara wakati serikali imesema ni 23%

Na hiyo wage bill umeipata wapi?
 
ili nchi inayoendelea ipige hatua inahitajika Kufanya Developmental expenditures nyingi (Miradi ambayo italeta faida kwenye long run) na sio kuzidisha recurring expenses (wages & salaries) ambazo hazina tija sana in a long run

knowledge ya kawaida tu, kama kijana wa kawaida nlivyoskia hivyo nkashangaa considering hali ya uchumi ya sasa “God have mercy on us”
Habari za huko? Wale wanyama wanaendeleaje? Habari ya Ile airport ? Mpaka Sasa imeingiza watalii wangapi?

Sent from my TECNO BA2 using JamiiForums mobile app
 
Vita gani tena. Vita iko Ukraine. Hapa tunachambua vitu kama watu huru.

Kuhusu wakulima hata JPM alikosea sana infact serikali zote toka awamu ya pili hazijawahi kumsaidia mkulima kwa dhati.

Nilimkosoa sana JPM kuhusu kilimo, kodi, mazingira ya biashara. Alikuwa vizuri sana kwenye miundombinu kama maji, umeme, barabara. Nidhamu serikalini, kuthibiti mfumuko wa bei, kwa hayo tulimpongeza.

130bn kwa mwezi kwa mwaka ni kiasi gani? 1.5Trillioni permanent imeongezwa ndani ya matumizi ya serikali. Kwanini usingeongeza kidogo kidogo, manageable sums of money say 5%, kila mwaka unaongeza uchumi ukikuwa unaongeza zaidi.

Kulikuwa na ulazima gani kuondoa ruzuku kwenye pembejeo, kuweka tozo mbalimbali?

Kwanini bwawa la umeme kasi imepungua ya kulimaliza,? Ingeleta tija, faida kubwa sana kwa taifa.

Faida hizo ni kama watu kujiajiri, viwanda kujengwa,unafuu mkubwa wa maisha kwa Watanzania wengi. SGR, maji,kodi,barabara, mazingira mazuri ya biashara elimu hivi vitu ndio vinaifungua nchi.
JK alijitahidi Sana kwenye kilimo kuliko Rais yeyote..

Sio tuu alitoa ruzuku lakini alikuwa anataka ku transform kilimo kuwa cha kibiashara kwa kutumia kauli mbiu ya kilimo kwanza na Kwa kuungwa mkono na wadau wa sekta ya kilimo kupitia program za Feed the Future,Agra,Saggot nk..

Samia yuko kwenye uelekeo huo ndio maana next budget ame priotise irrigation,Mazao strategic na mbolea.

Ruzuku kwenye mbolea alifuta Mwendazake.

Wafanyakazi hawajaongezewa salary kwa miaka 7 kwa hiyo ulazima ilikuwepo na Kwa kufanya hivyo tunaingiza pesa kwenye mzunguko ambapo unaongea consumer demand ambayo ni muhimu sana kwa ajili ya ku boost investment/production..

Hili la Kasi ya kupungua kwa ujenzi wa Bwawa unaweza thibitisha? Taarifa za Serikali ni kwamba Kasi imeongezeka kuliko awali na ujenzi uko zaidi ya 50%..

Mwisho usijitoe ufahamu kwamba huelewi athari za vita na covid kwenye uchumi.
 
Wewe hujui kitu, tulia ! Hata maana ya bilioni huijui!
Angalia kupunguza Tshs.29 tu ya bei ya Lita Moja ya petroli ambapo zitahitajika Tshs.bilioni 100 imebidi Serikali kuomba mkopo WB.
Sasa itakuja kuwa 250 bilioni kila mwezi!!!
Nasisitiza HUJUI KITU, TULIA!
Haka ka 23.3% kanatoa watu roho! Kuna watu watakufa kwa pressure kisa wenzao wamefutwa vichozi !! Elewa kama hujapata wewe shangazi yako atapata...!!!!

Sent from my TECNO BA2 using JamiiForums mobile app
 
Hata miradi ya sasa hakutakuwa na pesa ya kuiendeleza. Yote itakufa.

Tutachukua mikopo kulipia hili tangazo.
Kwani wewe unajidanganya kuwa hiyo miradi ilikuwa ikijegwa kwa fedha za ndani! Duu! Kumbe bado ujinga mbao?


Amka toka usingizini ndugu miradi yote mikubwa, mwendazake iliijenga kwa mikopo mikubwa ya kibiashara ya riba kubwa na Hadi Sasa umeshaanza kulipa riba hiyo.
 
Akili ndogo,hapo unadhani sasa kwamba Mimi napinga nyie kuongezewa Mishahara! Utapata akili pale utakapokuta Mshahara wako umeongezewa elfu 10 na wewe kuchekelea asilimia 23.3% ambayo ni kwa kima cha chini ambacho wewe haumo!
UJINGA NI MZIGO MZITO SANA KWA BINADAMU!
Kama hayupo kima Cha chini atakuwa Cha kati au Cha juu. Mchukulie anapata tsh400,000na nyongeza kwa ngazi yake iwe 15% atapata ext 60,000 anayepata 5,000,000 na nyongeza ya 1% bado ataongezewa 50,000/-

Sent from my TECNO BA2 using JamiiForums mobile app
 
Kukuza Uchumi hakuhitaji rocket science ila nashindwa kuelewa viongozi wetu wanafeli wapi…

Nchi za kiafrika zinajitaji viongozi jasiri na madikteta siasa na demokrasia ndio umaskini wetu….bila hivyo hatutoboi…
Nguruwe akizidiwa njaa, wanawe hugeuzwa kitoweo. Beware udikteta ni maafa kwa taifa!!!!!!!

Sent from my TECNO BA2 using JamiiForums mobile app
 
Ndio maana nimekwambia ongea na wenye mamlaka watakwambia pesa watatoa wapi.
Upo karibu naye mshtue. Huwezi kusimama ukawaambia wananchi wa USA, UK Sweden, nchi yoyoye inayojitambua nitaongeza hivi bila kusema vitatoka wapi? Watakutoa serikalini siku hiyo hiyo. Everything must, need to be costed.

Hivi balance sheet yetu ya TZ ikoje? kikaratasi cha kuonyesha mapato, matumizi, assets, liabilities, mikopo. Uwiano wa mapato matumizi, mikopo umekaaje?
 
Na inflation inasemaje huko vs ongezeko la mshahara kwa watumishi? Halafu msifikir ni watumishi wa serikali tu ambao hawafiki hata laki tano ndio wenye wako entitled na hii nchi.
Hapo wapo madaktari waliokutahiri, na kukuandikia dawa za minyoo. Kama wamekusaidia hivyo unaona uchungu Gani wakilipwa kwa huduma njema walizokupatia?

Sent from my TECNO BA2 using JamiiForums mobile app
 
Ukisoma vizuri kitabu cha WHY NATIONS FAIL ( The Origins of Power,Prosperity & Poverty) cha DARON ACEMOGLU na JAMES A.ROBINSON utajua kwa uhakika ni kwa nini Tanzania yetu ni masikini hivi na itachukua muda mrefu kubadili hali hii.

Kwa ufupi ni kwamba tunacho kila kitu kinachohitajika kwa ajili ya maendeleo katika Nchi yetu kasoro watu wenye maarifa na taasisi imara.

Hata watu wachache wenye maarifa tulionao pia wana maarifa yaliyopitwa na wakati (obsolete) au waliyo karirishwa tu! Tunaweza kusema maarifa yao hayo ni USELESS KNOWLEDGE tu.

Nchi bila uzalishaji na kuingiza Nguvu kazi kubwa katika uzalishaji ili kuongeza tija ni kazi bure tu.

Viongozi wetu na wachumi wetu waliwasoma akina Adam Smith kwenye THE WEALTH OF NATIONS kwa ajili ya kukariri kujibia mitihani tu!

Watu wetu hata wasomi wakubwa hawajui kutafsiri hata vitu basic kabisa!

Watu wanaambiwa kima cha chini la Mshahara kimeongezeka kwa asilimia 23.3% ,wao wanakimbilia Rais ameongeza Mishahara kwa asilimia 23.3% ( akili za Ki- Mwijaku Mwijaku)!

Jiulize kwanza kama Mishahara itaongezwa kwa asilimia 23.3% yote ,Wage Bill yetu itakuwa Shilingi ngapi?!

Wage Bill ikifika bilioni 900 kwa mwezi na madeni tunayolipa kwa mwezi ni bilioni 900 wakati Mapato yetu kwa mwezi Trilioni 1.5 ( bilioni 1500) Nchi itakwendaje?!

Ukitaka kujua Nchi hii ina tatizo kubwa katika Wealth Creation angalia utitiri wa tozo katika mafuta!

Kwahiyo ukifuatilia sasa mjadala ni asilimia 23.3% ya ongezeko la Mishahara ni kwa kima cha chini pekee au Mishahara yote!
Wewe ndo huna akili. Kwani umezaliwa lini.
Maana miaka yote serikali hutangaza nyongeza ya mishahara na kutaja kima cha chini, hayo madaraja mengine % inapungua as you go up.
Halafu kama tangu 2015 yule mwendakuzimu angeongeza 5% sasa hivi ingekua 30%.
Roho yako ya kisukuma inakutesa haikusaidii chochote mama ni mama tu na mambo yatakwenda vizuri kuliko enzi za wasukuma
 
Nibora hasinge ongeza mishaara mfumuko wabei utakuwa mkubwa Sana vitu vita panda bei mfano Kodi ya Nyumba chumba cha 50,000 kitapanda mpaka 60,000.
Miaka yote mishahara ilikuwa inapanda.... Ni upuuzi uliofanywa miaka 6 iliyopita ndio kimewafanya muone kama jambo la ajabu. Nadhani Kuna haja ya kuwapa kaelimu kadogo ka uchumi ngazi ya chekechea na msingi. Hii itasaidia watu waelewe uhusiano kati ya mshahara na uzalishaji na ni namna gani vinavyotegemeana!!

Sent from my TECNO BA2 using JamiiForums mobile app
 
Wewe ilivyo kichwa maji unahisi Serikali huwa inaweka wazi mikopo yote! Huyo mama ameshakopa hela nyingi sana tokea aingie! Na kwa taarifa yako yale makusanyo ya TRA ni uongo ndo maana saizi wanakazania matumizi ya EFD lakini kipindi anaingia aliwaaminisha wafanya biashara wawe huru kuonesha yeye ni mshikaji! Na kingine umeona kwenye mafuta wameingiza bilioni 100 kushusha inflation lakini imeshuka sh 29 tu kwa lita! Imaonesha Serikali haina pesa! Brabra za wanasiasa tu!
Sasa si bora hata huyu ana yesema hata hiyo michache kuwa amekopa!!na yule aliyekuwa akiwaaminisha wajinga kuwa kila mradi ni pesa zao, kuwa Tanzania ni tajiri, huku deni la taifa likikuwa kwa kasi nani afadhari?!!eti wanakazania efd, kuna kipindi ambacho hizo efd zilikazaniwa na ubabe juu ili kuzinunua?!!alisema hawezi akatumia njia za kijambazi kama zile, .
Mwendazake ameliacha taifa ktk wakati mgumu sana, kwani alikuwa akianzisha miradi bila kuzingatia vipaumbele na uwezo wa kifedha.
Kweli mimi ni kichwa maji kama kilivyo kuwa cha jiwe(ambaye wewe ni muumini wake!!hivyo wewe utakuwa kichwa maji square!!
 
Vicious circle hiyo!

Bei za vitu ikipanda, dawa huwa ni kupunguza fedha mitaani siyo kuongeza. Mabenki hupandisha interest rates ili kupunguza fedha mitaani. Sasa wakati bei inapanda wewe unasema utaongeza fedha mitaani maana yake ni kuwa bei zinapanda maradufu.

Bei kupanda maana yake ni kuwa kuna fedha nyingi mitaani kuliko thamani ya bidhaa zinazouzwa, kwa hivyo bei inapanda ili thamani ya bidhaa iwe sawa na hela zilizoko mitaani. Hayo ni maelezo mepensi kwa lunga rahisi watu wa uchumi wanaweza kutoa details zake.
.
Wafanyabiashara wanadai wanalinda bidhaa hakuna wateja, wateja wanadai pesa hakuna mfukoni....!!

Sent from my TECNO BA2 using JamiiForums mobile app
 
Back
Top Bottom